Hadithi kali: Baniani mbaya.....

Mommadou Keita

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2013
Posts
230
Reaction score
238
BANIANI MBAYA…


NI asubuhi bado sijaamka kutokana na uchovu kwa sababu nilikuwa nimetawaliwa na hang- over ya pombe nilizokunywa usikuwa jana.


Nilikuwa bado nagalagala kwenye kitanda changu cha thamani ghafla simu iliyokuwa pembeni ya kitanda ikaita.
Nilipepesa macho na kuangalia katika screen ili kumjua mpigaji, moja kwa moja macho yangu yakakutana na jina la la baba yangu mzazi, mzee MziziMkavu.
Nilijaribu kufikisha macho kwa kiganja cha kulia cha mkono wangu kuhakikisha kama ni kweli mzee ndiye aliyekuwa kinipigia,.
Najishauri kwa muda kuipokea simu hiyo au kuacha maana nilikuwa najua kabisa alichokuwa akitaka kukisema.
Kipindi hicho nilikuwa na ugomvi na mzee huyo ambaye alikuwa akinitaka nifunge ndoa.
“Haloo baba…” niliipokea na kusema kwa sauti ya upole.
“Haloo mwanangu, hujambo?”
“Sijambo shikamoo…”
“Marhaba… eenhe, umefikia wapi?”
“Baba bado najipanga, sijampata mwanamke hasa ambaye nadhani anaweza kuwa mke wangu, nikimpa….,”
“Sikia MOMMAdou nadhani una baba mwingine ambaye unamsikiliza zaidi kuliko miye, nimeshakwambia hata huku Mwanza wanawake wapo, miye nimeshampata… Kama mpaka Jumamosi hutakuwa umefika Mwanza na huyo mwanamke anayekusumbua huko mjini, basi nitapeleka posa kwa mwanamke wa huku kijijini ili umuoe tofauti na hapo sitakuwa na radhi na wewe tena…” alisema kwa hasira.
“Lakini babaa….”
“Hakuna cha lakini huo ndiyo uamuzi wangu… nimemaliza hebu ongea na mama yako…” alisema na baada ya muda nikasikia sauti ya mama.
“Ng’wanone….” alisema kwa Kisukuma akimaanisha mwanangu.
“Eeeh Mayu…” (Eeeh mama) nami nilimjibu kwa lugha hiyohiyo.

“Ndegelekage ubhabha wako, ubhise ukukijiji kunu tutina lubhango tulitogwa tubhabhone abhizukulu bhise kabla tutinacha.(Msikilize baba yako, kwani siye hatuna amani huku kijijini tunataka tuwaone wajukuu zetu kabla hatujafa).
“Nahene mayu, nakwita chene.” (Sawa mama, nitafanya hivyo).
Baada ya mama kusema hivyo tukaagana na kukata simu.

PRETTA WANGU
Nikayazungusha macho chumbani kwangu, kisha nikatoka na kwenda sebuleni nikiwa kama vile naikagua nyumba yangu kama ndiyo kwanza nilikuwa nikiiona kisha nikawaza:
“Hii nyumba ya kukaa mwanamke wa kutoka shamba kweli,?” nikajihoji huku nikitafakari elimu yangu yangu yote ya Chuo Kikuu nikaoe mwanamke kutoka kijijini.
“Haiwezekeni…” nilisema kwa hasira huku nikitafuta njia za kuweza kumdhibiti mzee Mzizimkavu asiweze kuniingilia katika uamzi wangu wa kufunga ndoa na mwanamke ninayempenda kwa dhati.
Jina la pretta likagonga tena akilini mwangu, mwanamke ambaye ni msomi mwenzangu niliyekuwa naye pale Mlimani. Baada ya kumaliza chuo tukatengana kwa kuwa alipata chuo nchini Uingereza ili kuendelea na elimu ya juu huku tukiwekeana ahadi ya kufunga ndoa.
Katika akili yangu niliamini kabisa mwanamke huyo ndiye haswa anayeweza kuingia ndani ya nyumba yangu na kunizalia watoto wenye akili lakini wazazi wangu hawataki kusikia habari za mwanamke anayesoma nje ya nchi.
Baada ya kujiandaa nikatoka nyumbani kwangu Kijitonyama jijini Dar, nilipofika nje nikawasha sigara yangu ambayo niliamini kabisa kwamba inaweza kunipa fikra za kuyatafakari maneno ya mzee Mtimkavu.
Nikatoka hadi katika baa ya Hongera ambayo hata usiku wa jana nilikuwa hapo nikinywa sambamba na marafiki zangu Mentor, cha arusha, TUKUTUKU, Bitilanga na kinubi.
LOVENESS
“Wee mwanaume ….” Sauti ya kike iliniita pembeni, nikageuka na kumwangalia alikuwa ni Loveness mhudumu aliyeanza kazi katika baa hiyo hivi karibuni.
“Unasemaje…?”
“Juzi wakati ukiondoka hukulipa pesa za sigara…” alisema.
“Usiwe na wasiwasi nitakulipa… utaiongezea kwenye bili yangu ya leo,” nilimjibu huku nikiwa sina uhakika kama kweli alikuwa akinidai au ni ujanja wake wa kujipatia fedha zaidi kutoka kwangu.
Nawajua mabaameidi wengi wao ni wajanja wajanja sana na maisha yao ni ya kuungaunga kutokana na mshahara midogo wanaolipwa, fedha nyingi wanategemea kuzipata kutoka kwa wanaume hasa wale wanaolewa na kutokuwa na kumbukumbu ya matumizi yao.
“Haya mpenzi leo utakunywa nini…?” aliniuliza Loveness huku mshipa wa fahamu ukiwa haunishtuki kwa kuniita jina hilo la mpenzi kwani miye ni mlevi wa aina yake niko tofauti na walevi wengine.
Binafsi nina msimamo sana katika masuala ya wanawake, na wanawake sumu kwangu ni mabaameidi, siwapendi hasirani na katu siamini kama kweli mtu mwenye akili zake anaweza kuwachukua na kwenda kulala nao.
Ninachoamini ni kwamba wengi wa mabaameidi wana tabia mbaya na hawafai kuwa wake za watu.
Ndiyo maana nasema kwamba miye ni mlevi wa aina yake kwani hata nilewe vipi siwezi kuondoka baa nikiwa naambatanana baameidi kwenda naye nyumbani kwangu hata kama nimeshikika kwa kiasi gani … siwezi kugonga shoo na baameid, miye ndiye Mommadou Keita… siwezi kamwe kufanya upumbavu huo!
Naamini hata walevi wenzangu huwa hawawapendi mabaameidi kabla ya kulewa, kwa kuwa huwa wanawaona wabaya lakini kadiri kiwango cha pombe kinavyoongezeka akilini mwao ndivyo wanavyobadili mawazo na kuwaona wazuri.
Tofauti na miye kila kiwango cha pombe kinapoongezeka ndivyo ninavyozidi kuwachukia.
“Baby nikuletee nini?” alisema tena Loveness na kunitoa katika lindi la mawazo.
“Aaah nipatie mchemsho wa kuku… kisha niongeze na bia moja…” nilisema na kumfanya Loveness aondoke kwa madaha huku akitingisha umbile lake akidhani labda anaweza kunitega.
Hakuniuliza aina ya pombe ninayotumia kwa kuwa kila mhudumu katika baa ile anakijua ninachokunywa.
Ghafla mawazo yakarudi kwa baba yangu mzee mtimkavu, nikawasha sigara nyingine na kuivuta huku nikitafakari.
MKAKATI NA BANIANI
“Yeye anataka nimpelekee mwanamke ambaye atakuwa ni mke wangu, mwanamke nitakayefunga naye ndoa baada ya yeye kumuona na kukubaliana na tabia zake…” nikajisemea kimoyomoyo huku nikiuachia moshi wa sigara hewani.
“Yap nimepata wazo….,” nilijisemea huku akili ikinituma kwa Loveness kwamba angefaa kuwemo katika mkakati wangu wa kumwingiza mjini mzee mtimkavu na kisha kuendelea kumsubiri pretta wangu.
Iko hivi, kwa kuwa mabaameidi ni wanawake wasiokuwa na heshima mbele ya jamii, nikimchukua Loveness kwa malipo na kwenda kumtambulisha kijijini kwetu, nitakuwa nimefanya jambo la kuwatuliza wazazi wangu.
Lakini kutokana na tabia mbaya za wanawake hao, Loveness ataharibu tu mbele ya mzee mtimkavu kisha hatamkubali mwanamke huyo lakini atashindwa kuniambia, nitakaporudi Dar na kumwambia nimemuacha mwanamke huyo atafurahi na muda huo pretta wangu atakuwa amerejea.
“Hapo nitakuwa nimepata muda mwingine wa kumsubiri pretta wangu na kila kitu kitakuwa kimekwenda sawa,” niliwaza.
Nilishtuliwa na Loveness aliyekuwa akiweka supu ya kuku na kinywaji juu ya meza yangu.
“Leo unaonekana uko mbali sana kwa mawazo…” alisema .
“Eeeh, tena kuna mchongo mmoja wa kuingiza pesa za harakaharala nataka nikushirikishe… sijui utauweza…?” nilimwambia.
“Mchongo gani tena MOMMA…” alilikatisha jina langu kama wengine wanavyofanya huku akibana sauti na kunifanya niinue macho na kumwangalia.
“Mzee wangu ananisumbua sana, anataka nioe… sasa unataka nikufanye wewe ndiye mchumba wangu tunaenda Mwanza kisha tukirudi Dar kila mtu kimpango wake…”
“Eeeh kwani mpaka leo hujaoa…?”
“Hilo halikuhusu, sikiliza kile ninachokwambia…” nilimkatisha.
“Makubwaa…” alisema .

“Sasa nataka tufanye hivyo… nitakulipa fedha yoyote utakayotaka,” nilimwambia Loveness huku nikimkazia macho kumuonesha kwamba sikuwa nikitania kile nilichokuwa nikikisema.
“Hiyo safari ni lini…?”
“Leo Jumatano, Ijumaa tunapanda ngege hadi Mwanza..unasemaje kama huwezi sema nimtafute mtu mwingine?”
“Kwa kuwa sasa niko kazini, tutaongea baadaye kwa kina?”
“Powa…” nikamaliza supu yangu huku nikiamini kabisa kwamba Loveness hataniangusha kwa kuwa yuko mjini kwa ajili ya kutafuta fedha.

Akili yangu ikatulia, nikaamini kabisa kwamba sigara kilikuwa ni kitu muhimu sana maishani mwangu, kwani mawazo yote niliyapata baada ya kuchangamsha akili yangu kwa kuvuta sigara.
Nikanywa kinywaji changu kisha nikaongeza na kingine na kingine, nikamuaga Loveness kwa ahadi ya kuonana jioni ya siku hiyo atakapotoka kazini.
Jioni nilifika katika baa hiyo mapema sana tofauti na siku nyingine ili kuweza kumalizana na Loveness.
MIMI NA BANIANI
“Hiii ishu tusiiongelee hapa,” alisema na kunitaka kutangulia nyuma ya Chuo cha Ustawi, nikatangulia lakini sikuona sababu ya kukaa chobingo na mwanamke huyo, nikatamka twende nyumbani kwangu kabisa jambo ambalo aliliafiki.
Tuliambatana hadi nyumbani kwangu.
Loveness alishtuka alipoingia sebuleni kwangu, nadhani hakutegemea kama angeweza kukutana na samani alizozozikuta, zuria lililotoka Uarabuni, flat screen kubwa na redio iliyokuwa ikipiga nyimbo laini za kubembeleza.
Pamoja na kwamba nyumba hiyo haikuwa mwanamke wala msaidizi wa kazi lakini ilikuwa safi kitu kilichomwogopesha Loveness.
“Karibu…” nilimkaribnisha .
“Asante…”
“Utakunywa kinywaji gani…?
“Soda yoyote ile…” akasema na kunifanya nilifuate jokufu, nilipolifungua Loveness aliashangaa kuliona limesheheni vinywaji vya kutosha.
“Kwa nini huwa unakuja baa?” aliniuliza.
“Huwa nafuata kampani tu…”

“Ingekuwa miye nisingetoka ndani…”
Niliachana na mawazo yake na kumrudisha kwenye kile kilichotufanya tukutane pale, nikaanza kwa kumweleza upya mkakati mzima wa kwenda kumfunga mdomo mzee mtimkavu.
“Utanilipa kiasi gani…?” aliuliza.
“Laki tatu…”
“Ndogo, kazi kubwa hiyo… ongeza kidogo…”
“Laki nne na nusu…” nikaongeza naye akasema nimpe laki tano.
Kwangu haikuwa tatizo, nikamkubalia kwamba nitampa kiasi hicho.
“Leo utanipa nusu, tukirudi utanimalizia,
“Sawa…”
“Kwenu Mwanza sehemu gani…
“Geita…

“Nipe mchanganuo wa ndugu zako… yaani zaidi ya baba na mama kuna akina nani tena…?”
“Kuna mdogo wangu wa kike ana miaka 21 na mdogo wangu wa kiume ambaye ananifuata ana miaka 30,” nikamwambia na wajihi wa ndugu zangu hao.

SAFARI YA MWANZA
Asubuhi ya Ijumaa, tulikuwa ndani ya ndege ya shirika la ndege la Air Tanzania kwa ajili ya safari hiyo ya Mwanza.
Baada ya masaa mawili tulitua Mwanza mjini na baada ya hapo tukavuka Kivuko cha Kamanga kwenda Sengerema kisha tukapanda gari aina ya Toyota Land Cruiser ambazo ilitufikisha hadi Geita Mjini ambako nilikutana na mdogo wangu Masumbuko aliyefika kunipokea.
“Aaah kaka ni heri umekuja na huyu wazazi walikuwa wakitaka umuoe Kaulani…” alininong’oneza Masumbuoko baada ya kumuona Loveness.
Nilikuwa nikimjua Kaulani hakuwa mwanamke mzuri hata kidogo, kwanza darasa la saba kisha hakuwa na mvuto wowote zaidi ya sifa yake ya ukulima.
Masumbuko alikiri kwamba shemeji yake alikuwa mzuri kwelikweli kwa jinsi alivyotengeneza nywele zake na mavazi yake ya gharama aliyokuwa ameyavaa.
Tuliingia kijiji kwetu Nyamigota jioni na kupokewa na shangwe na baadhi ya ndugu waliokuwa na hamu kubwa ya kumuona mke wangu mtarajiwa, kisha Loveness akampa zawadi za vitenge na blanketi akampatia mama , baba akapewa koti lenye thamani.
Masumbuko akapewa mashati na dada yangu akapewa magauni mawili yaliyomkaa vyema.
Binafsi wala sikushtuka niliona ni jambo la kawaida sana kufanywa na Loveness kwa kuwa alikuwa ameuvaa uhusika haswa.
KASHESHE CHUMBANI
Giza lilipoingia niligundua kuwa nilikuwa nimepangiwa kulala chumba kimoja na Loveness katika nyumba mojawapo ya familia.
Sikushtuka kwa kuwa nilijiamini na nilihisi hata yeye alikuwa akijua kwamba hakuna kitu kitakachoweza kutokea kati yetu kwa kuwa hatukuwa wapenzi na wala hatukuwa na mkataba wa kufanya mapenzi.
Baada ya kulala mapema kutokana na uchovu wa safari, nilishtuka saa sita za usiku… nikageuza macho kumwangalia Loveness alikuwa amelala na night dress.
Mapigo ya moyo wangu yakaanza kunidunda mara baada ya kumwangalia umbile lake lililojichora vyema kwenye nguo hiyo.
Mh! Inatosha kukwambia kwamba Loveness alikuwa ameumbika, utadhani ndiyo kwan za nilikuwa namuona.
Tamaa ikaniiingia katika nafasi yangu kutokana na kibaridi kilichokuwa kikipiga usiku huo.
Pamoja na ustahamilivu wangu wote na ujanja wangu wote, lakini nilijikuta nikichemsha, mzee alikuwa akidai haki yake, nikajipa moyo kwamba ninaweza kupiga mara moja tu, kisha nitaachana naye na sitakuwa na habari naye tena.
Nikanyoosha mkono wangu wa kuume na kumgusa Loveness. Alikuwa na joto la ajabu.
Mwili wangu ukazidi kusisimka, nikashusha pumzi nzito nikasema misimamo mingine wakati mwingine inakuwaga haina maana.
Nikakaa vizuri na nikamvuta Loveness upande wangu, bila ya hiyana motto wa kike akasogea na kunigusa mwili wangu akiwa amejilegeza bila ya kutegemea tukaanza kupasha miili yetu kabla ya kuingia msambweni.
Baada ya dakika tano tulikuwa tukigonga shoo, ilikuwa shoo nzuri sana ambayo sikutegemea kuipata kutoka kwa baameidi.
Ilikuwa ni raundi moja tu, lakini ilikuwa na utamu wa aina yake, hakika Loveness alikuwa msafi na alikuwa akijua kufanya kile alichofundishwa na kungwi wake.
Mwanamke matata hata pretta wangu haoni ndani.
Lakini baada ya dakika tano ya tendo hilo nikakumbuka kwamba sikuwa nimetumia kondomu, hata hivyo nilijipa moyo kwamba kwa siku hiyo moja isingeweza kubadilisha chochote katika maisha yangu.
LOVENESS AJIPENDEKEZA
Nilishtuka kutoka usingizini saa mbili asubuhi, Loveness hakuwepo chumbani, nikatoka nje na kuulizia kwa watu niliowakuta, wakaniambia kwamba ameambatana na wazazi na ndugu zangu kwenda shamba.
Moyo wangu ukasema kitu: “Mwache ajipendekeze, tukirudi Dar nampiga chini namsubiri pretta wangu…”
Wiki moja ilikatika, nikawaaga wazazi kwamba kesho yake nitaondoka na mke wangu kurudi Dar lakini nilipata kipingamizi kutoka kwa Loveness ambaye alizungumza mbele ya wazazi kwamba yeye atabaki kwa kuwa kilikuwa ni kipindi cha mavuno, hivyo aliona bora awasaidie wazee kuvuna.
Bado niliona Loveness alikuwa akijipendekeza tu kwa wazazi wangu lakini niliamini kuwa alikuwa akiheshimu makubaliano yetu kwamba akirudi Dar kila mmoja anashika hamsini zake, pretta anachukua nafasi yake.
Kesho yake mi nikaondoka kurudi Dar huku nikimwachia Loveness nauli kwa kuamini kuwa kazi yake alikuwa ameimaliza vyema ila atakaporudi.
Sikuona sababu ya kutompa fedha zake, nikamwita pembeni na kumpa chake chote, tukawa tumemalizana.

KIZUNGUZUNGU CHA GHAFLA
Nilifurahi kwa Loveness kuendelea kukaa kijijini kwetu kwa kipindi kirefu kwa kuamini kuwa ataharibu kama nilivyokuwa nikiwaamini mabaameidi.
Miezi tisa ilikatika sikuwahi na mawasiliano na Loveness, nikajua labda alirudi Dar na kuhamia kufanya kazi sehemu nyingine.
Nilishaanza kusahau habari za mtu anayeitwa Loveness kagtika akili zangu.
Siku moja baba alinipigia simu na kuniambia kwamba mwenzangu amejifungua.
Nilishtuka!
“Amejifungua… nani…?” nilihoji.
“Eeeh amejifungua mapacha wa kiume, tena wanafanana na wewe kwelikweli…” alisisitiza mzee mtimkavu.
“Nani…?” niliuliza kwa ukali kidogo.
“Si mkeo uliyemuacha huku…” nilishtuka hapohapo Loveness akarudi akilini mwangu.
Nilikuwa kama nimezinduka katika ndoto ya muda mrefu na kusema “Kumbe Loveness baod alikuwa kijijini kwetu?”
Nihisi kama vile nilikuwa nikitaka kuanguka kwa kizunguzngu kilichonikumba ghafla.
Sikuweza kuendelea kuzungumza na mzee mtimkavu nikakata simu, pamoja na usomi wangu lakini siku hiyo nilijiuliza swali la kipumbavu
“Mimba inaweza kuingia kwa kufanya tendo kwa siku moja?”
Nilitafakari sana, sikupata jibu kwa kuwa watoto nilikuwa nawapenda na hawakuwa na makosa lakini kufunga ndoa na baameidi itakuwa shughuli… nikatafakari, je pretta akirudi atanielewa kweli…?
Sikujua hata cha kumwambia pretta wangu, nikabadili laini ya simu na kwenda Mwanza, nilipofika nilipewa sifa kedekede za Loveness na nikatakiwa kufunga naye ndoa.
Hivi ninavyoongea na wewe tayari tumefunga ndoa na Loveness, tuna watoto wawili ambao ndio waliosababisha nimuoe mama Loveness.
Sababu kubwa ni kwamba nimefanana na hao watoto mpaka basi, kweli nimeamini Baniani Mbaya lakini Kiatu chake Dawa…!



























 
Last edited by a moderator:
Hahahhaha, mommaaaa we noma kaka, nimeipenda hii senema, Bongo movie inakuhusu
 
Aisee Loveness ni nomaaa.....
 
barmaid teh teh ndege mjanja hunasa katika tundu bovu
 
tamu....aishih amu
 
Last edited by a moderator:
Weee MOMMAdou ni noma aiseee yule aliyekuwa akikuponda yuko wapi... unatisha mzazi kweli unastahili pongezi.
 
Last edited by a moderator:
Aisee!!!! very nice story, short and Clear, Asante sana umeifanya asubuhi yangu kuwa njema maanake nilikuwa very stressed. Big up MOMMA !!!
 
Last edited by a moderator:
Hiii hadithi nilishaisomaga zamani kidogo ila sikumbuki ni lini. All the same thanks for bringing it up once again
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…