Hadithi: Jimama la supu ya pweza

Hadithi: Jimama la supu ya pweza

salehek

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2014
Posts
268
Reaction score
305
Jimama La Supu ya Pweza-1
“Mama Sabinamu, hujambo mke
wangu?”
“Sijambo mume wangu. Vipi kazi?”
“Kazi njema. Upo nyumbani?”
“Ndiyo mume wangu.”
“Eee, nenda kwenye kalenda ya
ukutani, funua nyuma kabisa, kuna
namba za simu nimeziandika,
nitumie sasa hivi.”
“Sawa mume wangu,” alijibu mama
Sabinamu huku akikata simu.
***
“Kwa hiyo ndugu zanguni, kama
nilivyokwishasema, subirini ije hiyo
namba tumpigie Ngoswe,
atakachosema ndiyo tutakuwa
tumepata majibu,” baba Sabinamu
aliwaambia wageni wake.
***
Mama Sabinamu alimwamuru dereva
wa Bajaj aendeshe kwenda mbele
baada ya kumsimamisha pembeni ya
barabara ili aongee na simu na
mume wake.
Aliiseti simu vizuri, akaipiga...
“Jema, umeshatoka kwenye maji?”
“Ndiyo mama.”
“Haya, nenda sebuleni, fungua
kalenda, nyuma kuna namba za simu,
nitumie sasa hivi,” mama Sabinamu
alimwambia msichana wake wa
kazi.
“Sawa mama.”
****
Msichana wa kazi alikwenda kwenye
kalenda hiyo na kufunua nyuma
ambapo alikutana na namba kibao...
“Khaa! Sasa mbona namba ni nyingi
sana?” msichana wa kazi alijiuliza,
akawaza kumpigia mama Sabinamu.
“Mama, mbona namba zipo nyingi?”
“Zipo nyingi?”
“Ndiyo mama.”
“Nitumie zote.”
“Haya.”
****
Baba Sabinamu alipoona dakika saba
zimekatika bila kutumiwa namba
hizo alimpigia tena mkewe lakini
hakupokea, akakasirika kwani
alikuwa akiisubiri sana namba hiyo.
Mama Sabinamu baada ya kutumiwa
namba zote, na yeye alizituma kwa
mume wake akamsindikizia na
ujumbe uliosema...
“Nimekuta namba nyingi, nimeona
nikutumie zote.”
Baba Sabinamu alizidi kukasirika,
akampigia...
“Halo mume wangu...”
“We mama Sabinamu una akili
kweli?”
“Kwa nini?”
 
Jimama la Supu ya Pweza
Mama Sabinamu alikuwa na usafiri,
yaani gari lakini kwa safari zake za
mbali na haramu kama hizo
hakupenda kulitumia kwa sababu
mumewe akirudi na kukuta gari yeye
husingizia alikuwa jirani tu.
JIRUSHE MWENYEWE...
“Haloo Jema, hebu tungua hiyo
kalenda hapo ukutani, kisha chukua
bodaboda kimbia unikute hapa
Shekilango.”
“Sasa hivi mama?”
“Asa ingekuwa baadaye
ningekwambia uchukue bodaboda?”
“Sawa mama, nachukua nakuja.”
“Haraka.”
Mama Sabinamu alishuka na
kusimama kwenye supermaket moja
iliyopo Shekilango akimsubiri
msichana wake wa kazi afike na
kalenda.
Kila baada ya dakika moja alikuwa
akimpigia simu na kumuuliza aliko...
“Ndiyo tunapita Kijiweni mama.”
“Haraka.”
“Sawa mama, lakini siendeshi mimi.”
Mama Sabinamu akakata simu kwa
hasira ya jibu la hausigeli wake huyo.
Hata hivyo, baada ya dakika moja
alimpigia simu tena akamwuliza kwa
nini alimjibu vile!
Kufuatia kuulizwa swali lile na bosi
wake, Jema aligundua alikuwa
amemkwaza akamuomba msamaha.
“Siku nyingine unapowajibu
wakubwa zako inatakiwa uwe
makini, bahati yako umegundua kosa
lako leo ningekurudisha kwenu,”
Mama Sabinamu alimwambia Jema.
“Mama nisamehe, sitarudia tena!”
Jema alimwambia bosi wake.
“Haya niambie mmefika wapi?”
Mama Sabinamu alimwuliza
msichana wake huyo wa kazi.
“Nimekaribia kufika mama!” Jema
alimjibu.
“Hivi wewe Jema leo una nini humo
kichwani mwako? Nakuuliza umefika
wapi unanijibu umekaribia, sema
ulipo?” Mama Sabinamu alimwuliza
kwa ukali ambapo msichana huyo
alimfahamisha kuwa alikuwa
Shekilango.
***
Msichana wa kazi alifika, mama
Sabinamu aliipokea kalenda, kisha
akaomba kuingia ndani ya
supermaket hiyo na kumtwangia
mumewe bila kumpa maelekezo
hausigeli wake huyo kwamba
aondoke au la!
“Haloo baba Sabinamu...”
“Unasemeje?”
“Nakutajia hizo namba kwenye
kalenda.”
“Umeshaifunua?”
“Ndiyo.”
Mwanamke huyo alizitaja namba
hizo, alipofika kwenye namba ya tatu
na kutaja jina lake, baba Sabinamu
akamwambia ndiyo aliyokuwa
akiiitaka.
“Oke, asante, uwe unapokea simu
bwana.”
“Sasa mume wangu, nilikuwa
chooni.”
“Sawa, halafuuu...huyo dada yupo?”
“Yupo.”
“Zile pesa alizoomba
mwambieeee...hebu nipe niongee
naye mwenyewe.”
Wateja kwenye supermaket hiyo
walishangaa sana, kwanza
walipomwona mwanamke huyo
mnene, aliyejichubua kupita kiasi,
miwanja kwenye nyusi kibao na uturi
wa kujaza kikombe, akisoma namba
kwenye kalenda kubwa ya ukutani
ndani ya supermaket.
Hata muuzaji kwenye supermaket
hiyo, ingawa alimruhusu kuingia
lakini hakujua alitaka kufanya nini.
Yeye alijua lengo lake aongee na
simu kisha atoke.
“Dada shika, ongea na baba,” alisema
mwanamke huyo akimpa simu.
“Haloo...sijambo...eee....haya...haya
asante baba.”
Mama Sabinamu alipokea simu yake,
alitoa shilingi elfu kumi na kumpa
msichana wake ili amlipe mtu wa
bodaboda...
“Chenji utachukua.”
“Sawa mama.”
Ndipo mama Sabinamu roho yake
ilipotulia na kuanza safari tena
kwenda alikokuwa anakwenda.
Bajaj iliegesha nje ya nyumba moja
yenye geti jeusi huku yeye akiwa na
simu sikioni...
“Ee, niko nje hapa Masoud...sawa.”
Baada ya dakika moja, geti dogo
kwenye geti kubwa lilifunguliwa,
akatokea kijana mmoja mdogo kwa
sura, mweusi, mwembamba na
mrefu...
“Karibu baby,” yule kijana
alimkaribisha mama Sabinamu kwa
salamu hiyo jambo lililomshangaza
sana dereva wa Bajaj.
“Huyu mwanamke ni kichaa au? Ina
maana ni kweli huyu mtoto ndiyo
bwana’ke?”
“Asante my dear, upo na nani ndani?”
mama Sabinamu alimuuliza kwa
sauti iliyojaa amri kwamba,
japokuwa Masoud ni mpenzi wake na
ndiye mwanaume lakini yeye ndiye
mwenye sauti ndani ya penzi lao,
pengine kutokana na kuwa na uwezo
mkubwa wa kifedha...
“Nipo peke yangu. Si nilikuwa
nakusubiri wewe mpenzi!”
“Oke, vipi ulikunywa ile kitu?”
“Na ndiyo nilikuwa namaliza kunywa
darling.”
Masoud na mama Sabinamu
walipishana miaka mingi sana.
Wakati Masoud alikuwa anacheza
kwenye miaka 22, mama Sabinamu
alikuwa na miaka 63. Ina maana
alimzidi miaka 41!!
Walizama ndani wote, mama
Sabinamu akiwa amemshika kijana
huyo kama vile ameshika mfuko wa
rambo wenye mabumunda ‘popcorn’
ndani, yaani alionekana ameshika
kitu chepesi.
Waliingia hadi kwenye chumba cha
Masoud, kitandani pwaa!
“Baby kama kweli umekunywa leo
usinicheleweshe. Nimekuwaza tangu
asubuhi mwenzio, nikasema leo
lazima nije unikate kiu ya kweli.
Haya sasa nioneshe kama
umekunywa,” alisema mama
Sabinamu huku akimwangalia
Masoud kwa macho yaliyomlegea
kama mla kungu.
“Nakuja sasa hivi,” alisema kijana
huyo huku akiondoka chumbani.
Alikwenda jikoni, akafunua mfuniko
wa sufuria, akachukua bakuli,
akachukua na kijiko kikubwa na
kuchota mchuzi uliokuwa kwenye
sufuria hiyo na kuunywa mfululizo...
“Leo akisema hajasikia kitu kama
siku ile itabidi nimkodishie
mwanaume mwingine,” alisema
Masoud akiwa anatoka jikoni...
“Yaani toka asubuhi mpaka muda
huu tayari nimekunywa supu vikombe
vitatu vya chai.”
Masoud aliingia chumbani na
kumkuta mama Sabinamu ambaye
mwenyewe alipenda kumwita
jimama kwa vijana wenzake, akiwa
kama alivyozaliwa tena amelala kwa
kujiachia. Tumbo kubwa, nido nido
kweli, kama kandambili namba kumi
ya Kimarekani. Sehemu ya mkono wa
mama Sabinamu, yaani kuanzia
kwenye kiganja hadi kwenye kiwiko
ndiyo paja la Masoud.
“Njoo baby njoo, natenda dhambi
kwa ajili yako,” alisema mama
Sabinamu mkono ukiwa hewani
kumwita kijana huyo.
 
JIMAMA LA SUPU YA PWEZA-
Mama Sabinamu hakuwa na jinsi,
aliingia bafuni kuoga ili aondoke
zake.
Akina Miriam siku hiyo
walimshangaa sana mdogo wao
Masoud. Alikuwa akihangaika sana,
mara chumbani, mara jikoni, mara
nje.
“We leo una nini kwani?”
RUKA NAYO...
“Niko sawa dada Miriam.”
“Mbona huku na kule, utadhani
hujatuona?”
“Hamna bwana dada,” alisema
Masoud lakini uso wake ulionesha
wasiwasi mkubwa.
Masoud alikaa kwenye kochi
sambamba na dada zake, lakini
kabla hawajasalimiana sana, simu
yake iliita, alikuwa mama Sabinamu.
“Sorry, nakuja.”
Alikwenda chumbani kukutana na
mwanamke huyo...
“Nikwambie kitu Masoud?”
“Niambie baby.”
“Siwezi kusubiri mpaka huo muda wa
kuondoka hao dada zako ndipo na
mimi niondoke, kama vipi
wasababishie waende kokote ili
nipite, kama haiatawezekana basi
nipite zangu mbele yao.”
Masoud alihema sana. Hakuna kitu
asichopenda dada yake Miriam kama
yeye kujihusisha na uhusiano wa
mapenzi mapema, alitaka asome
kwanza.
Nyumba anayoishi Masoud ni ya
familia, baada ya kifo cha baba yake
na mama yake, familia hiyo yenye
watoto watatu tu, Miriam, Sharifa na
yeye Masoud iliamua kijana huyo
aishi hapo kwa kuwa Miriam na
Sharifa walikuwa na uwezo
walipanga nyumba Mikocheni.
“Kwa kweli haitawezekana,” alisema
Masoud huku akitingisha kichwa
akimaanisha kwamba hakuna namna
zozote za kuwafanya dada zake
waende sehemu ili mwanamke huyo
apite sebuleni kutoka nje na
kuondoka zake...
“Basi nipite hapohapo sebuleni.”
“Mh! Baby, unajua dada zangu ni
wakali sana kwangu, sijui
itakuwaje?”
“Kwa hiyo sweet we uko tayari
niachike kwa mume wangu kwa
sababu ya ukali wa dada zako siyo?”
“Sina maana hiyo.”
“Basi nipite.”
Ilibidi Masoud akubali japo kwa
shingo upande, lakini akamwambia
watoke wote, wakifika sebuleni
atamtambulisha kuwa yeye ni nesi
alifika hapo kumchoma sindano ya
dozi ya mwisho.
“Poa, mimi ilimradi niondoke, sasa
ukisema ni nesi, ni mwalimu wa
tuisheni utajua mwenyewe.”
Masoud alitangulia mbele, mama
Sabinamu akawa nyuma, kufika
sebuleni, Miriam alishtuka kumwona
mwanamke huyo akitoka chumbani
na mdogo wake mdogo...
“Huyu nani Masoud?”
“Ni nesi dada Miriam.”
Wakati kijana huyo anasema ‘ni nesi
dada Miriam’, mwanamke huyo
mwenyewe alikuwa akitingisha
kichwa chini juu kuashiria kwamba
anachokisema Masoud ni kweli
kabisa...
“Hivi Masoud ni nani unaweza
kumdanganya wewe, nesi huyu?”
alihoji kwa ukali Sharifa huku
akimtaka mama Sabinamu
amwangalie yeye maana tangu
amefika hapo macho yake yalitua
kwa Miriam tu.
Mama Sabinamu alishtuka sana
kuonana na Sharifa, alimkumbuka...
“Dada Miriam, huyu mwanamke
ndiyo yule niliyekwambia
alifumaniwa kwenye nyumba ya
jirani yangu na wazazi wa mvulana,
alikuwa akimchukua na kwenda naye
kwa rafiki yake naye shangingi kama
yeye na kushinda naye humo badala
ya kwenda shuleni.”
“Ha! Kweli?”
“Muulize mwenyewe si huyu hapo!”
Mama Sabinamu uso ulimshuka
kwani ni kweli kabisa alikutwa na
mkasa huo wa aibu.
Ili kuficha aibu yake, alianza
kuondoka bila kuaga...
“Yaani jimama zima unamfuata
mtoto wako kulala naye kitandani,
loo! Aibu gani hii?” Miriam
alimsindikizia.
Nje ya nyumba hiyo, mama
Sabinamu aliona hata aibu
kusimama kusubiri Bajaj zinazopita,
alitembea haraka kuelekea
barabarani.
Bajaj zilichelewa kupita, akapanda
bodaboda ambapo njia nzima kila
walipopita gumzo alikuwa yeye kwa
jinsi alivyokaa kwenye bodaboda
hiyo.
“Wewee, mpeleke afike huyo,” vijana
wa kihuni walisema barabarani kwa
vile wowowo la mwanamke huyo
lilitokezea kwa nyuma na kumfanya
aonekane kituko flani.
Alipofika nyumbani alichukua namba
ya simu ya dereva huyo wa
bodaboda...
“Unajua kwa sisi tunaopenda kwenda
safarisafari za haraka muhimu kuwa
na simu za watu kama nyinyi,”
alisema mwanamke huyo huku
akijivuta kuingia ndani kwake.
Alibadili nguo haraka, akaingia
bafuni kuoga na kuendelea na
mambo mengine ya famillia.
Msichana wake wa kazi alishaanza
kuhisi jambo kwa bosi wake huyo,
hasa kwa kitendo chake cha
kumtuma kupeleka kalenda mbali
kiasi kile.
“Huyu mama kuna kitu anakifanya
lakini mume wake hakijui,” alisema
moyoni hausigeli huyo.
***
Dakika arobaini na tano baada ya
mama Sabinamu kurudi, mumewe
baba Sabinamu naye aliingia ndani
ya nyumba...
“Ooo mume wangu, pole na kazi
jamani!”
“Asanti mke wangu. Vipi za kushinda
hapa?”
“Nzuri tu, karibu sana.”
“Asante sana.”
Mama Sabinamu aliinama na
kumfungua kamba za viatu mumewe
huku akichekacheka...
“Asante sana,” baba Sabinamu
alisema. Moyoni aliamini ana mke
kumbe ana changudoa.
***
Usiku, mumewe akiwa amelala
fofofo, mwanamke huyo alikuwa
ameshika simu akichati...
“Kwani we suka unaishi wapi na
unaitwa nani vile?” mama Sabinamu
alianza kuchati na yule kijana dereva
wa bodaboda aliyempeleka
 
JIMAMA LA SUPU YA Pweza
ILIPOISHIA
“Kwani we suka unaishi wapi na
unaitwa nani vile?” mama Sabinamu
alianza kuchati na yule kijana dereva
wa bodaboda aliyempeleka
nyumbani akitoka kwa Masoud.
JIMWAGE NAYO...
Naitwa Sudi, naishi home.”
“Home ni wapi?”
“Mburahati.”
“Kwa wazazi wako?”
“Ndiyo.”
“Ukimaliza kazi huwa unapenda
kufanya nini?”
“Nakwenda baa.”
“Mh! Unakunywa pombe gani?”
“Viroba.”
Mama Sabinamu alicheka kwanza
mwenyewe huku mume wake
akiendelea kuuchapa usingizi.
“Kesho tunaweza kuonana?”
“Unataka nikupeleke mahali?”
“Mmh! Utajua hapohapo bwana,
wasiwasi wako ni nini wewe kijana?”
“Poa.”
Mama Sabinamu alilala lakini wakati
akiusaka usingizi alikuwa akijisemea
moyoni kwamba, akifanikiwa
kumpata kijana mwenye damu
inayochemka kama Sudi
atayafurahia maisha.
Wakati mama Sabinamu akiwaza
hivyo, Sudi alifurahi kumpata mteja
mpya.
“Ukiwa na wateja kumi wa uhakika
kama hawa mambo lazima
yakunyokee.
Baada ya kuwaza hivyo, alilala lakini
kwa mawenge kwa sababu tayari
kichwani alikuwa na viroba vitano.
***
Asubuhi, baada ya mumewe
kuondoka, mama Sabinamu alianza
kumchokoza kijana Sudi kwa
kumpigia simu...
“Halo, we nani?” Sudi aliuliza.
“Mmm! Jamani, ina maana namba
yangu hujaisevu tu?”
“Sijaisevu, we nani kwani?”
“Mimi ni yule mama wa jana
uliyempeleka nyumbani kwake.”
“Nilipeleka wengi, wewe ni yupi?”
“Mmm! Jamani, mimi ni yule mpaka
watu njiani wakawa wanapiga
kelele.”
“Oo, shikamoo.”
“Asante, mzima lakini?”
“Mimi mzima tu.”
“Sasa unaweza kuja kunichukua
kunipeleka mahali?”
“Si palepale uliposhukia jana?”
“Ndiyo.”
“Sawa nakuja.”
Mama Sabinamu aliamini
ameshamwingiza kijana huyo ndani
ya kumi na nane zake. Alianza kupiga
mahesabu ya namna atakavyomnasa
bila mwenyewe kujijua.
“Dawa yake ndogo, akifika nimtume
dada Soko la Kariakoo akanunue
nyanya na vitunguu kwa wingi,
mpaka akirudi tutakuwa tumefikia
mbali, tena si ajabu tutakuwa
tumemaliza kabisa,” alisema moyoni
mama Sabinamu.
“Dada.”
“Abee.”
“Hebu jiandae uende Kariakoo
kununua vitu.”
“Kama siku ile?”
“Ndiyo.”
***
Wakati msichana huyo akiondoka,
Sudi aliwasili na kupiga simu...
“Umefika kijana?”
“Nipo nje ndiyo.”
“Dada, hebu muingize ndani huyo
dereva wa bodaboda.”
Dereva aliingizwa ndani, akafikia
kwenye kochi na kukaa kiwogawoga
kama vile atachafua.
“Kaa tu usiogope,” mama Sabinamu
alimwambia Sudi kwa sauti tamu
huku akimwangalia kwa macho ya
mlegezo yaliyojaa mahaba ya kiutu
uzima.
“Dada we nenda, usichague nyanya
mbaya dada.”
“Sawa.”
Mama Sabinamu alisimama, akawa
anakwenda chumbani huku
akitembea kwa kujitingisha maana
alivaa khanga moja tu asubuhi ya
siku hiyo.
Mara akarudi lakini kabla hajafika
kwenye kochi, aliivua khanga kiaina
na kujifanya imemvuka kwa bahati
mbaya...
“Ha! Jamani hizi khanga nazo, hata
mbele ya wageni!”
Sudi alibahatika kuliona paja la
mwanamke huyo lilivyo jeupe,
akashindwa kukimbiza macho
pembeni na kumwangalia yeye.
“Pole,” alisema kwa sauti huku
moyoni akisema...
“Duuu! Bonge la paja, jimama
limeshiba hili.”
Mama Sabinamu alifikia kuufunga
mlango kwa kitasa huku akiimba
nyimbo za taarabu...
“Mume ataka matunzo siyo mambo
ya kihuni we mwenzangu... ooh
utalia... mwenzangu jiji utalijua...”
“Mh!” aliguna Sudi huku akiwa
ameinamisha kichwa.
Mawazo ya ubinadamu yalimjia,
aliwaza...
“Hivi jimama kama hili nikilipata
nitaliweza kweli?”
“Kwanza nitalipataje? Linaonekana
linapenda wakubwa wenzake, halafu
kulihonga hili hadi uwe tajiri.”
Mama Sabinamu alirudi kukaa...
“Kijana sasaaa....”
“Sasa si tunaondoka?”
“Tutaondoka, unakunywa nini
kwanza?”
“Nimeshiba.”
“Hata soda? Maana nataka nikiwa
najiandaa wewe uwe unapoteza
muda kwa kunywa hata juisi.”
“Basi nipe juisi.”
“Au viroba?”
Sudi aliposikia viroba mwili
ulimsisimka, akakubali.
Mama Sabinamu alikwenda dukani
nje kununua viroba vya konya vitatu
na kumletea, yeye akaenda chumbani
ambako alikaa kitandani na
kuwaza...
“Yule hakuna haja ya kumtongoza,
nifike na kumshika nimlaze kwenye
kochi mambo yaanze...
“Akikataa nitamwambia nitampa
hela, atakubali tu.”
 
JIMAMA LA SUPU YA PWEZA
Palepale alisimama na kumfuata
Sudi sebuleni huku mwili
ukimsisimka, alijiapiza kwamba
kijana huyo akikataa atambaka...
ENDELEA NAYO...
“ Kijana mzuri, unaonekana fundi
sana kitandani wewe, daa!
Nakutamani mwenzio,” alisema
mama Sabinamu huku tayari mikono
yake ikitua kwenye mwili wa Sudi
aliyekuwa akiendelea kukata viroba
vyake.
“Mimi huwa nafanya mazoezi ujue.”
“Kweli ee?” “Ee.” “Sasa hebu
nionesha hayo mazoezi yako jamani
Sudi.” “Aaa, kwako wewe siwezi.”
“Kwa nini huwezi?” “Nyie wa
wakubwa bwana, sisi tumezoea
uswahilini kwetu.
” “Hamna Sudi, kule na huku ni
kumoja tu, kweli wala usiogope
Sudi,” sasa mama Sabinamu alianza
kushika sehemu ya suruali pale
kwenye fraizi, Sudi akajua tayari hali
ya hatari imetangazwa, akajitutumua
kwa kuwa si kijana aliyelelewa kwa
maadili.
Angekuwa ametoka kwenye familia
yenye uadilifu kwanza angeshtuka
kumwona mwanamke sawa na
mama yake anamfanyia mambo yale
yeye akaona ndiyo sawasawa. “Basi
funga mlango kama unataka kweli au
unanitania? Ujue mi sitaniwi lakini?”
alisema Sudi kwa lugha ya kimtaani.
“Usijali Sudi jamani, mlango
nilishafunga mwenzio mapema.”
“Sasa, hapahapa au?” “We unataka
wapi Sudi?” “Popote pale.” “Hata
chumbani kwangu?” “Poa tu.” Mama
Sabinamu alimlaza Sudi kwenye
kochi kubwa na kumlaza ili aanze
kumfungua vifungo vya shati, kwenye
suruali na kumalizia kwingine lakini
Sudi hakutaka kusubiri, kazi hiyo
aliiwahi na kuifanya yeye.
Alipomaliza alimfungua kanga
mwanamke huyo ambapo hakupata
kazi sana kwani sehemu kubwa ya
kanga hiyo ilishafunguka yenyewe.
Sudi ndiye alimwendesha
mwanamke huyo tofauti kabisa na
yule kijana Masoud wa Kimara.
Sudi alimshikashika, akamchezea
kwa kufika sehemu ambazo ni za mtu
kujiheshimu na pia alikuwa
akimmwagia mabusu kila wakati
mwanamke huyo. Kuna zoezi moja
alilifanya ambalo mwenyewe alikuwa
analiita la kumcheki mafuta kama
yapo au hayapo, alipoona yapo Sudi
akaingia uwanjani kuanza mpira.
Ilikuwa siku ya pekee kwa mama
Sabinamu, hakuwahi kufikwa na hali
ile. Kila baada ya dakika tatu
alitangaza kuvunja dafu huku
akiweweseka na kelele za mbali
mpaka akawa hawezi kusema tena,
lakini Sudi wapi, yupo tu!
“Kijana ....kijana wewe,” mama
Sabinamu aliishia kuita hivyo bila
kuendelea na wala Sudi hakuwa
akimuuliza anachotaka kukisema.
Sudi alijua wamefikaje kwenye
mlango mkubwa wa kutokea nje,
lakini mama Sabinamu hakujua.
Hapo ni baada ya Sudi kuvunja dafu
lake la kwanza ambalo mwanamke
huyo hakutaka kusikia dafu la pili
likivunjwa. Alichokuwa akikifanya
Sudi wakati mwingine aliishika
miguu ya mwanamke huyo na
kuipeleka pande mbili za dunia huku
akimhemea masikioni utaalam
ambao ni wa hali ya juu sana...
“Baby...tumefikaje hapa mlangoni, si
tulikuwa kwenye kochi?” “Kazi
ilikuwa nzito.” Mama Sabinamu
alikuwa akihema kwa kasi sana,
moyo ulimwenda mbio mpaka
akajua anakufa sasa, mwili ulichoka.
Aliamka akashika simu na kumpigia
msichana wake wa kazi... “Uko
wapi?” “Mama nimeshuka hapa
kituoni nakuja.”
“He! Ina maana umefika Kariakoo na
kurudi?” “Ndiyo mama.,” “Sudi
anakuja msichana, vaa uende.” Sudi
alivaa haraka sana, kabla ya kutoka
mama Sabinamu akamwambia
asubiri getini. Aliingia chumbani,
akatoka ameshika shilingi laki mbili.
“Hizi nakupa zaidi ya kazi nzuri
uliyoifanya, nitakupigia.” Sudi alitoka
mbio akadandia pikipiki na kurudi
kijiweni kwake. “Washkaji leo
nilipata zali,” aliwaambia wenzake.
“Zali gani tena mwana?” Sudi
alisimulia kila kitu kuhusu mama
Sabinamu, wakashangaa sana hasa
alipowaonesha kitita cha pesa. “Sasa
mwana huyo mwanamke ukitaka
akujengee nyumba mnywee supu ya
pweza.
” “Supu ya pweza itafanya nini?”
“Ohoo, hujui?” “Sijui.” “Ile itakupa
nguvu zaidi.” “Lini?” “Ukijua leo
anakutaka we kunywa.” “Supu tu au
hata pweza wenyewe?” “Supu tu,
hata bodaboda atakununua yako.”
Sudi alichukua ushauri huo na
kuufanyia kazi.
*** Zilipita siku tatu, siku hiyo mama
Sabinamu akaenda kwenye maskani
ya Sudi... “Kijana hujambo?”
“Sijambo, karibu mama.” “Eti Sudi
nimemkuta? Maana simpati kwenye
simu.” “Sudi leo hajaja anaumwa.”
“Anaumwa nini?” “Homa tu.”
“Naweza kwenda kumwona?”
Aliposema anaweza kwenda
kumwona, kijana aliyeulizwa akajua
yule ndiyo yule mwanamke wa Sudi,
jimama alilolisema.
“Kwake hakuna anayepajua.” “Loo!
Jamani Sudi wangu.” “Kwani wewe
ni nani wako?” “Mtu wangu.”
“Kivipi?” “Elewe hivyo, mimi bila Sudi
siwezi kuishi.” “Sema vizuri mama,
vijana wako wengi hapa wanajua
kazi kuliko Sudi.” “Kazi gani?”
“Yoyote ile.
 
JIMAMA LA ya pweza
“Unaogopa ee? Mbona huji sasa?”
“Nakuja.”
Mlio wa simu ulimshtua mwanamke
huyo, akapeleka mkono kuichukua
huku moyo ukimwenda mbio...
JIACHIE KIVYAKO...“
Mh!” aliguna baada ya kujua ni
mumewe. Akaamua asipokee kwanza
mpaka moyo utakapokuwa tayari
kufanya hivyo akizingatia kuwa, swali
lake la kwanza linaweza kuwa...
“Upo wapi?” atashindwa cha kujibu.
Pia aliamua kwamba ampigie
kwanza msichana wake wa kazi,
Jema na kumuuliza kama baba
alishafika nyumbani ndipo ajue nini
kifuate.
Baba Sabinamu alipoona mkewe
hapokei simu yake alimtwangia
msichana wa kazi...
“Mamaaa...baba anapiga, si ajabu
anataka kujua mama yuko wapi?
Nitamwambia nini mimi?
Mamaaaa...”
Baba Sabinamu alikata simu,
akatulia lakini huku akiwa na
maswali kibao, nini kimewafanya
wote wawili wasipokee simu.
***
Akili za mama Sabinamu zilipokaa
sawa alitoka kitandani, akachukua
simu na kumpigia Jema...
“Mama baba alipiga simu sasa hivi,
sijapokea.”
“Hajafika nyumbani?”
“Bado mama.”
“Basi sawa, nitakupigia baadaye.”
Mwanamke huyo alijivuta na mwili
wake mkubwa akafungua dirisha na
kusimama hapo ili kelele za nje watu
wakipita na watoto wakicheza ziingie
ndani ya chumba hicho alichokuwa
na kijana wa bodaboda. Lengo lake
akimpigia simu mumewe ajue yuko
mtaani...
“Haloo mume wangu.”
“Upo wapi wewe?”
“Nipo mtaa wa pili kwenye duka la
mama Tatu.”
“Kweli?”
“Kabisa mume wangu. Kwa nini siku
hizi huniamini lakini?”
“Hebu nenda nyumbani bila kukata
simu nataka kuongea na Jema.
Usikate simu tafadhali.”
“Sawa mume wangu.”
Kutoka kwenye duka hilo hadi
nyumbanai ni kama dakika tatu tu.
Mama Sabinamu aliona kimemnukia,
hakujua kama mume wake aliingiwa
na wasiwasi baada ya mtu wa
kibanda cha J-Pesa kusema pale ni
Mwananyamala. Mumewe naye
aliposikia hivyo akaona atumie
mbinu hiyo kujua ukweli na uongo.
“Umekaribia?”
“Ndiyo nakaribia, ungekata simu
niingie ndani basi nikifika.”
“Nimesema usikate simu, ukifika
gonga geti dada atasikia atatoka
kukufungulia.”
“Lakini baba Sabinamu huoni kama
hela kwenye simu itai...”
“Mimi ndiyo nimepiga.”
“Sawa lakini uangalie na bajeti,”
hapo mama Sabinamu alishavaa,
sasa alikuwa amefungua pochi huku
simu ameiminya na bega kwenye
sikio akatoa shilingi elfu hamsini,
alimpatia yule kijana na kumwambia
kwa ishara watoke nje waondoke.
Alitangulia kutembea kutoka huku
akihakikisha milango ya gesti hiyo
haitoi milio. Alipofika mapokezi, huku
simu bado ikiwa sikioni na
akizungumza na mumewe, mhudumu
alitaka kumwambia ‘karibu tena
anti,’ lakini ile anataka kunyanyua
midomo tu, mama Sabinamu
akamuwahi kwa ishara kwamba
asiongee, mhudumu akafunga
mdomo.
Walipofika nje, kijana aliwasha
bodaboda...
“Hiyo bodaboda ipo wapi mama
Sabinamu?” aliuliza mumewe.
“Nje kwa mzee Mkalikuyu hapa.”
“Imemleta mtu au imekuja
kumchukua?”
“Nadhani ilikuja kumchukua.”
“Sawa, si umekaribia kufika
nyumbani?”
“Ndiyo mume wangu.”
Mwanamke huyo alijua kimemnukia
kwani akisema apande ile bodaboda,
mumewe atajua kwa kelele na hali ya
upepo kuvuma, bahati nzuri lilitokea
teksi ambapo aliisimamisha na
mkono huku akimwambia yule kijana
wa bodaboda kwa ishara kwamba
aende atampigia naye akakubali kwa
ishara.
Mlango wa teksi ulipokuwa wazi,
mama Sabinamu akazama ndani bila
kusema na kumwamuru dereva kwa
mkono uelekeo anaotaka waende.
Dereva akachoma mafuta huku kila
wakati akimtupia macho mwanamke
huyo ili aone ishara yake...
“Nakaribia mume wangu, usiwe na
wasiwasi.”
“Unajua sasa ni dakika kama nne?”
“Ni kweli na ndiyo nimefika sasa.”
“Haya gonga geti.”
Ilibidi mama Sabinamu agonge paa
la juu la gari hilo ili ionekane amefika
kweli...
“Pupupupuuuu...dada...we dada
wewe.”
Kwa dereva wa teksi kwake lilikuwa
jambo jipya sana, hakujua nini
kilitokea ikabidi achezeshe akili na
ndipo alipogundua kuwa, mwanamke
huyo amemdanganya mume wake
yuko nyumbani kumbe sivyo...
“Hafungui?”
“Nashangaa mume wangu, dada siku
hizi amekuwaje sijui.”
“Gonga tena.”
“Pupupupupuuu...dada!”
Kama si kufunga vioo vya gari hilo,
watu mitaani wangeshangaa sana
kusikia mtu yumo ndani ya gari
halafu anaita dada kwa sauti ya juu.
Dereva alijikuta amesimamisha gari
nje ya nyumba ya mwanamke huyu,
akashuka huku akimwambia dereva
kwa ishara kwamba amsubiri.
“We dada,” aligonga sasa
kiukweliukweli.
“Abee.”
“Abee nini njoo ufungue geti.”
Jema alifika getini, akafungua...
“Ongea na baba,” baba Sabinamu
alimpa simu.
“Haloo baba, shikamoo.”
“Marahaba, za kazi?”
“Nzuri.”
“Nataka jioni unitengenezee juisi
nzuri ya machungwa, sawa?”
“Sawa baba.”
 
JIMAMA LA SUPU YA PWEZA-9
SAWA baba.”
“Haya mpe simu huyo mama yako.”
“Mama simu hii.”
“Haloo mume wangu...”
“Nimeshaongea naye, tutaonana
baadaye,” baba Sabinamu akakata
simu.
Mama Sabinamu wala hakuwa na
haja ya kumuuliza msichana wake
wa kazi mumewe alikuwa anataka
nini kwani alishajua alitaka
kuhakikisha yupo nyumbani au la!
Alikaa kwenye kochi na kuwaza.
Alianza kuona hali ngumu, mumewe
ameanza kuwa mfuatiliaji wa nyendo
zake za kila siku kuliko zamani...
“Lakini mi mjanja bwana, haniwezi,
akiijua kushoto mimi nitapita kulia.
Najijua kinachonifanya nahangaika
hivi ni tabia yangu ya ukware, mimi
kutulia na mwanaume mmoja naona
kama najipunja maisha,” alijisemea
moyoni mwanamke huyo.
***
Wiki moja ilikatika lakini kila siku
mumewe baba Sabinamu akiwa
kazini alikuwa akimpigia simu na
kutaka kujua alipo, kama ni
nyumbani alimtuma kitu ambacho
hakihamishiki kirahisi ili ahakikishe.
Siku hiyo mama Sabinamu alikuwa
na mchecheto wa kutoka kwenda
kukutana na kijana mmojawapo kati
ya wale wawili wa bodaboda ili
akarushe roho mahali, aliamini
mumewe atampigia simu kama
alivyokuwa akifanya kwa wiki nzima,
hivyo aliamua kukodi Bajaj na
kupakiza baadhi ya vitu ambavyo
mara kadhaa mumewe alikuwa
akimuuliza avifanyie kazi ili ajue
kama yupo nyumbani.
Alibeba tivii, brenda, deki,
king’amuzi, redio na kalenda ya
ukutani...
“Dada kwani unahama?” Jema
alimuuliza bosi wake.
“Hayakuhusu.”
“Siyo hivyo dada, naona unabeba
vitu.”
“Nimekwambia hayakuhusu kabisa
Jema. Hebu nisaidie kuvibeba hadi
nje.”
Jema alibeba vitu hadi nje ambapo
mwanamke huyo alisimamisha
Bajaj...
“Nakwenda Mwananyamala, shilingi
ngapi suka?”
“Na hivyo vitu?”
“Ndiyo.”
“Nipe elfu kumi maana vitu ni vizito.”
Ili kuokoa muda, mama Sabinamu
alikubali ambapo suka huyo alishuka
na kuvipakiza vitu hivyo kwenye
Bajaj.
“Kata kulia... hapo mbele ingia
kushoto... punguza mwendo... hapo
kuna njia inaingia kushoto, simama
hapo nje ya hiyo gesti.”
Bajaj ilisimama, mama Sabinamu
akashusha vitu vyake na kuomba
msaada kwa dereva hadi mapokezi...
“Karibu anti.”
“Asante, nataka chumba.”
Alipewa chumba cha kwanza kabisa
ukiingia ili iwe rahisi kuingiza vitu
vyake ndani.
Baada ya kumaliza zoezi hilo alikaa
kitandani sasa, akampigia simu Sudi
kwanza...
“Haloo.”
“Upo wapi baby?”
“Du! Nipo mbali sana, Kibamba
huku.”
“Basi,” alikata simu mwanamke
huyo, akampigia mwenzake na
Sudi...
“Haloo.”
“Hujambo my dear?”
“Sijambo, shikamoo.”
“Asante, uko wapi?”
“Nipo kijiweni hapa, we upo wapi?”
“Nipo kwenye ile gesti ya siku ile,
unaweza kuja?”
“Poapoa, nakuja sasa hivi, dakika
sifuri tu.”
Kijana huyo alikwea bodaboda kwa
fujo na kuondoka. Alijua anakwenda
kupata mambo mawili, penzi halafu
pesa...
“Sisi ndiyo wenye bahati zetu bwana!
Tena ndiyo wakali wa hizi kazi.”
Mama Sabinamu ile anakata simu ya
kijana huyo tu, ya mume wake
inaingia...
“Mh!” aliguna kwanza, akataka
asiipokee lakini akabaini kwamba
asipopokea, anaweza kumpigia
msichana wake wa kazi na kwa
sababu aliondoka na vitu akajua
anahama, anaweza kumwambia
jambo ambalo mume huyo atarudi
nyumbani haraka...
“Halo mume wangu.”
“Upo wapi?”
“Nyumbani.”
“Una uhakika?”
“Ndiyo mume wangu, sasa niende
wapi miye?”
“Haya, hebu niambie kwenye tivii
kuna kipindi gani muda huu?”
“Muda huu kuna...” alisema mama
huyo huku akichomeka waya wa tivii
kwenye umeme ukutani, akachomeka
na king’amuzi na kuweka sawa
antena, akakumbuka alisahau
kubeba rimoti, ikabidi atumie njia ya
mkono kuminyaminya.
“Sasa hivi ni kipindi cha mapishi.”
“Sawa... sasa hebu weka tibisii
wani.”
“Nimeweka mume wangu.”
“Kipindi gani?”
“Marudio ya kipindi cha...”
“Okeoke, hebu washa brenda.”
Mama Sabinamu alichomeka waya
wa umeme na kuwasha brenda,
ikalia kwa fujo hadi mhudumu
akakimbia kwenda kugonga
mlango...
“Sawa, baadaye kidogo basi.”
“Sawa mume wangu, mi siku hizi
sitoki nyumbani.”
“Ngo ngo ngo...” mlango uligongwa
kwa fujo.
“Ingia,” jimama hilo lilijua kijana wa
bodaboda amefika na kuelekezwa na
mhudumu, kumbe sivyo...
“Anti vipi kwani?” mhudumu
alimuuliza mwanamke huyo baada
ya kusikia mlio wa brenda...
“Nilikuwa naijaribu hii mashine
yangu.”
“Ooo...sawa... nilidhani nini sijui, da!
Nimeogopa sana.”
“Hamna kitu. We nenda tu.”
Mhudumu aliondoka, lakini simu ya
mumewe ikaingia tena...”
“Nitumie elfu hamsini zipo ndani ya
mfuko wa koti jeusi nyuma ya
mlango.”
“Sawa mume wangu.”
Mama Sabinamu akaondoka mpaka
kwenye kile kibanda alichotuma
fedha siku saba nyuma kwenda kwa
mumewe huyohuyo...
“Hebu nitumie elfu hamsini hizi
kwenda namba hizi,” alimwambia
mwenye kibanda.
Kabla ya kutuma fedha hizo, mwenye
kibanda alimwangalia mama
Sabinamu kwa macho ya
kumsisitizia, akamkumbuka kwamba
ndiye aliyempa fedha za kutuma
halafu akapigiwa simu kuulizwa na
mtu akidhani ni Mikocheni...
“Tayari zimefika kwa Johanes
Yohana Mfukowake...”
“Sawa, ni huyohuyo,” alisema mama
Sabinamu akiondoka kurudi gesti.
Baba Sabinamu alishtuka kuona
namba iliyomtumia fedha ni ileile ya
siku saba nyuma, ikitokea
Mwananyamala, akashtuka...
"Khaa! Ina maana yupo
Mwananyamala na si Mikocheni
nyumbani?"
 
JIMAMA LA SUPU ya Pweza 10
ILIPOISHIA IJUMAA WIKIENDA:
Baba Sabinamu alishtuka kuona
namba iliyomtumia fedha ni ileile ya
siku saba nyuma, ikitokea
Mwananyamala, akashtuka...
“Khaa! Ina maana yupo
Mwananyamala na si Mikocheni
nyumbani?”
RUKARUKA NAYO…
Baba Sabinamu papo hapo alishika
tena simu yake na kumpigia mwenye
kibanda kwa namba ile
aliyomfahamishia…
“Eti ni kibanda cha wapi hapo?”
“Mwananyamala.”
“Oke, asante. Lakini eti, ni
Mwananyamala gani?”
“Jirani na ilipokuwa pub ya Aunt
Ezekiel.”
“Oke, nikija naweza kukuona?”
“Kwani kuna tatizo?”
tuma pesa hapo yupo?”
“Kaondoka.”
“Yukoje?”
“Mwanaume fulani hivi, mnene,
mrefu, ana wowowo.”
“Kaelekea wapi?”
“Sijui, unajua mimi nina wateja
wengi, si rahisi kujua ameelekea
wapi mteja anapotoka hapa.”
“Asante sana.”
“Poa.”
Baba Sabinamu akapiga simu kwa
msichana wa kazi, lakini
hakupokea…
“Hapana nachezewa mchezo kabisa,
wala si la kuuliza hili. Ni kwa nini
msichana wa kazi hapokei simu?
Halafu mke wangu si alisema yupo
nyumbani na nimempigia
nikamwambie awashe tivii,
akawasha, awashe brenda
akawasha, Mwananyamala kafika
saa ngapi?
“Dawa ya huyu moja tu, nimwambie
anisomee namba za kwenye kalenda.
Maana kama ni tivii hata gesti zipo,
Brenda si ajabu aliwasha kitu kingine
kikaunguruma kama brenda, ila
kalenda si rahisi namba zake
kuzipata kwingine.”
Alimpigia mkewe mama Sabinamu…
“Ulisema uko nyumbani?”
“Ndiyo mume wangu.”
“Hapo ulipo ni sebuleni chumbani?”
“Sebuleni.”
“Oke, hebu sogelea kalenda ukutani.”
“Oke, nimeshaifikia.”
“Funua nyuma kabisa.”
“Nimefunua tayari.”
“Soma namba ya mwisho kulia,
naamini niliiandika kwa wino
mwekundu.”
“Nimeiona ni ya mtu anaitwa Samuel
Tupatupa.”
“Sawasawa, nitajie namba zake.”
Mama Sabinamu alizitaja namba
hizo, kisha mumewe akamshukuru na
kumwambia baadaye…
“Sasa, kama yupo Mwananyamala
kalenda nayo? Ina maana ameibeba
kwenda nayo Mwananyamala?
Haiwezekani.”
Mama Sabinamu alijirusha na kijana
wake mpaka hamu ikamwishia,
walipumzika, wakalala, walipoamka
muda ulikuwa umekwenda, mama
Sabinamu akaondoka akimwachia
kijana huyo shilingi elfu hamsini.
“Mimi natangulia zangu,” aliaga.
“Sawa, siku nyingine basi.”
“Sawa mpenzi wangu lakini usiwe na
mwanamke mwingine, vibinti
vidogodogo achana navyo haviwezi
kukusaidia kitu kama mimi, sawa
mpenzi wangu?”
“Nimekusikia mpenzi.”
“Nafurahi kusikia hivyo,” alisema
mama Sabinamu huku akimwangalia
kijana huyo kwa macho ya mlegezo.
Lakini yule kijana alimsaidia
mwanamke huyo kutoa vitu vyake
ambapo alishangaa sana. Hakuwahi
kumwona mwanamke anaingia gesti
na vitu kibao kwa lengo la kupoteza
maboya kwa mumewe punde akitaka
kujua alipo.
***
Bajaj ilipaki nje ya nyumba,
mwanamke huyo akashuka na
kumwita msichana wake wa kazi…
“Hebu saidia kuingiza vitu ndani.”
***
Saa kumi na moja jioni, baba
Sabinamu alitua Mwananyamala
eneo ambalo aliambiwa ndipo kilipo
kibanda cha kurushia pesa, akapiga
simu…
“Nimefika maeneo ilipokuwepo pub
ya Aunt Ezekiel, kibanda chako kipo
kwa wapi?”
“Kipo hapaaa…kwani wewe upo
kwenye gari au?”
“Kwenye gari ndiyo.”
“Ni hiyo VX nyeusi?”
“Ndiyo.”
“Mimi nakuona kwa ng’ambo mbele
kidogo, kwa hiyo rudi nyuma.”
Baba Sabinamu alirudisha gari
nyuma hadi jirani na kibanda hicho,
akashuka.
Alivuka barabara hadi kibandani…
“Hujambo?”
“Sijambo, shikamoo tena.”
“Marhaba tena. Nataka kujua huyo
mwanamke anayekupa pesa
kunitumia hapa tulipo akitoka
anaelekea upande gani?”
“Huwa anakata kona hiyo hapo
mbele.”
“Kwa hiyo anaingia huko
ndanindani?”
“Ndiyo. Kwani vipi?”
“Nimeuliza tu.”
Baba Sabinamu aliaga kwa
kushukuru, akaondoka kuelekea
uelekeo alioambiwa ambako
alipofika alianza kwa kuulizia gesti…
“Samahani ndugu, eti wapi kuna gesti
hapa?” alimuuliza muuza chipsi
mmoja.
“Pale mbele,” muuza chipsi
alielekeza kwa mkono.
“Asante.”
Baba Sabinamu alifika kwenye gesti
hiyo na kupiga hodi licha ya mlango
kuwa wazi…
“Karibu, ingia.”
Alizama ndani…
“Eti, kuna mgeni wangu kaniambia
yuko hapa, ni kweli sijui?”
“Nani?”
“Anaitwa Theresia.”
“Mh! sijapata mgeni wa jina hilo
leo.”
“Jana je?”
“Hata jana, hata juzi! Hata juzi ile.”
“Leo hajaja mwanamke mmoja
mnene sana, mrefu, ana wowowo hivi
“Kunaaaa…kuna Mwanaidi, Safia,
Zuuuwena na Mary, wako ni yupi?”
“Nadhani hakutumia jina lake.”
Hapo mhudumu akashtuka, kama
hakutumia jina lake kwa nini aulize
ana mgeni wake?
Baba Sabinamu alitoka akipiga simu
kwa mkewe… “Uko wapi?
 
JIMAMA LA SUPU YA PWEZA-11
ILIPOISHIA
Alizama ndani…
“Eti, kuna mgeni wangu kaniambia
yuko hapa, ni kweli sijui?”
“Nani?”
“Anaitwa Theresia.”
“Mh! Sijapata mgeni wa jina hilo
leo.”
“Jana je?”
“Hata jana, hata juzi! Hata juzi ile.”
“Leo hajaja mwanamke mmoja
mnene sana, mrefu, ana wowowo
hivi?”
TEMBEA NAYO…
Walikuja wengi, yupi sasa?”
“Hebu nisomee majina yao kwenye
kitabu chako.”
“Kunaaaa…kuna Mwanaidi, Safia,
Zu…uu…wena na Mary, wako ni
yupi?”
“Nadhani hakutumia jina lake.”
Hapo mhudumu akashtuka…
“Kama hakutumia jina lake kwa nini
uulize una mgeni wako hapa? Kwa
nini asitumie jina lake wakati anajua
wewe utamfuata? Au ni mkeo
umekuja kumfumania? Sema mzee
usaidiwe.”
“Ni kweli, kuna mke wangu nasikia
anafika sana maeneo haya, sasa
nilitaka kujua kama leo kafika au la!”
“Anaitwa nani?”
“Theresia kama nilivyosema awali.”
“Hapana, mwanamke wa hivyo
aliyekuja hapa ndiye Safia.”
“Atakuwa huyohuyo, alikuja na nani?”
“Alikuja na kijana mmoja, mdogo.
Kwanza mi nilidhani mwanaye.”
“Huyo mwanamke yukoje?”
“Mnene, mrefu, ana wowowo la
nguvu.”
“Alivaaje?”
“Gauni la kitenge, lina maua ya kijani,
bluu na nyeusi.”
“Mh! Hata yeye anavaaga hivyo ila
sijui kama leo alivaa hivyo, lakini
nashukuru sana, nitajua cha kufanya
nikifika nyumbani,” alisema baba
Sabinamu akitoka.
Akili yake ilimwambia kwamba
akifika nyumbani kwake akatupie
macho kwenye kapu la nguo chafu,
kama mkewe alivaa gauni hilo siku
hiyo angepata jibu.
***
“Mama leo hujanipa nguo chafu,”
msichana wa kazi alimuuliza mama
Sabinamu.
“Tena kweli, hebu ngoja nikutolee.”
Mama Sabinamu aliingia chumbani
kwake akiwa ndani ya kitenge tu na
kulifanya wowowo lizidi kucheza
mpaka basi. Msichana wa kazi
mwenyewe alikuwa akimwangalia
huku anacheka na moyoni akisema…
“Ama kweli kuna watu wameumbwa!
Mtu unakuwa na wowowo kubwa
kama umebebeshwa kifurushi cha
nguo!”
Mara, mama Sabinamu alitoka akiwa
amebeba nguo, akambwagia
msichana wake wa kazi…
“Lakini hilo gauni langu la kitenge
nililolivaa leo nipe, halijachafuka,
nitalirudisha kwenye kabati,” alisema
mwanamke huyo.
Mama Sabinamu alirudi chumbani,
akalitupia gauni hilo ndani ya kabati.
Ile anatoka sebuleni tu, mumewe
akawa anaingia…
“Karibu mume wangu, pole na kazi.”
“Asante,” baba Sabinamu alijibu kwa
mkato.
“Naona leo kama umechoka sana?”
“Kawaida tu.”
Alipitiliza hadi chumbani lakini tayari
mke wake alishahisi kuna taa
nyekundu inawaka siku hiyo.
Kule chumbani, baba Sabinamu
alitupia macho kwenye sehemu ya
nguo chafu, hakuona hata moja zaidi
ya ‘makufuli’ yao ambayo huwa
mama Sabinamu hatoagi yafuliwe na
msichana wa kazi zaidi yake
mwenyewe.
Baba Sabinamu alitoka hadi chumba
kingine ambako kuna tenga la nguo
chafu, akazifumua zote, moja baada
ya nyingine lakini hakuona gauni hilo
la kitenge aliloambiwa na yule
mhudumu wa gesti.
Alirudi kukaa sebuleni na kushika
rimoti akibadili stesheni mbalimbali
huku akijikausha kwa yote aliyonayo
moyoni. Yeye aliamua kufuatilia kwa
siri mambo yote ili ukweli ukae
mkononi siku moja.
“Leo umechoka sana na kazi mume
wangu?”
“Kawaida tu, kama siku zote.”
“Mbona haupo sawa?”
“Nipo sawa.”
Mara baba Sabinamu alisimama,
akaenda jikoni kwa msichana wa
kazi…
“Ni kwa nini huwa hupokei simu
yangu?”
“Nakuwa sijaiona, nikiiona simu
yangu inakuwa haina fedha.”
“Leo mama alitoka?”
“Mh! Sikumbuki baba!”
“Hukumbuki wakati umeshinda
hapa?”
“Ni kweli lakini huwa anatoka
anarudi.”
“Anarudi baada ya muda gani?”
“Muda huohuo, mara nyingine
anakaa muda kidogo.”
“Oke.”
***
Mama Sabinamu alikaa wiki mbili
bila kutoka ndani huku mume wake
akirudi nyumbani wakati wowote ili
kujiridhisha kwa macho, lakini siku
hiyo aliamua kutoka baada ya
mumewe kwenda safari ya kikazi,
Mwanza.
Alimpigia simu Sudi, akamtaka
amkute kituoni ili waende kunanilii…
“Usitoke hapo, mimi nakuja sasa
hivi.”
Baada ya kujiandaa, mama
Sabinamu alitoka, lakini kufika getini
tu mumewe akapiga…
“Haloo.”
“Uko nyumbani?”
“Ndiyo.”
“Nataka kuongea na Jema.”
“Haya…we Jema simu yako hii.”
Jema ambaye alikuwa nyuma ya
mwanamke huyo ili afunge geti,
aliongea na baba Sabinamu lakini
palepale mama Sabinamu akajua
kimenuka, lazima mume wake
ataanza tabia zake za kumwambia
funua kalenda, washa tivii, sukuma
kabati. Alichoamua alirudi ndani na
kumwomba msichana wake wa kazi
amsaidie kutoa vitu
atakavyomwambia…
“Dada, hebu toa tivii, deki yake,
rimoti, cd mbili za dini, blenda,
kalenda. Na aaaaa….” kabla
hajamalizia, mumewe alimpigia tena
simu…
“Haloo…”
“Hebu fungua friji, angalia kuna bia
niliziacha jana, ziko ngapi?”
“Zipo…ooooo nne.”
“Na ile wine ipo?”
“Ipo.”
“Oke.” Akakata simu.
Mama Sabinamu akachoka kabisa
kwani ndani ya friji pia mlikuwa na
pombe kali ambazo mumewe
hakuziulizia, ikabidi azishike idadi ili
akiulizwa ajue cha kujibu.
“Dada niwekee naaa…naaa ngoja
nikachukue brifkesi ndani, halafu
nitolee na viatu vyake pea mbili,
kama kuna soksi ulifua weka pea
mbili pia.”
“Mh! huyu mama mi simuelewi, hivi
vitu anakwendaga navyo wapi?”
“Toa na vile vitabu pale.
 
JIMAMA LA SUPU YA PWEZA-12
ILIPOISHIA
“Mh! huyu mama mi simuelewi, hivi
vitu anakwendaga navyo wapi?”
SASA ENDELEA…
“TOA na vile vitabu pale
anavyosomaga baba, vitoe kumi na
tano.”
Jema alitii lakini alikuwa hajijui
kiakili, aliamini kwamba kuna
biashara anayofanya huyo
mwanamke lakini anashindwa
kusema kwa uwazi.
“Mama kwani unakwenda wapi?”
“Wewe maswali ya nini sasa?”
“Basi mama, nisamehe.”
“Weka na…aaa…naaa…weka na ngoja
nikachukue mwenyewe kibegi chake
anapendaga kubebea vikaratasi
vidogo vidogo.”
Mama Sabinamu mwenyewe
alizama ndani, alipotoka alibeba
kibegi hadi nje, wakaweka vitu vyote
hapo…
“Unachukua Bajaj?” aliuliza Jema…
“Ndiyo! He! Nimesahau, nenda
chumbani ukaniletee kadi ya
kununulia luku na ile
tunayonunuliaga muda wa
king’amuzi.”
“Ile yenye rangi rangi?”
“Ndiyo.”
Jema aliingia ndani, aliporudi na vitu
hivyo alikuta dereva Bajaj
ameshapakia mizigo yote alikuwa
anasubiriwa yeye tu.
“Haya, hakikisha geti halikai wazi,
sawa?”
“Sawa mama.”
“Wapi mama?” suka alimuuliza
mwanamke huyo.
“Mwananyamala.”
Bajaj ilitoka kasi, ikakata kona na
kutokea barabarani, ikaingia
kwingine mwishowe ikafika
Mwananyamala, tena nje ya gesti
hiyo.
Alisaidiwa na dereva kuvipakua vitu
vyote…
“Mama unahamia hapa gesti au kwa
muda tu?” suka alimuuliza.
“Hayakuhusu, tena hayakuhusu
kabisa.”
“Nisamehe sana anti.”
“Tena ukome.”
Ukimya ulitawala, baada ya mizigo
yote kushushwa na kuingizwa ndani,
mama Sabinamu alimpigia simu
Sudi.
“Uje hapa jirani na kituo cha daladala
cha Komakoma, nitakuelekeza
nilipo.”
“Sawa, sasa hivi?”
“Ndiyo, unataka uue usiku?”
“Nakuja mama nakuja.”
“Umekunywa supu ya pweza lakini?”
mama Sabinamu aliuliza kama kwa
utani huku akiachia kicheko cha
nguvu. Ikabidi na Sudi naye kucheka
sana…
“Nimekunywa,” alisema Sudi huku
kicheko kikiendelea.
Palepale aliwasha pikipiki yake,
lakini kabla hajaondoka, wenzake
walimuuliza anakokwenda…
“Nakwenda kwa jimama.”
“Lipi?” aliuliza yule kijana aliyelala
na mwanamke huyo mara mbili
kwenye gesti hiyo…
“La supu ya pweza.”
“La supu ya pweza? Ndiyo lipi hilo?”
“Iko siku utalijua.”
Baada ya Sudi kuondoka, yule kijana
alihisi jimama la supu ya pweza
linaweza kuwa jimama lake pia.
Akampigia simu…
“Mama vipi?”
“Salama, hujambo kijana wangu?”
“Sijambo mama, uko wapi?”
“Leo siyo zamu yako, nitakutafuta
kesho.”
“Si nimekuuliza ulipo lakini mama!”
“Nimesema leo siyo zamu yako
kijana wangu, nitakutafuta.”
“Sawa, maana leo nilikunywa mchuzi
mmoja hivi, haufai mama.”
“Mchuzi wa samaki? Maana ndiyo
una shombo sana.”
“Hapana, wa pweza.”
“Wa pweza?”
“Ndiyo, wa pweza. Basi daaa! Mwili
wote unasisimka, natamani kama
tungekuwa kitandani. Na kama
ingekuwa hivyo leo ingekuwa asubuhi
mpaka jioni, acha kabisa…maana
ningekubinua, ningekupindua,
ningekubeba mpaka ungesema basi.”
“Mh! We kijana, kweli?”
“Khaa! Unajua nilipeleka wateja pale
Shekilango, kwa pembeni karibu na
kituo ndiyo nikaona supu ya pweza,
si nikanywa, weee!”
“Kwa hiyo hapo ungekuwa na mimi
ningekoma leo?”
“Usingekoma, ningekukomesha.”
Mama Sabinamu alijikuta akisisimka
mwili kwa maneno ya kijana huyo
kiasi kwamba aliamini Sudi hana
kitu, kwanza wala hajanywa supu ya
pweza…
“Huyu wala sijamuuliza kasema
mwenyewe, yule mpaka
nimemuuliza, itakuwa kweli,” aliwaza
mwanamke huyo huku akiendelea
kuongea na kijana huyo.
“Hebu subiri, nipe dakika sifuri
nakupigia sasa hivi.”
“Sawa mama.”
Baada ya kuzungumza na kijana
huyo, mama Sabinamu alimtwangia
Sudi…
“Mama nimekaribia.”
“Subiri wewe, achana na kukaribia
kwanza. Hivi umekunywa supu kweli
au maneno tu?”
“Nimekunywa mama.”
“Utaniweza?”
“Aaa, sana! Kwa nini nikushindwe?”
“Haya njoo.”
Mama Sabinamu akakata simu ya
Sudi, akampigia kijana…
“Sasa sikia, eeee….fanya hivi, we njoo
hadi kwenye kona ya Hospitali ya
Mwananyamala, nisubiri hapo, kaa
sehemu, kunywa hata soda
nitakupigia kukuita.”
“Sawa mama. Maana da! Hii supu ya
pweza leo ni balaa humu mwilini
mwangu.”
“Usijali kijana wangu, ee!”
mwanamke huyo akakata simu,
akapokea ya Sudi...
“Nimefika hapa Komakoma mama.”
“Nenda mbele, kata kulia, uliza mtu
yeyote ilipo gesti.”
“Sawa.”
Ndani ya dakika tano, Sudi aligonga
mlango wa chumba alichokuwemo
mama Sabinamu…
“Nani kakwambia nipo humu?”
“Mhudumu.” “Ulimuulizaje?”
“Kuna jimama limeingia humu?
Akaniuliza si yule mama mpenda
vijana? Nikamwambia mimi sijui
kama anawapenda au anawachukia.
Akasema ni huyohuyo, ingia chumba
namba nane.”
“Mh! Hana adabu.”
“Kwani anajua kama mimi mpenzi
wako?
”“Hajui.”
“Sasa kwa nini ameongea hivyo?”
“Akili zake mbovu.”
“Na kweli. Sasa mbona humu ndani
kuna mizigo mingi, ni ya mpangaji
mwingine au?”
Kabla mama Sabinamu hajajibu,
simu yake iliita…
“Subiri subiri, usiongee…ngoja
nipokee simu ya mume wangu.”
Sudi alimkubalia kwa kutingisha
kichwa juu chini…
“Haloo…”
“Upo nyumbani?”
“Ndiyo mume wangu.”
“Hebu angalia dayari yangu hapo juu
ya kabati, ndani kuna sehemu
nimeandika kiasi cha pesa
nilichonunulia kile kiwanja cha
Kimbiji. Fanya haraka, nasubiri na
sikati simu.”
 
Endelea basi, mbona unakata stimu?

Ukirudi naomba uniite
 
Back
Top Bottom