Hadithi hadithiiii: Baba mwizi, mama mwizi, watoto wezi.

Pastor Achachanda

JF-Expert Member
May 4, 2012
3,024
2,000
Baba akayasogelea mahindi akaiba huku anajisemea, "mke wangu na watoto wasinione".
Mama akayasogelea mahindi akaiba huku akijisemea, "mume wangu na watoto wasinione"
Watoto wakayasogelea mahindi huku wanajisemea, "Wazazi wasituone"
Yakabaki mahindi kidogo ambayo hayaibiki kwa namna yeyote. Walichofanya familia hii wakabaki wanakodolea macho kidogo kilichopo. Lakini watoto wakastuka wakawauliza wazazi wao, "mbona mahindi yamepungua"? Mama akawajibu, "muulizeni baba yenu yeye ndiye kichwa cha nyumba". Watoto wakamuuliza baba swali hilo mara kwa mara asitoe jibu linaloeleweka. Mwishoni akatangaza kujiuzulu kuwa kichwa cha familia. Anajivunia nini?Yale mahindi aliyoiba kuna mahali alikuwa anayaficha. Watoto wakaendelea kumuuliza mama. Naye mama akatangaza kujiuzulu kulea familia hii. Watoto wakarudisha mahindi waliyoiba wakatafuta mwekezaji ailee familia hii. Mwekezaji alikuja kwa unyenyekevu akawa mdogo kama piriton. Alivyozoea amevimba sharubu amewanyang'anya hadi ufunguo wa stoo na hati ya shamba.ITAENDELEA...
 

Crispin Nyoni

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
413
195
Hili bandiko limepotea njia au?Maana huku ni Mahusiano, Mapenzi na Urafiki(MMU) sasa haya ya familia yanakujeje?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom