Hadithi Hadithi.....

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
Hadithi Hadithi.....Hapo zamani za kale alitokea mwanaume mmoja anaitwaWANANCHI WENGI, baada ya kufikia umri wa kuoa akamuoa mwanamke mmoja anaitwa CCM. Mwanamke huyo alikuwa mzuri na mrembo sana wakati huo.Waliishi vizuri kwa muda mrefu, lakini baadaye tabia ya mwanamke huyo CCM ilianza kubadilika. Alianza kuwa kiburi ambapo akaanza kumdharau mumewe WANANCHI WENGI na kufuata anasa za dunia.

Akaanza kutembea na wanaume wengine nje ambao baadhi walifahamika kama KUJILIMBIKIZIA MALI, mwingine aliitwa MIKATABA MIBOVU na kijana mmoja dogodogo na mchachari anaitwa UFISADI. Mumewe alipogundua mwanamke huyo hakujali kutokana na dharau yake.Hata hivyo kutokana na kutopenda kujitunza, badala yake kula kula hovyo CCM ilipoteza mvuto, akanenepa sana na alipojichubua kupita kiasi ndiyo kabisa. WANANCHI WENGI baada ya kuchoshwa na visa vya mkewe CCM aliamua kuoa mwanamke mwingine aitwaye CHADEMA.

Mwanamke huyu alikuwa liwazo la mumewe baada ya yule wa awali kuwa hamjali na badala yake kufuata anasa za dunia. Kuona hivyo, mke mkubwa CCM akaingiwa na woga kuwa ndoa yake iko mashakani, akaamua kwenda kwa mganga wa kienyeji aliyeitwa JESHI LAPOLISI.

Mganga huyo alimpa dawa mbalimbali CCM za kumdhibiti mumewe WANANCHI WENGI. Dawa hizo baadhi ya MAGARI YA MAJI YA KUWASHA, MABOMU YA MACHOZI, RISASI ZA MOTO, na nyingine nyingi ambazo zilionekana kufaa ili mume apoe.
Baada ya miaka kadhaa kupita CHADEMA alipata ujauzito na mumewe akasema iwapo atazaliwa mtoto basi atamwita jina KATIBA. CCM naye aliweka matambara tumboni alijifanya mjamzito hadi mwenzake alipojifungua. CCM alimwiba mtoto KATIBA na kujifanya wa kwake, huku akimshutumu mke mwenzake CHADEMA kwa madai amemnyonga mtoto wake baada ya kujifungua na kumzika kisirisiri.

CHADEMA akalia na kusema ameibiwa mtoto wake KATIBA na mke wenzake CCM. Jambo hili lilimshangaza WANANCHI WENGI asijue nini kimetokea na ukweli ni upi, lakini hata hivyo akasema atafanya uchunguzi..........

Hadithi hii itaendelea toleo lijalo
 
Saaaaana tu,thumb up mkulu wa nchito nikimaanisha mkubwa wa kazi!
 
tatizo la wananchi wengi alikuwa goigoi sana. Ilifika wakati mkewe wa kwanza alimtukana sana eti ukila lazima uliwe...
 
Back
Top Bottom