Hadithi: Gamboshi

SEHEMU YA SABA (7)

Alitoka mpka nje alikuta watu wakiwa wamejaa wamezunguka maiti ya binti yule ambae wamemaliza kumtoa mtoni mda si mrefu, afande baraka na mzee walikuwa wamesimama pembeni wakiwa wanamsubiri
“Nini kinaendelea”
“Familia ya marehemu imekuja inataka mwili wa binti yao”
“Hicho kitu hakiwezekani”
“Kimila na desturi ni vema mngewapa mwili wa binti yao” yule mzee alimwambia afande mwita bila kupepesa macho huku afande baraka akibaki kimya
Sababu ya afande mwita kukataa alikuwa anahitaji kufanya upepelezi wa nani kafanya hivi na kwa nini kama ilivokuwa kawaida akipata kazi kipindi cha nyuma
“Naombeni tuskilizane”
“Naomba nifahamu familia ya huyu binti” alinyoosha kidole na kuuliza
Walijitokeza mama mmoja akiwa na binti mdogo wa miaka 17 kwa pembeni yake
“Samahan we ndo familia ya huyu binti aliyelala hapo”
“Ndio”
“Ni nani yako”
“Ni mwanangu mimi mama yake mzazi “
“Kwanza mama nikupe pole”
“pili mimi naitwa mwita ni askari wa jeshi la polisi nimekuja na mwenzangu”
“Baraka” afande Baraka alijitambulisha
“Lengo la kuja hapa ni kurudisha amani na pamoja haki na uhuru wenu kama wanakijiji”
“Pia kutokomeza vitendo vya kikatili kama hivi, Kwahiyo nakuomba tubaki na mwili wa binti yako” akaongezea huku akimtzama mama yule machoni.
“Sawa” alijibu na kugeuka akiwa na binti yake bila kuongezea chochote na kuondoka pale
Afande mwita alishusha pumzi tena na kumwita afande baraka waweze kurudisha ule mwili kwenye gari yao ya jeshi la polisi, Afande mwita alimfata yule mzee na kumuuliza ni wapi wanaenda kufungua kituo chao basi mzee yule alikubali na kuwapeleka mpka eneo lenyewe kilikuwa ni chumba ambacho kilitumika kama sungu sungu miaka ya nyuma lakini mazingira yalionesha hakijatumika kwa muda mrefu sana walikuta uchafu kwa wingi sana huku panya zikiwa zimekufa kila mahari na wadudu wengine
“Hii sehemu inanuka kama buka man” Afande baraka alikuwa akijiuliza
“BUKA MAN NDO NANI”yule mzee aliuliz
“Ni kitabu tu hata sio hadithi ya kweli”Afande mwita alimjibu
“Mnamanisha BUKAKILAMA SIO BUKA MAN”
“Na alikuwa sio mwanaume alikuwa ni mwanamke” akaozengea
“Inaonesha unamjua ni nani” Afande baraka alishangaa badaa ya yule mzee kuongea lile neno
“Sijui chochote “ yule hakutaka kuendelea na mazungumzo na aliondoka na kuacha wafanye usafi kwenye hilo eneo
“Wanawake wa hivo huwa wanafaa w apatane na bishoo kama wewe”
“Nani?”
“Bukakilama”
“Me nioe mchawi”
“Ata ivyo mapenzi uchawi”
“Kwahiyo we umerogwa”
“ Na nani sasa Veronica au Janeth “ afande baraka aliuliza na kumwacha afande mwita akimtazama tu huku akitabasamu, sababu afande mwita alikuwa anafaham afande baraka ni mtu wa matani sana kwahiyo hakujibu swali lake
“Embu tufanye kazi iliyotuleta hapa”Afande alimjibu na kuendela na shughuli zingine akiwa anaendelea kufanya usafi alikota karatasi moja ambayo ilikiwa imekunjwa na kuikunjua alikuta ilikuwa ni ramani flani ambayo kwa wakati huo akuielewa lakini aliona kuna rangi ya mduara mwekundu ulikuewa umezungushiwa kwenye ramani ile aliikunya kama alivo ikuta na kuiweka mfuko wa nyuma
Aliendelea kufanya usafi lakini simu yake ya mfukoni iliita alitoa na kuangalia alikuwa mkuu wa kituo cha polisi mkoa wa simiyu akifahamika kama Njegele kulwa alipokea
“Hello”
“Habari yako Afande” Alikuwa ni mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa simiyu bwana
Huku mwita kiendelea kuongea na maongezi simu ya afande baraka pia iliita alitoa mfukoni na kuangalia alikuwa ni veronica alipokea
“Hello”
“Mambo Vp shem”
“Acha basi masihara baraka”
“Haya safi nambie”
“Mbona napiga simu ya mwita hapokei”
“Yupo anaongea na simu nyingine”
“Ooh okay”
“Na mnaendeleaje hapo”
“Tupo tunafanya usafi, japo tulikuwa na changamoto kidogo”
“changamoto gani?”
“Tumepata maiti kipindi tunarudi kijijini”
“Mungu wangu”
“Ndio na Familia ilikuwa inataka kuchukua mwili ikazike leo lakini na sisi tunafata sheria”
“Lazima maiti ifanyiwe uchunguzi”Veronica alimalizia
“Ndio”
Maongezi yakiendelea kwenye simu baina yao wawili Afande baraka aliskia akiitwa ivyo alimwaga na kukata simu kwenda kuskiliza alikuwa akiitiwa nini
“ulikuwa unaongea na nani”
“Dem wako!”
“NANI?”afande mwita alitahamaki
“Veronica” Afande baraka alijibu bila wasiwasi
“kapiga akitaka kujua unaendeleaje akaona aulizie tunaendeleaje”akaongezea
“Ukamjibuje?”
“Tunaendelea vizuri sana”
“Na wewe ulikuwa ukiongea na nani”
“Njegele”
“Anasemaje”
“Alikuwa anaulizia maendeleo nikamwomba aniongezee askari wawili”
“Kakubali”
“Ndio”
Walimaliza maongezi hayo mafupi na kuendelea na kazi hadi saa moja jion wakiwa wamefika asalimia 90 ya marekebisho na usafi ukiwa umeenda vizuri mzee yule ambae mpaka saa hamna kati yao anaemjua jina alifika na kupeleka mpka mgahawani kwenda kupata chakula walipofika mgahawani waliagiza na kukaa lakini akiwa amekaa anasubiri chakula afande mwita aliangalia kwa njee na kuona dada mrembo sana na kutokewa kuvutiwa sana alijikuta akimtazama mdada hakika alikuwa mrembo sana akiwa kasuka rasta rangi yake kama mtoto wa uchagani lakini hakupata nafasi ya kusemesha sababu yeye alikuwa kwa ndani na mdada alikuwa kwa nje.
Walimaliza kupata chakula na mzee yule kuwaambia waende moja kwa moja kula na wao walimskiliza ikiwa ni siku yao ya kwanza wamemaliza wakiwa kijijini gamboshi walikuwa wachovu sana ivyo kila mmoja alipata maji ya kuoga na kwenda kupumzika kitanda
“Huwezi kuamini kipindi naambia watu watawanyike pale mtoni nilikuwa na hofu labda wanaweza kupinga”afande mwita akimwelezea afande baraka huku akiwa amelala chali
“Hata kipidi naongea na yule mama nilikuwa na hofu sana, nilikuwa nikimtazama machoni naona kama anahasira sana na mimi au dunia nilikuwa sielewi” aliendelea kuongea huku afande baraka akimskiliza kwa makini sana akiwa yupo kitandani pia
“Hawa watu wameumia kwa mda mrefu na wanaitaji matuamini tena labda wewe unaweza kuwa shujaa wao”afande baraka akimwelezea mwita kwa nini hao watu wako hivo
“Siku zote umekuwa shujaa kwenye kila kitu, unakumbuka ulisadia maisha yangu “
“Siwezi kusahau iyo siku”
“hata hawa unaweza wasaidia”
Mda wote afande akiwa anaongea afande mwita alikuwa kimya
“Unajua nini siku zote nimekuwa shujaa kwenye mambo yote kumbuka na wewe ulikuwa nyuma nyangu, na saizi upo na mimi kwenye kufanya hili jingine”
Walisamama na kugonga tano huku wakihadi kusaidia hiki kijiji ,Afande mwita alipo rudi kitandi alikumbuka kuna zawadi alipewa na mke wake kipindi anaondoka nyuma alikulupuka na kutoka nje huku afande baraka akiwa tayaru kashapitia na usingizi baada ya maongezi yale alifika kwenye gari kufungua ilikuwa kwenye dashboard alichukua na kurudi ndani alifika na kukifungua kile kiboski alikuta kuna rozari ya wakristu ambayo imetengenezwa na madini ya shaba alifurahi sana huku ndani kukiwa na ujumbe mfupi wa maandishi “NI BUSU KABLA HUJALALA” hakika alibusu huku tabasamu likiwa limetawala uwo wake aliwaza kumpigia mke wake lakini aliona mda umeshaenda hivyo aliahid asubuhi atakuwa mtu wa kwanza kumpigia.
 
Sehemu ya saba iko tayari karibuni msome wapendwa na wapenzi wa gamboshi aisee poleni sana kwa kusubiri naona wafuatiliaji mmekuwa wengi sana nashukuruni sana
 
Picha ndo kama limeanza hivi afande mwita kama namwona shusha like na comment yako niendelee kuweka kazi nzuri
 
Huu uandishi mbona unaboa sana kuelewa jamani?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…