Hadithi: Gamboshi

Sehemu ya tatu hii hapo mkimaliza kusoma natamani kuskia maoni yenu mpka hapo
 
Ni hadithi au ni simulizi ya kweli?
 
SEHEMU YA NNE

Tarehe 19 mwezi wa 3 mwaka 1999 siku iyo kulikuwa na sherehe kubwa ya binti aitwae Anjella kunti alikuwa akitimiza miaka 12 hapo mzee kunti akiwa ni baba yake mzazi, alikuwa mwenye furaha sana huku anjella akiwa ni mtoto wake watu tatu huku wa kwanza akiwa anaitwa john pamoja katerina. Kunti akiwa ni mtu mkubwa sana kijiji hapo basi sherehe ilileta watu tofauti kutoka ndani na nje ya kijiji watu wakubwa viongozi mashuhuri lakini wao walikuwa wamekuja kwa kuzungumza mambo amabayo yalikuwa hayahusiani na sherehe kabisa, hata njisi walivoingia hamna aliyekuwa anajua wapo kwenye sherehe hiyo alikuepo katibu mkuu wa chama tawala mwenyekiti wa chama pamoja na raisi wa jamuhuri ya muugano wa Tanzania ilikuwa ni sehemu ya siri kabisa na maongezi yalipo kuwa yakiendelea mtoto wake na mzee kunti akiwa anazunguka ghafla alisikia watu wakibishana
“Naomba uniambie nini kinahitaji kuipata iyo dawa chochote nitakupatia” Mh rais alikuwa akizungumza na mzee kunti kuhusu dawa anayohitaji, nini kinahitaji mpatie aweze kumsaidia
“Mh Rais naelewa na nakuheshimu sana lakini unachohitaji kiko nje ya uwezo wangu sizani kama naweza kukusaidia”
“Tumekuwa marafiki kwa mda mrefu staki kuona hiki kitu kikifunja urafiki wetu”
“Fanya unavoweza hakikisha unanipa majibu kabla ya wiki mbili hazijaisha” aliongezea kisha akaondoka na akiwa na viongozi wenzake waliokuwa wamemsindikiza
John akiwa kajibanza pembene aliskia mazungumzo hayo na alibaki anajiuliza ni dawa gani baba anaombwa na Mh rais
Siku iyo mzee kunti alikuwa yupo mezani peke akiwa na gazeti mkononi na maji ya kunywa pembene akiendelea kusoma mwanae wa kiume john alikuja na kukaa pembene
“Hali ya hewa leo nzuri sana” john aliuliuza huku akimzatama baba
Mzee kunti alimtzama mtoto wake na hakujibu chochote
“Hivi unazan mtu kama mh rais huwa anashida yoyote” john aliendelea kuongea
“sababu anakila kitu pesa, nguvu lakini baba kuna vitu anahitaji huku akiomba”
Mzee kunti alimtazama mwanae na kumuuliza
“unataka nini”
“nataka nikusaidie”
Mzee kunti alicheka na kuuliza
“wewe unisaidie na nini”
“Mimi ndo mtu pekee nae jua kwamba mh rais alikuepo hapa siku ya sherehe ya anjella na sijamwambia”
“ata mama sijamwambia”Aliongezea
Ghafla sura ya mzee kunti alibadilika na kuongea akiwa anamtazama mtoto wake machoni
“ulichokiona au kuskia kiishie pale nikiskia kwa mama yako ntakufanya vibaya “mzee alimwambia bila kupepesa macho
“siwezi kuongea chochote nataka nikusaidie” ingiwa na vitisho john alimjibu baba yake
“nambie Mh rais anataka dawa gani”
“Hili swala halikuhusu niache mimi na wewe uendelee kufaanga mdomo wako”
Mzee kunti alikataa msaada ambao alikuwa anataka atoe mwanae japo alikuwa hajui anataka kutoa msaada gani alichomtaka ni asije kuskia izo taarifa kwa mama yake kwahiyo alimtaka afunge mdomo
John akiwa ni mtoto wake wa kwanza alikuwa na umri wa miaka 16 kwa mira na desturi za kijijini hapo alikuwa tayari kashatambulishwa kwenye mizimu na alikuwa na uelewa na baadhi ya mambo aliyokuwa akifundishwa na babu yake.Mzee kunti alibaki na mawazo mengi sana akijiuliza vipi mwanae alikuwa anataka kutoa msaada gani. Baadae jioni wakiwa wako wanaendelea kupata chakula cha jioni mzee kunti alikuwa bado hajafika mezani ki mila walikuwa hawatakiwi kuanza kula kama baba wa familia hajakaa mezani kwahiyo mama alimwagiza john aende kumwita baba yake john alinyanyuka na kwenda kumwangalia baba aliingia mpka chumbani wanapo lala wazazi wake huku akiita baba lakini kulikuwa kimya alivoendelea kuangaza aligundua kuna kama mlango mdogo sana upo wazi aliuzatama na kufikiria unaelekea wapi sababu ulikuwa mlango mgeni kwake aliingia na kuwacha wazi kidogo alifika mpka ndani huku kukiwa na mishumaa kusaidia kuona kwa mbali aliona mtu alivojaribu kutazama vizuri alikuwa ni baba yake mzee kunti aliposkia sauti alikuwa na nguvu ya kufunga akili ya mtu basi alifunga akili ya mtu bila kujua ni nani na kutokezea nyuma ya huyo mtu ndipo aligundua mwanae
“Anatafuta nini huku huyu” alijiuliza kwa hasira sana
Kwa uwezo aliokuwa nao alikuwa anaweza kufunga akili na kukufanya usahau vitu vilitokea mda mfuopi aliopita sasa aliwaza sana amfanayaje mwanae kumfungua ni kama kumwonesha iyo sehemu aliwaza kipi kitakuwa sahihi akaona mfungue tu
“Baba” alikuwa ni john baada ya kufungulia akili
“unafanya nini huku” aliongezea
“Mama kaniagiza nije nikuite tukale”
“Njoo nikuoneshe” Mzee kunti baada ya kumtazama alimwita huku akiendelea kutembea
John alimfata taratibu baba yake anapokelea, walifika sehemu kuna sinia likiwa na maji na makabati mengi mzee kunti alielekea kwenye moja ya makabati na kutoa kitabu kidogo na kumpatia john
“Fungua ukarasa wa kumi na moja”alikuwa ni mzee kunti akimweleza mwanae
John alifanya hivyo
“Haya soma inasemaje” aliongezea
“Mimi kama mkuu na mwakilishi wa mizimu naapa kuitumikia mizimu kwa uaminifu bila kufunja sheria wala desturi za kijiji” john alimaliza na kubaki akimwangalia baba yake
“Fungua ukurasa wa sita “ mzee kunti aliendelea kumwambia afungue kurasa mwingine
John alifungua tena kwa mara nyingine
“Soma”
“Zifwatazo ni sheria za mila na desturi za mizimu, moja usidanganye mizimu pili usifanye maamuzi bila kuhusisha mizimu tatu usifanye kafara kumuhudumu shetani”
“Haya maji unayoyaona hapa ni hatari sana usije ukawahi kuyashika wala kugusa ni hatari sana” aliendelea kumkazia kuwa yale maji anayo yaona ni hatari sana
Mzee kunti alimwambia mwanae na kumwelewesha kwamba babu yake alikula kiapo mbele ya mizimu lakini bado alifanya kinyume na kuizunguka mizimu na kupelekea kutokea maafa makubwa sana hayuko tayari kufanya ivo tena . Alichukua kitabu alichokuwa amempatia na kukirudisha alipo kitoa na kumwambia mwanae aongeze njia watoke nje, sehemu hiyo ilikuwa ya siri sana hata kipindi john anaingia aliacha mlango wazi lakini kipindi anarudi alikuta pamejifunga .
Basi mzee kunti alipafungua na kuelekea mpka mezani kupata chakula cha jion , john alibaki na maswali kesho yake asubuhi na mapema alijia ni mtu mmoja pekee ndo anaweza kujibu maswali yake na si mwingine ni babu yake kulikuwa na moja ya jengo kubwa pale kijijini lilikuwa limeandikwa “kwa mkombozi” humo ndani ndo alizikwa “ZAWA KEWA KUNTI” babu yake John.
Yalikuwa ni mazoea yake toka yuko mtoto kuongea na babu kila anapokuwa na shida lakini kwa kipindi hiki alikuwa hajaongea nae kwa kipindi kirefu baada ya kupigwa maarufu na baba baada ya kugundua mwanae anafundiswa uchawi.
Alifika mpka ndani kawaida ilkuwa lazima utoe salama na uchukue kisu kilicho pembene utoe damu kidogo uweke kwenye kikombe kilikuwa mezani kwa mbele kiufupi mazingira ya mule ndani yalikuwa yanafanana na makanisa ya wakatoliki. Baada ya kufata kila kitu alipa goti na kusuburi ghafla aliskia sauti
“Mjukuu wang”
“Naam babu”
“Unaendeleaje”
“Naedelea vizuri”
Yalikuwa ni mazungumzo ya john na babu yake.
Babu yake alitambua mjukuu anashida ikambidi aulize
“Una shida gani mjukuu wangu”
“Ni baba”
“kafanya nini”
“Mara ya mwisho alinikataza kuja kuonana na wewe”
“Pili kuna jambo ananificha hataki kunambia wala hajamwambia mtu yoyote”
“Na…” alisita alichokuwa anataka kuuliza
“Nambie mjukuu wangu wala usiwe na wasi wasi”
“Ni kweli ulisaliti mizimu”
“Hapana mizimu ndo ilitaka kunisaliti mimi baada mimi kutaka kuishi kitakatifu, nilikuwa nataka nibatizwe niwe mkristu mizimu ilikataa na kupanga njama za kuniua ndo mpka leo unaona zimezikwa kwenye kanisa hili la wakatoliki”
“Baba yako hataki kuona huo ukweli mimi ndo nilizungukwa” alishusha pumzi na kuendelea
“Saiv baba yako anapanga kutoa kafara na ni kafara haramu”
“la kumuhudumu shetani” John aliuliza
“Ndio”
“Kwa nini baba anataka kufanya hivo” John aliuliza tena huku taarifa iyo ikiwa imemfunja moyo
“Sijui lakini nataka nikusaidie na wewe umsaidie baba yako”
“Niskilize kwa makini mda mrefu hakujakuwa na sikukuu ya kusafishwa kwahiyo nataka uirudishe tena na unahitaji baadhi ya vitu kufanya hivo”
“Vitu gani”
“Kuna chumba katikati ya chumba ya baba yako na mama yako wanapo lala kile chumba ni dhahabu kuna kila kitu unachohitaji”John hakuelewa akauliza
“Chumba ambacho kuna sinia kubwa linamaji”
“umeshawahi kufika humo ndani” mzee zawa alishangaa sana baada ya kujua kwamba mjukuu wake anakijua hicho chumba na ilikuwa faida kwake alianza kuona kama mpango wake unaanza kwenda anavotaka
“Ndio, ilikuwa ni jana nilimkuta baba akiomba”
“Vizuri yale maji uliona ndo unayohitaji pamoja na kitabu kilicho ukuta wa tatu”
“Usiniulize maswali mengi ukishakamilisha njoo navyo kwangu”
Lakini bila kujua kila kitu alichoambiwa na babu yake kilikuwa ni uongo na baba yake alikuwa na mipango mingine kabisa wala sio kusaidia mtu.
 
Kwenye hii simulizi ndo kama tunaanza kuna uchawi mpka mtashangaa nawa ahid hutajuta kuisoma simulizi hii
 
Na kitu cha tofauti najaribu kufikilia ambacho kitaleta mamillion kuja kusoma kitabu changu nipen muda sehemu ya tano ni alhamisi
 
SEHEMU YA TANO
Ilikuwa jumapili asubuhi alfajiri ya saa kumi na mbili na robo [06:45] afande baraka akiwa anajinyoosha taratibu kitandani baada ya usingizi mzito na uchovu walikuwa na baada ya kutembea umbali mrefu mpka kufika kijijini hapo hatimae aliamka alikuwa ndani ya nguo zake za jeshi la polisi pembene kulikuwa na kitandana kingine ambacho alikuwa amepumzika afande mwita. Afande baraka alitoka kitandani na kuvaa jaketi lake kilikuwa chumba kikubwa sana alikitzama kwa makini kisha kuelekea mlango
“Huyu mzee alitufungia mlango sijui yuko wapi” alikiwa akijiuliza huku akielekea kushika kitasa cha mlango
Lakini alishangaa baada ya mlango kufunguka alitoka njee alichokioona hakuamini macho yake
Kulikuwa na watu wengi sana tofauti na walivo ingia jana yake usiku palikuwa kimya ndege zilikuwa zikilia juu ya miti na watu wakiendelea na shughuli zao kiukweli ile sehemu ilimfutia sana akiwa bado anatahamaki mazingira afande mwita nae alikuwa anaamka kutoka kitandani alifika mpka nje na kubaki ameshangaa
“Kaka tumeamka mkoa gani huu” Afande mwita alimuuliza afande baraka
“Sijui kaka”
“Habarini za Asubuhi”ilikuwa ni sauti ya mzee aliyewaleta jana akiwapa salam
“Salama tu”walimtazama na kuitikia wote kwa pamoja
“Poleni na safari pili msiongeleshe mtu msiemjua”
“Kwani tunamjua nani huku” Aliuliza Afande baraka
“Ndo nacho jaribu kusema hamna mnaemjua na kuongelesha mtu usimjua”
“Kingine jana mliacha gari itabidi mlifate ndo mambo mengine yaendelee”aliongezea
“Sawa.” waliitikia wote kwa pamoja
Basi aliwambia wamfate na waendee kufata gari walipo liacha jana usiku baada ya kuchelewa kufika na kutumia njia ya miguu kufika kijijini, lakini kilicho washangaza ni walitembea umbali mfupi sana
Kama dakika 15 tu kufika ambapo gari waliliacha usiku wa jana
“Kwa nini hatukutumia hii njia jana”Afande baraka aliuliza
“usije kujaribu kupita hiyo njia mida ya usiku” alijibiwa maneno machache sana na kiukweli aliogopa kuskia ivyo
Walikuta gari ikiwa kwenye usalama ulele waliliacha nao afande baraka ndo alikuwa na ufunguo basi ndo alichukua jukumu la kuendesha gari walifungua milango na kila mtu kuingia kwenye gari simu ya afande mwita aliita alitoa jina lilikuwa ni “Veronica” Alitoa tabasamu kigodo n huku afande baraka akichungulia kwa mbali akitamani kujua ni nani kapiga simu, afande mwita alipokea simu
“Habari za asubuhi mtoto mzuri”
“nzuri tu”
“Umeamkaje?”
“Salama vp nyie”
“Salama kabisa”
“Mama anaendeleaje?”
“Anaendelea vizuri nilikuwa nimemaliza kumlisha hapa”
“Basi ni habari njema kuskia ivo”
“Kweli kabisa”
“Nambie” Baada ya kusalimia na kujuliana hali, afande mwita alitaka kujua kwa nini veronica kapiga asubih

“Naomba niongee na mwenyeji wenu” aliomba aongee na mzee aliewapokea na kuwapeleka mpka kwenye makazi walipofikia
“Sawa” afande mwita alikubali na kumpatia simu mzee yule alikuwa kakaa siti ya nyuma kwenye gari
Mpaka sasa walikuwa bado hajui mzee anaitwa nani na kilicho washangaa sana ni baada ya kumpa simu maongezi yaliyoenda walibaki na maswali mengi
“Naam” mzee alishika simu huku akiitika
“Ndio”
“Hapna”
“mh”
“Ndio”
“Ndio”
“Sawa” Alimaliza na kuludisha simu kwa afande baraka
Sababu walikuwa hawawezi kuskia alichokuwa anaongea veronica waliishia kuskia majibu ya mzee tu ambayo walishangaa kwani walikuwa wanazungumza nini
Afande Baraka aliwasha gari na kuondoa kuelekea kijijini
“una mahusiano na veronica” Swali ambalo liliwafanya wote wageuke nyuma na kumwangila mzee
“ Hapana mimi na mke” afande mwita alijuwa swali lilikuwa linamlenga yeye basi alijibu
“unamwonaje kwenye kazi yake anaweza” aliuliza kwa mara nyingine tena
“Ndio anaweza ni mwanamke ambae kiukweli huwa ananishangaza sana an
aujasiri sijui kalisi kwa nani”
“na huwa ni mtu anajari kila mtu”aliongezea
“Sasa kwa nini cheo chake hakipandi siku zote”
Afande mwita alishindwa kujibu ilo swali na kubaki akimwangali mzee kupitia kioo cha mbele ya gari
“Lakini huwa anatabasamu sana akiona simu ya veronica” alikuwa ni afande baraka akiwa anajaribu kupunguza ukimya uliokuwa umetawala
“Embu acha masihara”
“Kwani uongo” Afande baraka aliuliza kwa matani tena lakini afande mwita hakujibu kitu alitabasamu tu.
Safari ikiwa inaendelea waliskia sauti kwa mbali ikipiga kelele afande baraka alifunga breki na kusimamisha gari waliskiliza kwa makini ni kweli kelele hizo zilikuwa zipigwa sio mbali na hapo basi walishuka na kuelekea mpka eneo la tukio walikuta watu wamekusanyika wengi afande mwita kutazama vizuri aliona mtu akiwa amelala kifudifudi kwenye maji kando kando ya dimbwi huku mwita akisogeza watu pembene kidogo afande mwita alipima kama mtu huyu bado yupo hai kwa kuweka vidole shingoni aligundua mtu yule kashafariki mda alisimama na kuendelea kuangalia mazingira yale alioona watu wawili wakiwa kwa mbali sana mmoja akiwa yuko ndani ya nguo aina ya suti alikuwa ni mwanaume mweye urefu inch 7 na akiwa na miwani pia rangi yake ilikuwa maji ya kunde sababu alikuwa basi hakuona sura yake vizuri afande alimtazama sana kisha kumwita afande baraka waje wasaidiane kuubeba mwili ule.
Walipo ugeuza mwili alikuwa ni binti wa umri kama miaka 25 afande baraka alirudi kwenda kusogeza gari iliwaze kuuweka mwili kwenye gari yao inayofamika kama defender alipoweka gari alishuka pamoja na yule mzee alimfuata nyuma kusaidiana kubeba maiti ya yule dada walipo maliza kuweka ilibidi afanye utaratibu watu watawanyike
“Naomba tuskilizane” afande mwita aliongea kwa sauti ya juu
“Kwa usalama wa kila mmoja wetu naomba turudi kwenye majumba yote tukae ndani” Basi alitoa maagizo hayo na watu walitawanyika na wao walipanda gari na kuondoa hata ivyo walikuwa wameshafika kijijini huku afande mwita akiwa na maswali mengi nani atakuwa anahusika na kwa nini wamtupe mtoni alishuka haraka kwenye gari na kuelekea chumbani akiwa anafungua mlango simu yake ya mkononi iliita alitoa mfukoni na kuangalia alikuwa ni imeandikwa “Wife” alipokea
“Jamani we mwanaume unataka kunitoa roho mimi” ilikuwa ni sauti ya mke wake kwenye simu akiuliza
“Hapana”
“Umeamkaje”afande mwita akaongezea baada ya kukataa sio kweli
“Sitaki” mke wake alijibu kwa kinyonge
“Nisamehe mpenzi wangu”
“kweli toka jana usiku hupokei simu”
“nilifika nimechoka alfu nimeamka na kazi kidogo”
“Sawa “
“umesha…” mke wake akiwa anataka kusema kitu ghafla afande baraka alikuja chumban na kumwita
“kaka njoo uone kitu mara moja” afande baraka alihitaji afande mwita aje aone kitu ambacho wenda anaweza toa msaada wowote
“Ntakupigia baada sawa kipenzi changu”
“Nakupenda , bye” alimalizia na kukata simu huku akitoka chumbani kwenda kuangalia nini afande baraka anamwitia.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…