Hadithi: Binti wa Mjini

Hadithi: Binti wa Mjini

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,764
Ilikuwa ni usiku wa manane nikiteremka basi kutokea Zambia ,nikiwa katika mihangaiko ya kusubiri tax itakayopita bila ya mafanikio ,ghafla ilinipita gari ndogo na kufunga breki kama mita 50 kutoka nilipo simama ,na ikarudi kinyumenyume kwa mwendo wa kasi na kunisimamia si mbali na miguu yangu ,ilikuwa na vioo vya kiza kwa vile sikuweza kumuona alie ndani ya gari ,mawazo na nilijuavyo Jiji la Daresalama ,niliingiwa na hofu ya kukutwa na jambazi nikasogea kwa mwendo wa kasi kuelekea pembeni ,nikasikia sauti ya kike ikiita Sebastian.....ITAENDELEA WIKI IJAYO(Hii inatungwa hapa hapa nakaribisha wengine kuchangia)
 
Nikaitikia na kumsogelea nikagundua ni msichana tuliye soma wote o level nikaenda naye mpaka kwake masaki... ITAENDELEA WIKI IJAYO.
 
Nikaitikia na kumsogelea nikagundua ni msichana tuliye soma wote o level nikaenda naye mpaka kwake masaki... ITAENDELEA WIKI IJAYO.

kwakweli ana maisha mazuri sana na aliishia kidato cha nne tu,, nakumbuka mara ya mwisho kuonana ilikua siku ya mwisho ya mtihani wetu wa kidato cha nne aliniaga anakwenda Arusha siku mbili baadae na atakwenda kuishi huko huko niliumia sana maana nilikua nampenda na sikuwahi kumweleza, tuliendelea kuwasiliana kwa muda lakini mara baada ya majibu ya mitihani kutangazwa huo ndio ukawa mwisho wa mimi na yeye kuwasiliana. kwa upande wangu majibu yalikua mazuri lakini kwake hali ilikua kinyume. niliendelea na maisha yangu bila kujua alipo nakumbuka nilikutana na rafiki yangu mmoja jijini dar akaniambia mary(binti wa mjini) yupo hapahapa dar ila hakujua ni wapi makazi yake. nikajipa moyo ipo siku nitakutana nae. mwaka mmoja baada ya kumaliza chuo nikapata fursa ya biashara nchini Zambia katika kampuni moja ya huko ilikua inahusika na kutafuta masoko ya bidhaa zao nchini Tanzania nilihamaki baada ya kuona jina la Mary Mateo ndie mkurugenzi wa kampuni ile hakika hili jina halikua geni kwangu nilihisi itakua ni yeye lakini nikatatizika nilipokumbuka nilipata taarifa kwamba Mary ni mama ntilie maeneo ya jangwani na ni taarifa nilizothibitisha kwa macho yangu nilipopita maeneo yale nikiwa katika bodaboda nawahi ofisini sikupata muda wa kumuongelesha ila niliweka azma ya kurudi pale nikitoka ofisini.. kwa bahati mbaya nikapata safari ya kikazi ghafla nilitakiwa kwenda mkoani Morogoro asubuhi ile ile na kwa bahati mbaya nikatakiwa kulala hukohuko... ITAENDELEA MUDA WOWOTE kaa tayari
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom