hakuna kazi ya kudumu milele
hata wewe kama umeajiriwa usiridhike hapo ulipo
tafuta sehemu yenye maslahi zaidi kuongeza wigo wako wa kufanya kazi
ni sawa na wachezaji wanaohama club.
eeba nae,sasa inakuwaje tena manake yule ndiye kinara wa RFA
sasa kuna yule mkongo zuberi ndiye wanamtumia kwa kila kitu
hawezi kukataa kwa sababu akifukuzwa inabidi arudi kwao kongo
eeba nae,sasa inakuwaje tena manake yule ndiye kinara wa RFA
sasa kuna yule mkongo zuberi ndiye wanamtumia kwa kila kitu
hawezi kukataa kwa sababu akifukuzwa inabidi arudi kwao kongo
RFA nayo kama Arsenal.
Inanoa majembe kisha wakulima wanakuja wanabeba.
Maremu Deo Kiduduye,Godwin Gondwe,Gabriel Zakaria,Kid Buoy,Sky Walker,Gabriel Yotam,... List ni ndefu sana ati..
Sasa atakuwa amebaki Uncle Sam na Mtoto wa Mama Sabuni tu!
Kuhusu Tontoo Zuber Msabaha,huyu sio mkongomani (kwa ufahamu wangu) ila ni mzaliwa wa Kigoma, likely Mmanyema. Halafu kuna Jamaa mwingine anatangaza kipindi cha Viva Africa kwenye Ebony Fm huko Iringa anaitwa Almasi Msabaha;na yeye anadeal na mambo hayo ya mabolingo,anafanana na Tontoo hadi sauti,sasa sijui kama ni ndugu,au mmoja ni role model wa mwingine!
RFA NA STAR TV,ziliimarika sana,kitendo cha mmiliki wa sahara media A. Dialo kuingiza u CCM kwenye kazi kimeharibu kabisa ladha ya vyombo hivi. Namshauri na Yahaya Mohamed ahame.
Nadhani huyu ni Fredwah anataka aone popularity yake iko kwa kiasi gani. Kama wewe siye basi huna haja ya kutupotezea muda mpigie simu umjulishe unashangaa hayuko RFA.