Hadi 2020 kila mtu atakuwa ameguswa

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,634
7,010
Leo nimekutana na msomi mmoja hana ajira na umri wake umezidi miaka 30.Awali alikuwa akifurahia sana watu kutumbuliwa wakiwa na tuhuma ya kuwa na vyeti bandia.Pia alikuwa akisifu sana hatua zinazochukuliwa na serikali hii katika mambo mbali mbali ikiwemo lile la kuorodhesha wanafunzi feki.

Sasa nimegundua kuwa kufikia mwaka 2020,hakuna atakayebaki salama kwani ukikoswa kwenye vyeti,utapatwa kwenye umri,ukikoswa kwenye umri,utapatwa TRA,ukikoswa TRA utapatwa kwenye mkopo wa loan board.Nina uhakika hakuna pa kutokea.

Wengine walilima mazao yakakauka,benki urasimu umeongezeka mara dufu,kwenye siasa nako hapatoshi!Na bado bomoa bomoa na kodi za viwanja na mashamba.Hakika hakuna atakayeachwa kipindi hiki.
 
Suala la umri wa miaka 30 kutoajiriwa limeshakanushwa! Halina ukweli wowote ndani yake
 
Tulivyo mbuzi mbuzi tutawachagua tena
Kupiga kura katika mfumo wa Tume isiyokuwa huru ni geresha tu. Wanaoamua nani awe rais na wabunge wa upinzani wawe kiasi gani ni KITENGO. WaTz wa karne ya 21 ni welewa sana, Kama wangeachwa huru kuchagua na uhuru wao ukaheshimiwa, leo tungekuwa tunazungumza lugha nyingine!
Tukubali tu kuwa wapole kwa mtukufu chaguo la Mungu, Rais wa wannyoge, shujaa asiyejaribiwa (MCMRWSA)
 
Hadi 2020 kila mtu atakuwa ameguswa .
Nakubaliana nawe kabisa, mie hapo naona kodi itazidi kuniumiza, ila poa tu, kama kweli ni kwa ajili ya kuiacha TZ vizuri kwa vizazi vyetu vijavyo sawa kabisa, tulikuwa tunaishi maisha "fake" kabisa, nimeshajitayarisha, pombe mara moja kwa wiki, tena natoa ofa kwa atakayerudisha mapigo, otherwise NO, nyama mara moja au 2 kwa wiki, maharage mara 2, mboga za majani kibao na matunda, nahisi pia kama mwili wangu uko poa kidogo aise, maana maharage na mboga za majani yalisahaulika hapa nyumbani, safi kabisa, acha hivyo miaka 2 iliyopita mama watoto nimeshuhudia akitupa mikate na mboga eti zimechacha, mara kadhaa...Kwa sasa thubutu, hata ka friji kamepwaya aise..tutaisoma namba kweli..Ila poa tu
 
Hivi huko serikalini kuna kitu gani mbona watu wengi wanakufagilia sana?
 
Waliokua wapigadili ndio wanaolalamika
Watu kama wewe walikuwepo Zambia majority walivyokuwa wakipinga serikali tawala minority walisema wanaopinga ni wavivu yalipokuja mabadiliko hao minority hawakukataa nyongeza za mishahara, hawakukataa ongezeko la miundo mbinu n.k, maana yangu ni hii kwenye maafara wa mamba KENGE hawakosi.
 
Back
Top Bottom