Mkuu, nani pia maandiko yamemtaja kuwa ndiye anayetangaza mtu kuwa mtakatifu? Mind you, utakatifu tunaongelea ni kuwa 'saint' (canonical declaration that a believer is formally reconised as examplary in living his or her faith). Ni tofauti na 'holy'. Kwa maneno mengine ni Mungu ndiye anayewafanya binadamu kuwa holy na wakati huohuo ni binadamu ndio wanaoshuhudia ambacho Mungu amekifanya ndao mwao. Kama binadamu atashindwa kutambua kuwa fulani ameishi vizuri, atashindwa pia kutambua kuwa Mungu yupo au ndiye anayemwongoza kutenda mema hapa duniani.
Hebu angalia: mbona watu wakijenga jengo na kulitoa kwa ajili ya Mungu tunasema ni nyumba ya Mungu au ya sala au ya ibada? Mbona watu wakiomba na kumweka mtu wakfu tunasema huyo mtu kachaguliwa na Mungu? Mbona watu wakimbariki mtu, tunasema huyo mtu kabarikiwa na Mungu? Na Yesu alisema: "Mtakalolifungua mbinguni litafunguliwa mbinguni na mtakalo lifunga duniani litafungiwa mbinguni pia", "Ombeni, nanyi mtapewa" etc? Kwa hiyo, kwa kutuumba sisi Mungu amependa kutushirikisha katika kazi yake ya ukombozi na hatushirikishi kama kondoo au mawe bali watu ambao ametupa uwezo wa kuona na kutambua kipi ni chema na kipi si chema katika maisha yetu.
Hata hiyo Biblia unayosema, si imeandikwa na watu? Kwa nini Mungu asingeitunga na kuiangusha ili tuiokote na kuanza kuitumia? Angalia pia namna nyingine: "Hakuna anyempenda Mungu kama hampendi jirani yake" (= kumpenda Mungu ina maana pia kumpenda jirani yako). Kwa hiyo, unapompenda jirani yako unampenda Mungu pia. Unaposhuhudia kitu chema ndani ya jirani yako, unashuhudia kile ambacho Mungu ameweka ndani mwake! Kama Wakatoliki wanaotambua kitu chema ndani ya Nyerere ina maana wanatambua kitu chema ambacho Mungu ameweka ndani mwake na wanataka waumini wao wakione na wajitahidi na wao kutenda mema kama Mkristo mwenzao alivyoweza kufanya. Hii ndiyo maana halisi ya kumtangaza mtu kuwa mtakatifu!