akatubwada
Member
- Feb 7, 2017
- 21
- 26
- VODACOM walifika hapa mwaka 2000 wakiwa hawana mteja hata mmoja na kwa mtaji wao wakapanga kwenye jengo lenye status kuliko majengo yote hapa nchini likiitwa PPF Tower lililoko kwenye kona ya mtaa wa Ohio na Garden.
- Humo PPF Tower walichukua floor si chini ya nne.
- Mwaka 2009 wakaweza kuongeza jengo jingine kule barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na kituo cha mafuta cha Victoria, jengo linaitwa RDK. Hili lilikuwa ni jengo la ziada kwani makao makuu yalibaki palepale PPF Tower.
- Pale Mwanza wakapanga PPF Plaza nalo lina hadhi Mwanza nzima. Hata kule Arusha hawakuchukua eneo au jengo
la kichovu.
MLIMANI CITY MALL imeanzishwa mwaka 2006 mwishoni ikiwa ni supermarket yenye hadhi kubwa si Tanzania tu bali Afrika Mashariki.
Katika majengo manne ya pale MLIMANI CITY PARK, TANZANIA INVESTMENT BANK ndiyo imechukuajengo moja tu (Building 3) lakini mengine yote matatu yaliyobaki (Building 1, 2 and 4) yalichukuliwa na VODA mwaka 2010 mwishoni na wamo humo hadi dakika hii.
- Sasa kuna tetesi kwamba VODACOM wanahama sehemu nzuri kuliko zote yaani MLIMANI CITY wanaendamaeneo ya KINONDONI ingawa sijathibitisha tetesi hizo!
- Ukweli ni kwamba kadiri binadamu unavyobadili “lifestyle” basi na status yako itaonekana. Walipohama PPFTOWER kwenda MLIMANI CITY, hapa status iliongezeka.
- Leo wanahama kutoka MLIMANI CITY kwenda KINONDONI, haya ni maeneo mawili tofauti kabisa kihadhi.
- Mlimani CITY VODA ilikuwa imechukua parking karibu eneo loote lile mnalojua linalotazamana na barabara yaSAM NUJOMA. Kinondoni ni eneo linalojulikana kwa ukosefu wa Parking .
- Bila ubishi hapa hadhi imeshuka,maana yake waendesha magari ndani ya VODA wamepungua, bila kujali ni magari yao au ya kampuni.
Sasa tujadili ilichobadilika ni hadhi ya sasa ya VODA. Wakati VODA inapanga vile tangu PPF TOWER na baadaye wakaenda MLIMANI CITY management walikuwepo wazungu.
- Sasa hivi kwenye management ukiangalia asili ya wahindi imeongezeka na bosi wao mkubwa unaona kama ni mhindi vilevile.
- Ukweli ni kwamba yapo mengi ya kuonyesha kwamba hadhi inashuka, unaweza kuongezea unayoona wewe.
- Na kama hadhi imepanda unaweza kunipinga.