Hadhi na heshima ya Baba wa Taifa iko mashakani

Hadhi na heshima ya Baba wa Taifa iko mashakani

Tuacheni unafiki jamani Nyerere hajashuka hadhi kiasi cha kukashfiwa namna hii. Mapungufu anayo lakini sio wa kufananishwa na watawala wengine waliokuja baada ya wewe interms of good governance and transparency! Hamuoni mmomonyoko wa maadili na ukiukwaji mkubwa wa miiko ya uongozi? Je, kuhusu ufujaji wa kupindukia wa raslimali zetu ni nani anaekemea ktk awamu hizi tatu baada ya JKNyerere? Suala la kero au mizengwe ya muungano halina impact kubwa ambazo zinamuathiri mtanzania moja kwa moja kiasi cha kumdharirisha Nyerere kihivyo ukilinganisha na utajiri mkubwa ambao katuachia. Leo hii watawala wanashirikiana bega kwa bega kuchota mali na kujilibikizia bila kuhojiwa.

Nitakuwa wa mwisho kumtukanisha Mwl Nyerere.
 
Hata mimi naamini ktk hilo lakini tunao watu ambao wangeweza kunusuru hali hiyo mfano mzee Mkapa yupo kimya sana
 
Alichopanda mwanadamu ndicho atakachovuna. Nyerere alizika kabisa demokrasia na uwazi.watanzania kwa zaidi ya miaka 30 walikua wanapiga kura kuchagua kivuli au mtu. Hapakua na mtu aliyeweza kuhoji. Katiba ya nchi ilikua kandamizi na kamwe hakuwaza kuwashirikisha wananchi kutunga katiba nyingine bora zaidi ya kuboresha ile ya mkoloni na sheria zake. Sidhani kwamba nyerere angetawala leo hii pangekua pakungekua hakuna wapinzani kwa sababu eti ni mtawala bora. Wakati wa nyerere wakenya walikua wanatucheka kwmb nyerere anatuswaga kama ngombe kwa sababu watu wengi hawakua na elimu. Mazuri yake yatajwe lakini pia na mabaya yake yakijulikana yawekwe adharani.
 
Alichopanda mwanadamu ndicho atakachovuna. Nyerere alizika kabisa demokrasia na uwazi.watanzania kwa zaidi ya miaka 30 walikua wanapiga kura kuchagua kivuli au mtu. Hapakua na mtu aliyeweza kuhoji. Katiba y
a nchi ilikua kandamizi na kamwe hakuwaza kuwashirikisha wananchi kutunga katiba nyingine
bora zaidi ya kuboresha ile ya mkoloni na sheria zake.
Sidhani kwamba nyerere angetawala leo hii pangekua
pakungekua hakuna wapinzani kwa sababu eti ni
mtawala bora. Wakati wa nyerere wakenya walikua
wanatucheka kwmb nyerere anatuswaga kama
ngombe kwa sababu watu wengi hawakua na elimu.
Mazuri yake yatajwe lakini pia na mabaya yake
yakijulikana yawekwe adharani.

Alitawala kwa mujibu Wa katiba ya wakati huo. Ukisikiliza hotuba zake kuna moja anasema katiba iliyopo inaniruhusu hata kuwa dikteta. Unaweza kuona uwazi Wa Mwalimu.
 
Nyerere aliamua kuacha Kazi yenye Heshima na Kupigania Uhuru wa Watanganyika.Hilo liliwashinda Wazee Wengi kabla yake hasa kutokana na Mapigo ya Wakoloni.Jiulize,Ni nani kati ya hawa Viongozi wa Leo wanaowaogopa Wawekezaji Wazungu wangeweza kumtimua Mkoloni?.Ukijipa Muda kidogo wa Kutafakari kwa Utulivu ndio utagundua Nyerere alikuwa Kiongozi wa aina yake.

No one is perfect!
 
Kama jambo la muungano pekee ndio lilimletea hadhi na heshima Nyerere, basi huenda ikapitia msukosuko. Jaribu kupitia upya umaarufu wake ulpatikanaje au ulisababishwa na nini?
 
Kama jambo la muungano pekee ndio lilimletea hadhi na heshima Nyerere, basi huenda ikapitia msukosuko. Jaribu kupitia upya umaarufu wake ulpatikanaje au ulisababishwa na nini?

Hotuba ya Lissu umeisonma?!

Yaliyomo kwenye hiyo hotuba ni madogo?
 
Kama jambo la muungano pekee ndio lilimletea hadhi na heshima Nyerere, basi huenda ikapitia msukosuko. Jaribu kupitia upya umaarufu wake ulpatikanaje au ulisababishwa na nini?

Hotuba ya Lissu umeisonma?!

Yaliyomo kwenye hiyo hotuba ni madogo?
 
Hotuba ya Lissu umeisonma?!

Yaliyomo kwenye hiyo hotuba ni madogo?

Hotuba nimeisoma, na simtetei Nyerere kwa matendo yake. Nimeangalia kichwa cha huu uzi kuhusu heshima ya baba wa taifa kushuka au kuwa matatani. Nikakwambia kama suala la muungano ndio suala pekee lililomletea heshima hiyo, basi itakuwa matatani.

Heshima yake imejengwa na vitu vingi sana, kwa hiyo kuishusha au kuiweka matatani nako ni lazima upime mambo mengi sana kwa kina.
 
Hata siku moja. Usidhani heshima yake Baba wa Taifa itakaa ishuke. Watakaopoteza hadi na heshima ni hawa wa leo wanaopinga kuwa mchana upo. Kwao kwa sababu wanakaa mle mjengoni mchana kutwa huku taa zimewashwa wanaona ni usiku tuu. Wao wanasema ka si usiku, mbona taa zimewashwa? Pole zao.
Nyerere angekuwa hai leo hii, angewacheka kweli kweli. Lazima wakubali MABADILIKO. Muungano huu sio msahafu, unaweza badilika wakati wowote. Tupitishe memorandam, tuulize kuwa tunautaka muungano wa aina gani? Serekali 2, 3, 1?? Muungano wa sasa hivi ni muungano wa kuibembeleza Zanziba. Kuwapa kila kitu wanacho lilia. Leo, wakisema hawanywi maji ya kwao na wanataka maji kutoka Oman, hakuna atakaye bisha bali ni madege yatakodishwa kwenda kuwanunulia.
Kila walichodai, wamepewa, mpaka katiba ya JMT wameipewa ili waisigine watakavyo. Katiba waliyo apa kuilinda, unataka nini tena???
 
tanganyika iko wapi?
 
Hotuba nimeisoma, na simtetei Nyerere kwa matendo yake. Nimeangalia kichwa cha huu uzi kuhusu heshima ya baba wa taifa kushuka au kuwa matatani. Nikakwambia kama suala la muungano ndio suala pekee lililomletea heshima hiyo, basi itakuwa matatani.

Heshima yake imejengwa na vitu vingi sana, kwa hiyo kuishusha au kuiweka matatani nako ni lazima upime mambo mengi sana kwa kina.

Kumbuka kwa binadamu unaweza fanya mazuri mengi ila baya moja tu likafunika mazuri yote na hii ndio itakuwa hatima ya Nyerere.
 
Tuacheni unafiki jamani Nyerere hajashuka hadhi kiasi cha kukashfiwa namna hii. Mapungufu anayo lakini sio wa kufananishwa na watawala wengine waliokuja baada ya wewe interms of good governance and transparency! Hamuoni mmomonyoko wa maadili na ukiukwaji mkubwa wa miiko ya uongozi? Je,
Nitakuwa wa mwisho kumtukanisha Mwl Nyerere.

Duh! Transparance Enzi za Nyerere ? Umezaliwa Mwaka Gani ?
 
Hata mimi naamini ktk hilo lakini tunao watu ambao wangeweza kunusuru hali hiyo mfano mzee Mkapa yupo kimya sana

Sio Mkapa ni ccm na Jk ndio wanapaswa kushauriwa wakubali rasmu ya serikali 3 .yaishe tuanze upya .vinginevyo lawama juu ya kudhalilishwa kwa Baba wa Taifa iko juu yao .ccm na Jk
 
Ukifuatilia kwa makini kuhusu hili swala la muungano,utagundua kuwa limegubikwa na utata na inawezekana kabisa moja ya waasisi wa muungano huu(mwalimu Nyerere) alicheza "foul" na imekuwa ni siri ya mika nenda miaka rudi ila sasa wakati umefika hii siri lazima ijulikane tofauti na hapo ni kuvunja muungano.

Hapa sasa naanza kupata jibu ni kwanini siku zote mwalimu alikuwa mkali pale watu walipokuwa wakihoji uhalali wa muungano na muundo wake.Bila shaka alitambua kuna mengi yangefichuka ila sasa wakati umefika yaliyokuwa yakifichwa yatafichuka na hapa ndio naposema hata hadhi na heshima ya mwalimu katika hili taifa itakapochafuka.

Mbali na mapungufu ya juu ya uhalali wa huu muungano kama vile hati ya muungano n.k,kitendo cha siri za muungano kuwa hadharani ni doa kubwa kwa Baba wa taifa kwani siri hizo zitathibitisha kama muungano huu ni "haramu" au laa.

Time will tell.

No, si kwamba hadhi yake itachafuka. Yeye ni mtu tu kama alivyo mtu mwingine yeyote ambaye hukosea na hutenda vyema pia. Better enough ni kwamba Mwl Nyerere mwenyewe alishakiri several times kuwa hawakuwa miungu!!

Nionavyo mimi ni kuwa tuwe tayari kurekebisha pale alipokosea kwa sisi wenyewe kustahiana na kuheshimiana.Na kwa kufanya hivi tunakuwa tunatunza heshima ya mtu huyu ndani na nje ya taifa letu ambaye kiukweli pamoja na kuwa ana makosa kama binadamu yeyote lakini bado ni mwasisi wa Taifa hili la Tanganyika anastahili kuheshimiwa.

Lakini hofu yangu ni hawa wenzetu CCM kwani misimamo yao ya ajabu ndiyo itakayoharibu heshima ya mtu huyu huko alikolala. Hawataki kukubali kuwa kuna makosa yalifanyika na hivyo tuutumie mwanya huu wa kutunga katiba mpya kurekebisha makosa ya Nyerere.

Katika hatua hii iliyofikiwa,Nyerere na Karume na Muungano wao huu wa ajabu ajabu watachimbwa sana mpaka mwisho wa ukweli wa mambo ujulikane hata kama katiba hii haitapatikana pale Dodoma!!
 
Back
Top Bottom