HabariLeo: Zitto hakamatiki urais 2015

HabariLeo: Zitto hakamatiki urais 2015

Mpinzani wako akikuunga mkono na kukusifia tena kupiga chapuo ili wewe upitishwe jua wewe ni dhaifu anauhakika wa kukubwaga ulingoni.APIME MWENYEWE ACHUKUE HATUA.
 
Habari zinazoongoza gazeti
la habari leo ni kwamba zitto ndie mtanzania anayepewa nafasi kubwa
zaidi kushinda urais 2015
Hili gazeti la wana ccm nimeshangaa kuandika habari hii ila nadhani
wamepania kumpa kichwa ili ahame chadema agawe chama. Sidhani kama zitto
anampita dr slaa hata kumkaribia

wana Jf tunasikitisha hatuhoji siku hizi, tunachofanya ni kutetea au kulaumu kwa kuzingatia mrengo wetu wa siasa, hii habari haikuandikwa na Haba
 
Ben Mkapa wakati fulani aliwahi kuzungumzia suala la uaminifu kwa watanzania...maelezo yalikuwa yanaelekea kufanana na haya" Hata kama ni ndugu yako...ikitokea akakuibia ukamkamata hata akitubu namna gani na kusema haibi tena kile kiwango cha kumuamini hapo kabla ya wizi...hakiwezi kurejea...". Na kwambieni vivo hivyo kitendo cha kutuhumiwa ni msaliti ndani ya Chama na yawezekana kabisa anawafadhili akina "MASALIA" ni vigumu sana kurejesha imani ya watanzania waliokuwa wanamuona na kudhani kuwa "Zito" ni kiongozi shupavu wa kuaminiwa na kukabidhiwa madaraka makubwa katika nchi hii.

Lazima afanye kazi ya ziada. Bahati mbaya sana "Zito" hawezi kutumia mbinu ya Ben Saa8 (kutubu) kurejesha imani ya watanzania kwake.
 
Habari zinazoongoza gazeti la habari leo ni kwamba Zitto ndie mtanzania anayepewa nafasi kubwa zaidi kushinda urais 2015
Hili gazeti la wana CCM nimeshangaa kuandika habari hii ila nadhani wamepania kumpa kichwa ili ahame CHADEMA agawe chama. Sidhani kama Zitto anampita Dr Slaa hata kumkaribia



Hasimkaribie kwa kipi? na si kumkaribia anampita kabisa Zitto anakubalika sana na kichwa wewe kama unamtaka Slaa n wewe ZItto hakuna kama yeye ndani ya Chadema, huna ushahidi wa kuonesha CCM wanampa kichwa ila ni fikra zako na dhana zako zisizo na maana
 
Hakamatiki,zito for ccm 2015

mbona ccm mnampenda sana zito kuna nini?????????????????????
 
Zitto ametumwa kukivuruga chadema ana ajenda ya siri yle.
 
Naamini zito yuko nyuma ya hii habari 100%....zito anawashwa washwa sana na uraisi and am sure he will never be a president of any country in this galaxy...............bet me ka unabisha
 
Labda mmesoma vibaya .. URAIS AU URAHISI...
 
Habari zinazoongoza gazeti la habari leo ni kwamba Zitto ndie mtanzania anayepewa nafasi kubwa zaidi kushinda urais 2015
Hili gazeti la wana CCM nimeshangaa kuandika habari hii ila nadhani wamepania kumpa kichwa ili ahame CHADEMA agawe chama. Sidhani kama Zitto anampita Dr Slaa hata kumkaribia

Bila ushabiki Zitto anamzidi Dr Slaa kwa mbali. Ikumbukwe kuwa wapiga kura wengi wa 2015 ni vijana , hivyo Zitto ni kijana. Kwa hila zilizotengenezwa kwa makusudi Dr Slaa na Chadema kama Chama wana tofauti kubwa na upande mmoja wa jamii ya watanzania; lakini Zitto ana weza kuondoa dhana hizo potofu na kupenetrate ndani kabsa ya jamii hiyo. Wote wawili ni wasomi waliobobea.

Ilihali Dr Slaa hakaubaliki miongoni mwa idadi kubwa ya waislamu, Zitoo kwa kuwa msomi anakubalika miongoni mw aidadi kubwa ya wakristo. In short Dr Slaa alikuwa very deadly 2010, lakini ni spent force for 2015. Ni lazima twenda na wakati na wahusika wenyewe wakubali kwenda na wakati.
 
Hakamatiki amekuwa kambale?? kama hamna cha kuandika wauzie wauza vitumbua hizo karatasi wafunge nazo
 
Back
Top Bottom