Ngisibara
JF-Expert Member
- Jan 2, 2009
- 3,413
- 2,276
Nimekuwa nashangaa kila mara ninapotaka kupata taarifa mbali mbali kupitia mitandao ya wizara au idara za serikali yetu basi hukutana na habari zilizopitwa na wakati na ajabu hakuna hata mtu mmoja kutoka kwenye sehemu husika ambaye anabeba usumbufu wa kumkumbusha mtu wa IT kufanya mabadiliko katika mbao zao wanazotumia kuhabarisha, MFANO: leo nikijaribu kuangalia distance ya kutoka Dar hadi Manyara ndani ya mtandao wa Tanroads ndipo nilipokutana na chart ya mwaka 2012 na haina Mkoa wa Manyara, pia nikaangalia project zao nikakuta Mfugale flyover ya Tazara ni Ongoing wakati ilishafunguliwa na Rais? nilipoendelea kuchungulia chungulia nikakuta kasoro hizo za kushindwa kurekebisha dosari hizo ni nyingi tu na nikaamua niwaandikie email kwa account waliyoweka wao wenyewe , cha ajabu unatakiwa uweke "verification code" kabla ya ku submit lakini nayo haipo hivyo nikashindwa kuwa na mawasiliano nao...watanzania inabidi tubadilike kwani hii Business as usual inatupeleka pabaya tukilinganishwa na wenzetu ambao wako serious huko duniani