samaki2011
JF-Expert Member
- Dec 17, 2013
- 1,775
- 469
Wanajamvi habari za jioni. Kwa wale mliokuwa mkiangalia taarifa ya habari ya saa 2 usiku, mtakumbuka kuna habari moja ya kusikitisha ya mtoto mmoja mwenye kichwa kikubwa kuliko kawaida (Jina lake ni Baraka na mama yake anaitwa Fatuma Chaduku), mama wa mtoto huyo ameomba msaada kwa watz ili wamchangie pesa kwa ajili ya upasuaji wa kichwa kwani uzito wa kichwa ni mkubwa kiasi cha kumwelemea mtoto kiasi cha kushindwa kukaa au kusimama.
Nafahamu sana kwamba jukwaa hili ni la siasa ila nimeamua kupost thread hii ktk jukwaa la siasa kwani viongozi wetu wengi wa kisiasa hujinadi na kuomba kura kwa wananchi huku wakijidai kuwapenda na kujali matatizo ya watu na ahadi lukuki na zisizotekelezeka. Wanasiasa wenzangu naomba tuwe mstari wa mbele kujitokeza na kumsaidia mtoto huyo. Toa mchango wako kupitia TBC1 Naenda mbali zaidi.......
Wiki chache zilizopita tuliwaona viongozi wa kisiasa wakipita huku na huko wakila ubwabwa na wabibi kule vijijin dk chache kabla ya uchaguzii, wengine wameonekana wakishiriki shughuli za kilimo mashambani kama ishara ya upendo kwa watz kwamba vyama vyetu vinawajali wananchi huku tukijisahau kufuatilia kwa karibu huduma za afya mahospitalini na kuwabana wezi wa dawa.
Hatutaki unafiki na hapa naanza kwa kupanga safu ya uchangiaji. CCM mtakuwa wa kwanza kumchangia huyu dogo kwa sababu zifuatazo:
1. Nyie ndio mmeshika dola hivo mnpaswa kuonyesha mfano
2. Tumewapa dola miaka 53 hadi sasa huduma za upasuaji si zakuaminika hosp za serikali na mmetoa rufaa ya kwenda INDIA
3. Mnatumia nguvu nyingi kulaghai wananchi na kupoteza pesa nyingi kuhonga wapiga kura huku wananchi wakikosa matibabu
4. Vikao vingi na safari nyingi zisizo na tija pesa ambazo zingejenga hospitali za kimataifa nchini
5. Duuuu wadau ongezeeni nisiwanyime haki ya kuchangia CHADEMA mtafuata baada ya magamba kwa sababu zifuatazo:
1. Ninyi ni chama cha ukombozi nchini kwani mmemkomboa mwananchi kifikra kwani isingekuwa ninyi tusingejua kwamba tunaibiwa na kuhujumiwa uhuru na utu wetu
2. Ni chama kinachopendwa na wote Tanzania
3. Hampendi watz wateseke ktk nchi yao wenyewe
4. Mna nia ya dhati ya kumwondoa mkoloni mweusi
5. Ninyi ni nguvu ya umma
5. Hamna unafiki wala ulaghai kama wale wanaosema ni wasikivu huku wakiuma na kupuliza kama panya Tunategemea pia kupokea michango kutoka vyama vingine vya upinzani. Source ya taarifa hii ni TBC, imeletwa hapa jamvini na kuongezewa nyama na mimi mzalendo wa nchi yangu-samaki2011