Habari wana jf


Santos06

Santos06

Member
Joined
Mar 11, 2019
Messages
67
Points
125
Santos06

Santos06

Member
Joined Mar 11, 2019
67 125
Profesa wa Uchumi wa Chuo Kikuu kimoja alizungumza darasani kwamba hakuwahi kufelisha mwanafunzi hata mmoja, hata hivyo wakati huu Darasa zima lilikua limefeli.
Darasa lilikua limejibu mtihani kuwa Ujamaa ni itikadi muafaka ya kichumu ya kuleta usawa, chini ya ujamaa hakuna tajiri wala masikini.

Profesa akataka darasa lizijaribu kanuni za kijamaa kwenye mtihani.
Kwamba alama watakazopata wanadarasa wote zitagawiwa kwa usawa baina yao; hakuna atakaefeli wala hakuna atakae pata alama 'A'.

Baada ya mtihani kila mwanafunzi alipata alama 'B'.
Waliojiandaa sana na mtihani walichukia, wakati ambao walijiandaa kiasi tu walifurahi.
Mtihani wa pili ulipokuja wale waliojiandaa kidogo wakajiandaa kidogo zaidi na wale ambao awali walijiandaa sana, wakati huu hawakujiandaa vilivyo kwani nao hawakutaka kujisumbua.

Matokeo ya wastani yakawa alama 'D'. Na hakuna aliyefurahia!

Ulipokuja mtihani wa 3 matokeo yakawa 'F'

Jaribio lilivyoendelea na matokeo yakawa mabaya zaidi, wanafunzi wakalaumina na kuitana majina mabaya. Hakuna aliekua tayari kusoma kwa faida ya mwingine.

Kwa Mshangao mkubwa wote wakafeli, na profesa akawaambia hatimaye Ujamaa pia utafeli kwakua pale malipo yanapokua makubwa na jitihada za kufanikiwa zinaongezeka. Lakini pale ambapo Serikali inafuta malipo yote hakuna atakae jaribu kufanikiwa.

Pengine hizi ndio sentensi 5 zinazotawala jaribio hili.

1. Huwezi wafikisha masikini kwenye mafanikio kwa kuwaondoa matajiri kwenye mafanikio.

2. Kile ambacho mtu analipwa bila kukifanyia kazi, kuna mtu amekifanyia kazi bila kulipwa.

3. Serikali haiwezi kumlipa mtu kitu, ambacho serikali hiyo haijampora kitu hicho mtu mwingine.

4. Huwezi uzidisha utajiri kwa kuugawanya.

5. Pale ambapo nusu ya watu wanaona hakuna haja ya kufanya kazi kwakua kuna nusu ya watu wanafanya kazi kwa ajili yao. Na pale wanaofanya kazi wakiona kwamba hawana sababu ya kufanya kazi kwakua watu wengine watafaidika na kazi zao; huo ndio unakua mwanzo wa mwisho wa Taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
D

Deceiver

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2018
Messages
448
Points
1,000
D

Deceiver

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2018
448 1,000
Wewe sio mbunifu kabisa.
Kwa uvivu huu unategemea ingekua novel ungeuza?
Kwa staili hii hata puchi huuzi.
 
K

kikokotoo kipya

Senior Member
Joined
Dec 18, 2018
Messages
169
Points
250
K

kikokotoo kipya

Senior Member
Joined Dec 18, 2018
169 250
Uzi mzuri sana nimeupenda,Lakini kama wengine wanavyokushauri badilisha kichwa cha habari,wengi wataupita huu uzi kwasababu ya kichwa chake cha habari.wanaweza dhani kuna ujinga ndani yake kumbe umeandika vitu vya maana sana,na mfano wa maana sana.Acha kubishana na wanao kushauri BADILI KICHWA CHA HABARI.Watu umewatoa kwenye kuchangia uzi badala yake wote wameishia kukosoa heading yako.
 
James Comey

James Comey

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2017
Messages
4,530
Points
2,000
James Comey

James Comey

JF-Expert Member
Joined May 14, 2017
4,530 2,000
Kuna kitabu kinaitwa miongozo miwili: Kupaa na Kuanguka kwa Azimio la Arusha by Issa Shivji.
Kitafute ukisome.

Pia tafuta machapisho ya mwal. Nyerere. Yeye alitaka mfumo wa ujamaa uliboreshwa kukidhi hali ya kisiasa na uchumi kwa Tanzania. Mfumo ule ungekufa baadaye lakini kama tungekaa nao kwa kipindi hata cha miaka 40 huku ukibadilika taratibutaratibu ungetusaidia sana.

Shivji mpaka leo anahisi ule mfumo ungedumu nafkiri ndiyo tofauti yake kubwa na wanazuoni wengine
 

Forum statistics

Threads 1,285,012
Members 494,369
Posts 30,847,295
Top