Habari njema kwa wote

Mar 12, 2016
73
33
Mwimbaji chipukizi wa muziki wa injili nchini, Jimmy Gospian, amechaguliwa kuwania tuzo za ZABURI AWARDS 2016/17.

"Ndugu mtanzania, naomba unipigie kura kwenye tuzo za injili za ZABURI AWARDS 2016/17 kipengere cha MWIMBAJI BORA WA KIUME ANAYECHIPUKIA. Ili kunipigia kura, andika ujumbe wa maneno MWIMBAJI BORA WA KIUME ANAYECHIPUKIA JIMMY GOSPIAN kisha tuma kwenda namba 0714 92 15 89". Gospian mwenye makazi yake Jijini Mwanza ameiambia BMG.

Kwa sasa Jimmy Gospian aliyeachana na muziki wa kidunia, anatamba na wimbo wake uitwao Nakujua Bwana ambao umemtambulisha vema kwenye muziki wa injili ndani na nje ya nchi.

Kumbuka unapaswa kupiga kura moja tu na mwisho wa zoezi hilo ni April 12,2017 ambapo tuzo za Zaburi Awards 2016/17 zilizoandaliwa na kampuni ya Famara Entertainment ya Jijini Mwanza, zitatolewa April 17,2017 Jijini humo.
 
Back
Top Bottom