Habari Njema Kwa Wanawake.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Habari Njema Kwa Wanawake....

Discussion in 'JF Doctor' started by Dr. Chapa Kiuno, Oct 9, 2009.

 1. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  </SPAN>


  Maumivu ya tumbo wanayopata wanawake wakati wa kipindi cha hedhi wamepatiwa dawa
  Friday, October 09, 2009 8:07 AM
  Habari njema kwa wanawake, wanasayansi nchini Uingereza wamegundua dawa ya vidonge ambayo inazuia maumivu ya tumbo wanayopata wanawake wanapokuwa kwenye hedhi.


  Kipindi cha hedhi huwa ni kigumu sana kwa wanawake wengi duniani kutokana na maumivu makali ya tumbo wanayopata wakati wanapokuwa kwenye siku zao.

  Wanasayansi nchini Uingereza wamegundua dawa za vidonge ambazo zitazuia maumivu hayo na hivyo kuwafanya wanawake waendelee na maisha yao ya kawaida bila maumivu yoyote.

  "Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi yanayojulikana kitaalamu kama Dysmenorrhoea huwaathiri wanawake wengi duniani na hadi sasa kulikuwa hakuna tiba au njia ya kuyaondoa maumivu hayo", alisema Dr Jim Phillips toka kampuni ya Vantia Therapeutics iliyoko mji wa Southampton ambayo ndiyo iliyogundua dawa hiyo.

  "Tunaweza kusema kuwa huu ni ugunduzi mpya wa kwanza kwani hakuna tiba nyingine yoyote zaidi ya hii", alisema.

  Dawa hizo za vidonge zilizopewa jina la VA111913, zimefanyiwa majaribio na zimeonyesha mafanikio makubwa sana na zimethibitishwa kuwa ni salama.

  Dawa hizo zitaingia madukani baada ya miaka minne.

  Zitafanyiwa majaribio tena na wanawake 128 wa nchini Uingereza na Marekani wenye umri kati ya miaka 18 na 35.

  Wanawake watakaojitolea kujaribu dawa hizo ni wale wanaosumbuliwa na maumivu makali sana ya tumbo kutokana na hedhi kiasi cha kwamba hushindwa kuendelea na maisha yao ya kawaida. Wanawake hao watapewa dozi ya dawa hizo wakati wa kipindi cha hedhi zao.

  Dawa hiyo hufanya kazi kwa kuifanya homoni ya vasopressin, ambayo huifanya misuli ya ukuta wa uterus kusinyaa wakati wa hedhi iwe katika hali yake ya kawaida na hivyo kumuepusha mwanamke na maumivu hayo.

  Takwimu zinaonyesha kwamba maumivu ya tumbo wakati wa hedhi huwaathiri asilimia 80 ya wanawake duniani katika baadhi ya vipindi vya maisha yao.

  Wanawake wengi hujaribu kupunguza maumivu hayo kwa kufanya mazoezi ya kulainisha misuli ya tumbo, wengine hujikanda tumbo wakati wengine hushindwa kuvimilia maumivu hayo na hutumia dawa za kupunguza maumivu kama vile paracetamol, aspirin na nyinginezo.  Source: Daily Mail
   
 2. E

  EMMANUEL SHOMBE Member

  #2
  Oct 9, 2009
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jina la dawa hiyo sijalielewa kabisaaaa. usije ukawa tapeli....
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Dawa gani hii tena...mbona mimi mywife wangu akimeza Paracetamol 2tu, basi kila kitu kwisha...We ni agent wa hiyo kampuni nini boss!
   
 4. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Ha ha ha! Hiyo ya Paracetamol kali mkuu.
   
 5. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,364
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Dr Chapa mi naona ulichoandika hapo sio jina la hiyo dawa huenda ukawa umekosea ukaandika serial numbers za hiyo package!!
   
 6. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Mkuu tena hiyo paracetamol mama anaweza kunywa kabla mambo hayajaanza 'counter attack'. Option nyingine ni vidonge vya njia ya uzazi wa mpango kwa muda.
   
 7. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  hivi wewe unalijua tumbo la pediod unalisikia?
  haliponi kwa paracetamol, diclopar, wala diclofenac, likitulia ni dk 2 tu linaanza tena
   
 8. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ha ha ha!
   
Loading...