Habari njema kwa wafugaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Habari njema kwa wafugaji

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Tutor B, Jul 6, 2018.

 1. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2018
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,728
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Natumaini haujambo wewe unayesoma hii mada.

  Leo napenda kuwaleteeni habari njema ya kuwasaidia wafugaji wa kuku, bata, nguruwe, sungura, ng'ombe nk. Habari yenyewe ni kuhusiana na uwezekano wa kuzalisha chakula bora cha mifugo kwa bei rahisi sana.

  Chakula hicho kinafahamika kama Hydroponics Fodder; ni chakula halisi kinachozalishwa kutokana na mbegu za shayili, ngano, mahindi, serena n.k. Chakula hiki kinazalishwa kwa kutumia trei na virutubisho bila kutumia udongo.

  Iwapo utapenda kujifunza namna ya kuzalisha chakula hicho - tumekuandalia kitabu chenye maelekezo ya hatua kwa hatua. Unaweza kujipatia kitabu hicho kikiwa soft coy au hard copy kwa kuwasiliana nasi kwa nambari 0655-533543; e-mail: jnb14enterprises@gmail.com.

  Uliza chochote kuhusiana na Hydroponics Fodder utajibiwa.

  KARIBU.

  Updates
  Wakati nafuatilia tafiti mbalimbali nimesoma sehemu imethibitika kuwa ... Kati ya watanzania 10 (watu wazima); 8 hawana elimu zaidi ya Elimu ya msingi"
  Utafiti huu ulifanyika mwaka 2017 na Finscope Tanzania. Hapa jambo la kujiuliza ... machapisho mengi ya kusaidia watu kujifunza yameandikwa kwa lugha ya kiingereza ... video nyingi za youtube kama aliyoweka jamaa yangu kuonesha namna ya kuotesha fodder ni ya kiingereza ... ina maana teknolojia inayotolewa kwa lugha ya kiingereza inawafikia watu wachache sana.

  Kwa kulitambua hilo ndiyo maana tumeanza kuwashirikisha wadau mbali mbali ili tuuweze kupata machapisho ya kunoa bongo za watanzania yaliyoandaliwa kwa lugha ya kiswahili.
   
 2. Mazigazi

  Mazigazi JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2018
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 4,291
  Likes Received: 2,498
  Trophy Points: 280
  Ngoja nikagugo
   
 3. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2018
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,603
  Likes Received: 532
  Trophy Points: 280
  Tiririka kwa uchache, yaani summary ya utayarishaji ya hivyo vyakula
   
 4. Agenda1

  Agenda1 JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2018
  Joined: Aug 11, 2017
  Messages: 564
  Likes Received: 523
  Trophy Points: 180
  Tangazo la biashara
   
 5. Shunie

  Shunie JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2018
  Joined: Aug 14, 2016
  Messages: 86,403
  Likes Received: 247,258
  Trophy Points: 280
  Mh
   
 6. Abu_yazid

  Abu_yazid JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2018
  Joined: Mar 28, 2014
  Messages: 1,432
  Likes Received: 1,099
  Trophy Points: 280
  Kama yalivyo mengine
   
 7. uporo wa wali ndondo

  uporo wa wali ndondo JF-Expert Member

  #7
  Jul 6, 2018
  Joined: Dec 3, 2013
  Messages: 2,346
  Likes Received: 1,261
  Trophy Points: 280
  Umelipia tangazo?....kwa tanzania ukiona mtu anakuita kwenye fulsa juwa wewe ndiye fulsa yenyewe, ni tanzania peke yake utaona mtunzi wa kitabu cha ufugaji wa kuku au samaki lakini kwake hana mfugo ata yule paka wa kuzugia hakuna.au njoo uwe milionea kwa mtaji mdogo wa elfu 10 lakini muuzaji mwenyewe kiatu soli imeisha upande mmoja kwa sababu ya kupiga misele ovyo mitaani kutafuta wanunuzi wa vitabu.
   
 8. alphonce.NET

  alphonce.NET JF-Expert Member

  #8
  Jul 6, 2018
  Joined: Jul 19, 2013
  Messages: 661
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 60
  Sharing is caring, hii hapa YouTube video inafundisha Bure step by step kutengeneza hydroponics fodder bila kununua kitabu

   
 9. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #9
  Jul 7, 2018
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,728
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Sisi hatufanyi theory ... tunafundisha kwa vitendo.
   
 10. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2018
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,728
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  SAFI SANA ... INAPENDEZA .. ILA KUMBUKA WATANZANIA WENGI HAWANA ACCESS NA MITANDAO NDO MAANA TUMEJIDHATITI KWENYE NJIA AMBAYO TUNAAMINI KILA MTU ANAWEZA KUPATA MAARIFA HAYO.
   
 11. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2018
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,728
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Huo ni mtazamo wako ... awazalo asiyejua halipaswi kusumbua anayejua ...
  Wenye kuhitaji teknolojia hiyo wanaendelea kuja kituoni na kujifunza ... wewe endelea kukariri.
  Jambo la pili .. hii ni taasisi hivyo hakuna mtu anayetembea kusambaza kitabu .. wahitaji wanaagiza au wanakuja kituoni kwetu kwa ajili ya kuhudumiwa.
  Ni imani yangu kubwa kuwa ukifunguka macho ya rohoni utapata utambuzi.
   
 12. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #12
  Jul 7, 2018
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,728
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Sisi hatufanyi biashara, tunatoa huduma kwa jamii. Ila kumbuka kwenye huduma kuna kazi zinafanyika ambapo muhitaji huduma lazima achangie.
   
 13. mangi Lemule

  mangi Lemule JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2018
  Joined: Mar 7, 2017
  Messages: 380
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 60

  Umenena Mkuu, nlkutana na mtu kuchoka anahvo vtabu vya sampuli ya hicho cha mleta mada na vtabu vya watoto vya kujifunza kuandika.


  Swali kwanini hawasomagi hivo vitabu wao? Wakayafanyia kazi?
   
 14. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #14
  Jul 13, 2018
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,728
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Anayekuandikia haya ndo anatumikia NGO inayofanya kazi Tanzania bara nzima, anasoma vitabu sana na anavifanyia kazi. Tembelea www.mwasenda.org ukutane na timu nzima ya watenda kazi. Kwa taarifa yako ni kwamba ... kwenye NGO hii tupo watu wenye taaluma zetu; wengine ni watumishi wa serikali, wengine wanafundisha vyuo vikuu ... na uzuri ni kwamba wanaofundisha vyuo vikuu sio wabongo ... wanashangaa namna wabongo walivyo na fursa nyingi lakini hawazitumii.
   
 15. mangi Lemule

  mangi Lemule JF-Expert Member

  #15
  Jul 13, 2018
  Joined: Mar 7, 2017
  Messages: 380
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 60

  Mnauwezo mkubwa sana wa kushawishi watu vitu ambavyo hamjawahi kuvifanya. Hongeren kwa hilo.

  Nyie ndo watu mnaofundisha Ujasiriamali na hata hamjawahi kuuza pipi.
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Jul 14, 2018
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,881
  Likes Received: 4,422
  Trophy Points: 280
  Ninalisha mifugo yangu chakula cha kutengenezwa namna hii mwaka wa pili sasa.
   
 17. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #17
  Jul 14, 2018
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,728
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Hunifahamu ndo maana unaifananisha na hao...

  Alokwishaumwa nyoka akiona mjusi lazima ashtuke ...

  Bin adam akidanganyika sana mwishowe akili yake hupata kilema cha maisha ...

  Watanzania walio wengi wamepata vilema vya maisha ...

  Je na wewe ni mmoja wao?
   
 18. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #18
  Jul 14, 2018
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,728
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Hongera sana! hachana na wadanganyika waendelee kutonoa vichwa vyao!
   
 19. mangi Lemule

  mangi Lemule JF-Expert Member

  #19
  Jul 14, 2018
  Joined: Mar 7, 2017
  Messages: 380
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 60
  Hunifahamu ndo maana unaifananisha na hao..." Ni kweli sikufahamu ila wengi wa waandishi wa vitabu vya motivation wa Tanzania ni hovyo.

  Alokwishaumwa nyoka akiona mjusi lazima ashtuke ..." Mda mwingne si kweli Mkuu.

  Bin adam akidanganyika sana mwishowe akili yake hupata kilema cha maisha ... "" Umenena vema sana Mkuu.

  Watanzania walio wengi wamepata vilema vya maisha ..., "" mm sio Mtanzania

  Je na wewe ni mmoja wao?,,"" Hapana
   
 20. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #20
  Jul 15, 2018 at 11:48 AM
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,728
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Ok, ingia kwenye website ya shirika langu ... napaswa kuwahudumia watanzania .. kama wewe sio .. nisamehe bure.

  Sisi tunafanyia kazi tafiti zilizofanywa na wataalamu mbalimbali.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...