Habari njema kwa Vibonge!

Habari njema kwa Vibonge!

Maty

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2010
Posts
2,167
Reaction score
727
Habari senyu kwa mpigo.

Kwa wale wenzangu na mimi vibonge suluhisho hili hapa. Hapa kati niliongezeka uzito kwa kiwango kikubwa sana, kasheshe ikawa ni jinsi gani nitapungua kufanya mazoezi kidogo ni mvivu na pia hata muda wa kufanya mazoezi sina. Nimekunywa juice ya ukwaju wapi? maji moto na limao wapiiiiiiiiiiiiiiiii dah kidogo nikate tamaa nikasema labda uzee huu unaonijia inawezekana ndio imetoka hiyo kwa nini kila ninachojaribu kinashindikana

Atafutae hachoki katika kuperuzi peruzi nikakutana na hii soup ya kupunguza mafuta mwilini nikasema ngoja niijaribu ni ngumu kidogo mwanzoni, wiki ya kwanza nikajaribu nikashindwa nikapiga moyo konde wiki inayofuata nikajitahidi mpaka nikamaliza.

Wapendwa nimepungua kilo tano na nusu ndani ya wiki moja mpaka naandika hapa hata siamini kwa kweli ila ndio hivyo imetokea. Nikaona bora nishee na nyinyi maana hili janga la unene ni janga la kitaifa hasa kina mama wanaotoka kujifungua. Jaribu na wewe mimi imenitendea muujiza asee


Soup yenyewe hii

SOUP YA KUPUNGUZA MAFUTA MWILINI

Mahitaji:
Vitunguu vikubwa 6, Pilipili hoho 2, Nyanya 4 kubwa, Cabbage 1 kubwa, Leeks kubwa 4, Cube 2 za Knorr au Roiko (kwa ladha na si lazima). Hii inaweza kutosha kwa nusu siku mpaka siku nzima kutegemea uwezo wako wa kuila.
Boresha ladha kwa kuongeza chumvi, pilipili kawaida au manga, hot sauce au malimao/ndimu.

Namna ya kutengeneza:
Katakata mboga viwe vipande vidogodogo. Weka maji yajae kufunika mboga. Chemsha haraka kwa muda wa dakika kumi halafu punguza moto zitokote taratibu mpaka zilainike kabisa.
Baada ya hapo saga kwenye blender au utakavyoweza ili upate supu yenye rojorojo.
Kula hii supu kwa kadiri uwezavyo kwa kuwa haita ongeza calories kwenye mwili. Jinsi utakavyo kula hii supu ndivyo utakavyo pungua uzito.
Ni vema kuweka supu kwenye thermos asubuhi kama hautakuwepo nyumbani ili uendelee kula mahali popote utakapo kuwa.

TAFADHALI KUMBUKA: Mahali popote panapoandikwa supu, ni hii Basic Fat Burning soup hapo juu na siyo supu nyingine.
UKILA HII SUPU PEKE YAKE KWA MUDA MREFU SANA UNAWEZA KUPATA UTAPIAMLO (MALNUTRITION).
SIKU YA KWANZA
· Kula matunda aina yeyote isipokuwa ndizi.
· Matikiti maji yana calories chache kuliko matunda mengine kwa hiyo ni bora kula hayo.
· Siku hii kula supu peke yake na matunda.
· Kunywa chai isiyo na sukari pamoja na maji.
SIKU YA PILI

· Kula mboga aina yeyote ile.
· Kula mpaka ushibe mboga ambazo ni fresh kama vile saladi au mboga za majani zilizosindikwa kwenye kopo.
· Usile maharage yaliokaushwa, njegere au mahindi makavu.
· Kula hizo mboga pamoja na supu.
· Kwa chakula cha jioni siku hii unaweza kula kiazi kimoja kikubwa kilicho okwa na unaweza kupakaa siagi.
· Usile matunda ya aina yeyote nyingine.
SIKU YA TATU

· Kula supu, matunda na mboga za majani aina yeyote.
· Usile kiazi kilicho okwa.

Kama utakuwa umekula kama ilivyo onyeshwa hapo juu, na huja danganya, basi utakuwa umepoteza uzito wa mwili kwa wastani wa kilo 2 mpaka 3 baada ya siku hii ya tatu.
SIKU YA NNE

·
Kula ndizi mbivu na maziwa yaliyopunguzwa mafuta (skimmed milk).
· Unaweza kula ndizi mbivu tatu, maziwa glasi nyingi uwezavyo pamoja na supu.

SIKU YA TANO


· Kula nyama ya Ng'ombe na nyanya fresh.
· Kula nyama kiasi cha robo mpaka nusu kilo pamoja na nyanya fresh kadiri uwezavyo.
· Jaribu kunywa glasi 6 mpaka 8 za maji ili kupunguza uric acid kwenye mwili.
· Kula supu angalau mara moja siku hii.
SIKU YA SITA

· Kula kiasi chochote cha nyama ya Ng'ombe na mboga za majani. Ni bora kula saladi kwa wingi pamoja na nyama, lakini usile kabisa Viazi siku hii.
· Hakikisha unakula supu angalau mara moja.
SIKU YA SABA

· Kula wali, juice isiyo na sukari na mboga za majani. Kula kadiri utakavyoweza.
· Hakikisha unakula supu angalau mara moja.

Inategemewa kuwa baada ya siku ya saba utakuwa umepoteza kati ya kilo 4.5 mpaka 7.7 ya uzito wa mwili.
Kama umepoteza zaidi ya kilo 6.8 simama kwanza kwa siku mbili kabla hujaendelea na huu utaratibu wa mlo tena.
Utakapo anza tena, anzia siku ya kwanza na kuendelea mpaka siku ya saba tena.
Kwa kuwa miili ya binaadamu inatofautiana, diet hii italeta mabadiliko tofauti tofauti kutegemea mwili unavyo ipokea. Kawaida baada ya siku tatu mwili wako utajisikia nguvu zaidi kama hujadanganya.
VITU VISIVYO RUHUSIWA KABISA WAKATI WA DIET HII.

· Hairuhusiwi kutumia Mkate, Pombe aina yeyote, vinywaji vyenye gesi kama vile soda na vyakula vilivyo kaangwa na mafuta.
· Tumia maji, chai isiyo na sukari, kahawa isiyo na maziwa wala sukari, juice za matunda zisizo na sukari na maziwa yalio ondolewa mafuta (skimmed milk).
· Unaweza kula Kuku aliochemshwa au kuokwa badala ya Nyama, lakini uondoe ngozi yake. Unaweza vilevile kutumia Samaki aliyechemshwa katika siku moja inayohitaji Nyama badala ya Nyama lakini sio zaidi ya siku moja.
· Supu hii inaweza kutumika saa yeyote unapo hisi njaa. Kunywa uwezavyo. Kumbuka jinsi unavyo inywa kwa wingi ndivyo unavyo punguza uzito.
Supu hii haingiliani na dawa zozote utakazo andikiwa.
Endelea na utaratibu huu mpaka utakaporidhika kuona mabadiliko katika mtazamo na mwili wako.

ANGALIZO
Hii soup inapunguza mwili kwa haraka sana ila ukishapungua inabidi uangalie mlo wako inabidi upunguze vyakula vya mafuta mawali maugali badala yake ule mboga nyingi kuliko chakula, sio baada ya wiki unaanza kufakamia misosi mfululizo utanenepa zaidi ya mwanzo.
 
Hivi unajua pamoja na kazi kubwa ya kuandika maandishi yote hayo, lakini umeshindwa KUELEZA IPASAVYO namna ya uandaaji wa hiyo "SOUP"...
In short umeeleza tu namna ya kukata mboga(am assuming ni hizo kabeji), halafu unazitokoza hadi zilainike, mwishoni unaziblend na kuongeza chumvi au pilipili.
Ila hapo awali nimeona kuna mahitaji uliorodhesha ila sijaona kama umeainisha namna ya kuyatumia katika uandaaji wa 'SOUP"
 
Habari senyu kwa mpigo.

Kwa wale wenzangu na mimi vibonge suluhisho hili hapa. Hapa kati niliongezeka uzito kwa kiwango kikubwa sana, kasheshe ikawa ni jinsi gani nitapungua kufanya mazoezi kidogo ni mvivu na pia hata muda wa kufanya mazoezi sina. Nimekunywa juice ya ukwaju wapi? maji moto na limao wapiiiiiiiiiiiiiiiii dah kidogo nikate tamaa nikasema labda uzee huu unaonijia inawezekana ndio imetoka hiyo kwa nini kila ninachojaribu kinashindikana

.

[h=5]
[/h]


Hawa inawahusu samahani lakini?
 
Hivi unajua pamoja na kazi kubwa ya kuandika maandishi yote hayo, lakini umeshindwa KUELEZA IPASAVYO namna ya uandaaji wa hiyo "SOUP"...
In short umeeleza tu namna ya kukata mboga(am assuming ni hizo kabeji), halafu unazitokoza hadi zilainike, mwishoni unaziblend na kuongeza chumvi au pilipili.
Ila hapo awali nimeona kuna mahitaji uliorodhesha ila sijaona kama umeainisha namna ya kuyatumia katika uandaaji wa 'SOUP"

Sijaiandika mimi mpendwa nimeicopy huko nilikoitoa kama ilivyo na kupaste hapa, mimi niliprint nimefuata maelekezo hayo jinsi yalivyo na imenisaidia, sifanyi matangazo ya biashara nimeiweka ili kama kuna mtu amechoka unene kama ambavyo niliuchoka mimi atumie na inaweza kumsaidia
 
Lol, asante mdada uloshare hii habari, i had one diet, hii soup walikuwa wanaita "wounder soup" kama ulivyosema kiukweli hii supu mimi ilinishinda, mmmh, may be nijaribu tena, ila mimi nimefanya diet, so far nimeshaloose 20 kgs, na ninaendelea nayo, ninakata kilo 3 kwa week kama sikucheat, nikicheat 1 - 2 kgs!
 
haya mazuri sana bana utakuwaje kimbau mbau bana!!! hii ni hazina ya taifa
Umeona eeh? Watasababisha fahari ya macho ipotee mujini...jamani wengine tunaenjoy kuona vibonge...stress absober
 
Umeona eeh? Watasababisha fahari ya macho ipotee mujini...jamani wengine tunaenjoy kuona vibonge...stress absober

haya mpwa yana raha yake bana upo nalo maeneo maeneo umekaa nalo unapata moja baridi moja moto likaenda toilet angalia meza za karibu wanaume kwa wanawake wanavyo tumbua mimacho kuangalia Singida Dodoma kama wamebanwa na mlango.
 
Madame B watu wenye shepu za hivyo ni wachache sana. We ukipita barabarani unakutana na wangapi wenye pododo kama lako? wengi wamenenepa hovyo hovyo tu matumbo yametangulia

kumbe Maty unazungumzia wenye shepu ambazo ukiwa mita 35 huelewi wapi ni mbele na wapi ni nyuma sio?
 
Last edited by a moderator:
Aksante Maty it really work nilishaijaribu kipindi flani ikanisaidia.

tuseme sasa umeacha na kufumuka na kupoteza shepu mbele hakuelewiki na nyuma nako hakueleweki, mbele unaweza sema nyuma na nyuma unaweza sema mbele?
 
Ukipata ya kuongeza mwili tustue.

Kunenepa rahisi tu kula vizuri fakamia msosi hasa minyama, chips mayai kwa sana soda tano kwa siku maji kunywa kwa msimu ukisikia kiu kuywa pepsi. Ukiona unafanya yote hayo hunenepi basi una roho mbayaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa inakukausha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom