Habari kwa Picha

View attachment 1072281Patrick Oita Nyapara, ambaye ni police nchini Kenya alimuua mpenzi wake kwa kumtandika Risasi 7 baada ya binti huyo kumkataa, pindi alipomaliza masomo Chuo Kikuu. Kwa maelezo ya Patrick ni kwamba alimchukua mdada huyo aliyejulikana kwa jina la Christine Maonga kutoka katika familia duni kijijini na kumpeleka mjini Nairobi kama mke wake ambapo aliamua kumsomesha mpaka chuo kikuu. Alikuwa akimlipia karo na mahitaji mengine pamoja na kutuma pesa kwa mama mzazi wa binti huyo kama msaada kutokana na familia hiyo kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama za maisha. Baada ya kuhitimu masomo yake, Christine alimwambia Patrick kuwa amechoka kuwa naye kwani ni mtu asiyekuwa na hadhi yoyote na hafai kuwa mpenzi wake hivyo ni vyema kila mtu afanye mambo yake. "Nimepata mpenzi mwingine ambaye ananifaa sana pia ni Mkurugenzi wa Kampuni moja kubwa sana jijini Nairobi hivyo siwezi kuwa na wewe Patrick mtu usiyekuwa na future na ni daraja D ambalo ni dhaifu kwangu", alisema Christine. Patrick hakuielewa kauli ya mpenzi wake, akaamua kwenda kijijini kwa mama yake na Christine kuomba msaada wa suluhu ili aweze kumuoa binti yao kwani alikuwa ametumia gharama kubwa mno kumsomesha. Mama yake binti alijibu kuwa hawezi kumpangia mtoto wake mume wa kumuoa hivyo anapaswa aachwe ajiamulie yeye mwenyewe. Patrick hakukubali, akamtafuta dada yake Christine na kumwelezea hali halisi lakini alijibiwa kuwa hana hadhi ya kumiliki mwanamke aliyehitimu Chuo Kikuu hivyo atafute mwanamke wa level ya mgambo kama yeye. Aliondoka na kurudi nyumbani na kuchukua uamuzi mgumu wa kumuita Christine nyumbani kwa lengo la kuongea na kumaliza tofauti zao ili waachane kabisa, binti alienda nyumbani kwa Patrick mapema zaidi. Alifika na kumkuta Patrick amejihami kwa silaha, hawakuzungumza chochote zaidi ya kumkandamiza risasi 47 na zote zikapita mwilini mwa Christine hali iliyopelekea kifo chake papo hapo. Nini maoni yako?
Hata pichani huyu dada sio wa kuishi na police.
 
Mchungaji gwajima ni mhanga wa tukio na sii mtuhumiwa kama watu wanavyodhani
 

Attachments

  • FB_IMG_1557666974579.jpg
    FB_IMG_1557666974579.jpg
    36.9 KB · Views: 42
Mchungaji James Ng’ang’a awamwagia matusi maaskofu , awataka wamuheshimu mke wake, lasivyo atawatimua wote nchini Kenya | _ kanisa la Neno Evangelist Ministry amegonga vichwa vya habari kwa mara nyengine tena baada ya kutishia kufunga matawi ya kanisa lake la Neno Evangelism akidai kwamba maaskofu hawamuheshimu mke wake. Katika kanda ya video iliosambaa katika vyombo vya habari , anaonekana akiwakaripia maaskofu kwamba atawafurumusha wote iwapo hawataheshimu onyo lake akidai kuwa matawi hayo yamekuwa vibanda. ”Wakati huu nitawaonyesha uwezo wangu… mwanamke yeyote ambaye hatamuheshimu mke wangu ….mulinipata hapa na wake zenu, mumejitajirisha kupitia juhudi zangu” . ”Wajinga nyie…wajeuri…nilikuwa nikihubiri katika mkokoteni , naapa mbele ya Mungu nitawaonyesha Ng’ang’a ni nani….”. Kwa mujibu wa BBC. Mchungaji huyo anaonekana akiwaambia kwamba ni kinyume kwa wao kujigamba kuhusu utajiri waliojipatia kutoka katika kanisa lake na bado hawamuheshimu. ”Nataka kuwaambia nyinyi maaskofu, iwapo hamutamuheshimu mke wanngu nitawafurumusha katika kanisa langu. sitaki kujua wewe ni nani”, alisema mchungaji huyo. Ng’nga anasema kuwa amefikisha umri ambao anahitaji kuheshimika na maaskofu wote. Ninapo kohoa lazima mutii, alisema. Mchungaji huyo alisema kuwa anakabiliwa na changamoto kwa sababu shetani anataka kuliangusha kanisa lake. ”Shetani anakabiliana nami kwa sababu anataka kuniangusha, hakuna kitu munachoweza kuniambia….Mimi ni Neno na ndio maana ninapigwa…. Sitawaruhusu nyinyi na wake zenu kunipatia msongo wa mawazo zaidi”,alisema. ”Iwapo munataka kujiita maaskofu, munahitaji kufikiria kule mulikotoka, ni vipi munajigamba mbele yangu na mulikuja kwangu na umaskini…nitawafukuza nyie nyote… takataka”, aliendelea. Amesema kuwa atayafunga matawi yote na kusalia na makao makuu pekee. Ng’ang’a aliwataja maaskofu wake kuwa watu wasio na maana, wajinga na wasiomuheshimu kama mtu aliyewasaidia. ”Ni lazima waniheshimu la sivyo nitaelekea kuvifunga mimi mwenyewe vibanda vyote nibakie na kanisa kubwa lililopo jijini Nairobi. Mimi ndio mwanzilishi wa Neno”, alisema huku akipongezwa na wafuasi wake
61513779_134781731040426_8063452010958066192_n.jpg
 
Maajabu ya Mwenyezi Mungu ndani ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, mito miwili inapokutana na kuwa mto mmoja bila maji yake kuchanganyikana. Mto KASAI na mto MAYINDOMBE.
65129385_509891299550186_4891654179929892633_n.jpg
 
FAHAMU: Expire date iliyo kwenye chupa ya maji ni tarehe ya mwisho wa matumizi ya chupa sio maji. Ndio, unatakiwa kuzingatia sababu chupa inapofikia ukomo wa matumizi inaweza kutoa kemikali kwenye maji, Kemikali ambayo inaweza kukuathiri afya yako.‬
101029304_852973538532009_1697547530718933583_n.jpg
 
81437867_143264214002269_1067494191049110106_n.jpg
Mwanaume mmoja nchini Kenya amejisalimisha kituo cha polisi akiwa hana nguo baada ya kukimbia kutoka kwenye fumanizi nyumbani kwa mke wa Mwanajeshi Jijini Nairobi. Imeelezwa kuwa askari alirudi ghafla nyumbani bila taarifa na kumkuta mkewe na mwanaume huyo wakiwa ndani.
 
Back
Top Bottom