H.Kasongo Hour-Emanuel Ole Naiko Katia Aibu

¢ Extractive Resources Abundance in the Country
l World number one producer of Tanzanite.
l 4th Africa producer of Gold after South Africa and Ghana and Mali, followed by Burkina Faso
l Availability of natural gas, (oil exploration continues), diamond, uranium, titanium, nickel, iron ore.
¢ Inadequacy of
l Mining policy of 1997 [2009 does not intend to empower public but to facilitate administration/Govt.]
l Mining Act of 1998 [2010 there are still, unresolved issues around ownership, compensation, but the overall vision]
l Petroleum Act 1980/2008
l Energy Policy 1992 (revised 2003) – Mainland only, not in Zanzibar.
l No policy and law for gas
l No policy and law for Corporate Social Responsibility (CSR)
¢ Public voices on
l Increasing levels of poverty (resource curse?) - Human Development Reports.
l Dissatisfaction with foreign investors' role/operations (Extractive Industries).
l Lack of transparency and accountability in MDAs and Revenues from EI
l Human rights and environmental concerns of mining companies

¢ Government Responses
l Recommendations of Masha and other Committees on mining operations in Tanzania
l Bomani Committee report and its recommendations on EITI (2008

¢ Status of Foreign Investment in Tanzania's Extractive Industries
l Barrick Africa Gold ( North Mara, Kahama Gold/Ulyan'hulu Mine, Buzwagi and Biharamulo/Tulawaka)
l Anglo-Ashanti/Geita Goldmine
l Petra Diamond (WDL)
l Tanzanite One ( Mererani)
l Resolute Mining
l East Coast (Pan Africa Energy) - Songo Songo gas production)
l Artumas Group (Mnazi Bay gas production)
l Over twenty Petroleum Exploration Companies (e.g. Tullow Oil, PetroBras, Animex, Statoil).
 
Mie ni Fundi mchundo wa Ujenzi na nusu Mhandisi wa ujenzi mambo ya barabara.

Ukimsoma Waberoya utagundua kuwa ni kweli anaweza kuwa Mhandisi ila ni mhandisi wa ujenzi tu na siyo madini au anaweza kuwa mhandisi wa Madini ila si wa ujenzi. Walimdanganya kuwa yeye na wahandisi wa ujenzi, hamna tofauti sana. Ukweli ni kuwa kuna tofauti kubwa sana hata huwezi kuamini.

Alisoma shule moja ya ovyo sana au yeye mwenyewe alikuwa ni mvivu wa kutafuta na kuunganisha mambo.

Tafadhali bana, hizo michanyato uliyoweka hapo nyuma, imetosha kukufahamu.

Labda kama kwa makusudi tu ulitaka kudanganya watu hapa wasiojua hiyo kitu.

Kwenye ujenzi pia kuna somo la mazingira. Usafiri unasababisha sana Co2, makelele, mitetemo nk.

Ila huwezi kusema STOP kwani kwa dunia ya sasa utakuwa umeuwa kila kitu.

Ndipo wanapokuja na neno linalosemwa "Sustained transport".

Sihitaji kuwa na akili sana kufahamu kuwa hata kwenye madini inatakiwa iwepo hii kitu yenye jina karibu sawa na "sustained mine" kama sikosei. Hii maana yake ni Madini yachimbwe na mazingira yatunzwe. Kila activist analifahamu hilo na kila mhandisi analifahamu hilo.

Kuna mji walijenga Metro na kwa kutaka kusave pesa wakapunguza zile sponji zinazowekwa chini ya reli wakitegemea watu hawatalalamika. Ila watu wakaanza kulalamika sana kuwa metro ikipita, mitetemo hadi sahani kabatini unazisikia na mwisho wakaifumua reli na kuweka hizo sponji. Wahandisi wengi wa ujenzi/madini/ nk huu ni mchezo unaofahamika sana.

Kwa hiyo Waberoya, unachokisema naweza kukiita "unapishana na ukweli".

NB:
Kama nyie mnaishi karibu na High way na mchana/usiku makelele ni mengi sana, msisite kula sahani moja na Tanroad ili wawawekee kuta au miti za kupungza makelele. Mkisema "Mungu yupo" basi wao wanasema hewala.Haka ndiyo kamchezo ka akina Waberoya milele. Ukisema, wao wanadai "Activist" na wakati huo wao wanakula hela na sifa kuwa MHANDISI BORA.
 

Asante kaka nimekupata nimekuelewa!
 

Asante Rufiji kwa hoja nzuri

Kama ulivyosema pengine nazungumza vitu vingi kwa wakati mmoja, acha nijaribu kujirekebisha hapo

Ninachozungumzia ni kuwa issue za renewable na non renewable hawa watu walikuwa wanaongea nini mpaka wakafika huko? kama unavyosema tatizo ni mikataba, na mimi ninasema issue za mikataba ni ngumu sana, zimeshikiliwa na group fulani la watu ambao ni wenye nguvu ambao hata JK hawezi kufanya kitu kwa mikataba ya sasa! Botswana unazungumzia nchi yenye watu 1.5m people! bado hata huko mikataba ni mibovu japo utaona inasaidia , leo ukienda kahama, mwadui n.k unaweza kuona wameendelea na mkabishana sana simply kwa sababu ya service ya jamii.

Mikataba ya madini ni migumu, na ingekuwa mimi suluhisho ni aidha kutochimba au kuwa na wataalamu wetu wachimbe wenyewe.

Nimeshuhudia maandamano Mji fulani Canada kisa mikataba na uchafuzi wa mazingira nayo ni mwaka jana tu! walikuwa wanalalamika kampuni ya kizawa inayoitwa Vale kuuzwa kwa kampuni ya ki-Brazil inayoitwa Inco ikanunua na kampuni inaitwa Vale-Inco, katika explanation za serikali na projects za wanafunzi wengi wa mining ikawa kutafuta ufumbuzi na kujua kulikoni. kumbe issue ni Marketing, Inco ndiyo wauzaji pekee authorised wa Zinc nchini China, na wanachofanya hawapokei madini toka kwa kampuni nyingine, ndio dunia inavyoenda

Hapa Tanzania we have suffered the same in Tanzanite! bila Tanzanite kuwa na label ya Tanzania one ilikuwa haihuziki, swala la kuwa soko la madini ni monopoly sidhani kama lina ubishi sana. Tanzania pia kampuni za Ashanti zimeuawa simply kwa sababu hizo hizo na yamebaki majina operators ni wengine kabisa. Ashanti Ghana waliponea chupuchupu kwenye same issues na ikabidi waingie ubia na makapuni mengi, kuna Anglo pale na GGM !!!

Solution:

Sijajua ubishi uko wapi, we have to hit the target

Kwanza soko la madini liwe Africa, na kwingineko, we have to make sure tuna process madini mpaka final products, then tunatengeneza various products ambazo wateja wanataka.

Tukiwa na soko la finished products then tuta-mine kwa mitaji na uwezo wetu kiteknolojia.


Trend au status ya madini sasa ni sawa kabisa na issues za Pamba, katani, kahawa miaka ya 70 na 80, kitu ambacho hata wale wazalendo walishindwa.

Madini yanabiashara yake na watu wake wa tofauti kabisa, some say freemasons...

Bila hivyo tutazungumza, tutachukua video, tutaanzisha website, tutatukan, watu wanavuna na wanaondoka nayo, sisi tunatukana na kudharauliana humu. kushinda kwenye TV kuongelea mikataba ni anaother kichekesho,walipobadilisha mikataba ya madini hivi karibuni kilichotoka ni kichekesho kingine tu!!! hatuna wataalamu wa hii fani, wahandisi wengi tunajua kutumika kama robot na sio kwenye maamuzi.

Rufiji ukinipa nchi sasa hivi , nastopisha kwanza hizi shughuli za madini. tunatakiwa tujipange upya. Botswana nao wameona hilo tatizo na wanasomesha watoto wao kwenye hiyo sekta like crazy.

Rufiji angalai amijadala yoote ya madini uone inakoanzia na inakoishia, kwa mjadala wa juzi ndiyo imetoka hiyo, mjadala mwingine mwakani! itakuwa 2040, 2050 with same CCM no-way nothing will be done real
 
Hivi mnafahamu kuwa Ole Naiko aliwahi kuwa mkurugenzi mtendaji/ CEO wa mgodi wa dhahabu buckreef for something like 5 yrs????????? Sasa inashangaza anvyokuwa ancomment completely kama layman!
 
Waberoya,

Ulikuwa ni ukweli na utani kidogo. Kama ulichukua, utakuwa ulifanya makosa. Don't take it personal.

Habari ya mwisho imenifurahisha maana umechambua vizuri soko la madini.

Nilishawahi kuona historia ya soko la Almasi duniani. Pamoja na kusema eti sijui kampani gani pekee ndiyo ilikuwa inauza madini duniani, Wayahudi walikuwa wakionekana sana mitaa ya Charlottenburg Berlin na magwanda yao meusi na vibahasha. Siku nzima wanazunguka tu na ndani wamebeba vibahasha vya almasi. Almasi za Sierra leon walikuwa wakiuza sana na wengine walikuwa hadi wanaingia huko kuzitafuta. Ila sasa hivi Wayahudi wamewekwa chini na kampuni la India.

Tukija kwenye madini kama dhahabu, nchi za Asia wana masoko mazito sana ya hii mikufu na vito vingine vya thamani na masoko yao yako waziwazi. Tatizo la nchi zetu ni watu masikini na waliokuzwa kwenye familia masikini kama za Kinyamwezi na ghafla mtu huyu anakuja kusoma na kupewa kazi ya kuwekea mikataba. Kwanza akikaa meza moja na Wazungu basi anaomba na picha apigwe ili akawaonyeshe ndugu zake na maneno yanaanza "nilikuwa naongea na Obama, nilikuwa naongea na Sarkos nk" na inapokuja huyu mtu anataka kuweka mikataba, basi tunamfungulia hadi chumbani. akitutupia vi milioni 10 hapo bank, sisi "chukua yooote." Na Wazungu walivyo na akili nzuri, wanakomba yote.

Kwa hali ilivyo sasa na hasa globalisation, tungeliweza kabisa kuwa tunatengeneza half product au full product na kuuza. Kama wanelijifanya kutuzuia kuuza kama nchi basi wangelipewa watu kadhaa wakawa matajiri sana ingawa ukweli ubaki kuwa ni USALAMA WA TAIFA na mali zao nyingi zinaingizwa nchinina kufanya miradi na serikali huku wao wakitoa pesa nyingi. Wangilewaza hata kuwa na mashirika makubwa ya ndege na ya utalii. Utalii kuja Tanzania inakuwa bei nafuu na watalii wakija, wanakuja na kuzuoa vito kadhaa. Kuna maduka mengi tu siku hizi na kuna hata kuuza kwenye mitandao kama watu wana uhakika kuwa ni kampuni ya kuaminika.

Kwa ufupi ni kuwa kuuruka ubabe wa hawa Mabanyenye kwa sasa ni mkubwa sana. Ni wajinga tu hawataki kuamini hivyo au wanatudanganya kuwa hivi vitu haviwezekani. Kama Mhindi akikataa basi kuna Mchina. Kama Mchina hataki basi kuna akina Taiwan, Indonesia, Korea nk
Asante kaka nimekupata nimekuelewa!
 
Waberoya,
Nilitembelea mji wa Victoria Canada wakati mmoja. Kuna eneo walikuwa wanachimba madini. Yalipomalizika kampuni ya madini ilikuwa imesaini mkataba wa kuziba makorongo na kupanda miti na maua kuficha mashimo waliyoyaacha. Hivi leo hilo eneo la bustani linavutia watalii wengi kwani kumepandwa kila aina ya maua na kwa kweli usipoelezwa historia yake huwezi kujua kuwa once upon a time lilikuwa ni eneo la machimbo ya madini. Sisi huo ujanja hatuna. Tutabaki kuziba mashimo yetu wenyewe wazungu walishaondoka na madini yao. Kwa hiyo wape activists some credit.
 

Waberoya,

Nakubaliana na mengi uliyosema lakini nadhani tatizo ni zaidi ya hapo. Mimi nadhani tatizo la madini linaongezwa na rushwa ndani ya nchi yetu. Ni kweli masoko mengi ya madini yana monopoly ya hali ya juu mfano Debeers na almasi, lakini hii aijustify serikali yetu kupata 3% kama kodi kutoka kwenye haya makampuni. Nadhani tungeweza kupata zaidi ya hapo kama tungekuwa na watu ambao wangedesign mikataba inayojali maslahi ya taifa. Nchi kama Botswana, diamond pekee inacontribute 36% ya GDP. (BOTSWANA MINING REPORT - BABY CARE). Tatizo ni kuwa viongozi wetu huwa wanakula mlungula wakati wakienda kusaini hiyo mikataba!

Pili, resources ambazo nchi yetu imebarikiwa haziendani na uwezo wa kufikiri wa viongozi wetu. Ni jambo la kusikitisha kuona Rais wa nchi akitafuta misaada ya vyandarua wakati nchi ina resource za kumwaga.
 
Congratulaturations wachangiaji, mnatoa constructive ideas.
Hawa waleji wa vijisenti ndiyo wanaotuangusha maana hawayatilii mkazo mkazo mawazo mazuri kama haya.

Bado nalia na Ole NaikO, Akili yake ina MaRue Rue!!
 
Sentensi ya kwanza uliposema tofauti kati ya professional view na activist view, inaonekana una puuza "activists" na unaona "professionals" ni wa maana zaidi - ukijihesabu mwenyewe kuwa ni professional. pia unatangaza kwamba kuna wakati huwezi kuongea na Lissu kwa kuwa "ideas nyingi ziko ki-activist zaidi kuliko professional...". sasa Activist ni Activist, professional ni professional. activist ni mtu anayehamasisha mabadiliko, actively. Lissu ni mwanasheria kwa fani, "professional wa sheria" na ukiangalia rekodi yake, amefanya mambo mengi sana kisheria, yanayohusiana na mazingira. ametoa mchango mkubwa sana katika kuhamasisha jamii kuilewa na kufanya kitu kuhusu sekta ya madini. natambua kwamba kuna wakati kuna watu "walihukumiwa vifungo jela" kwa msukumo wa rushwa, ili kuwanyamazisha, na Lissu alifanya kazi ya ziada katika fani ya sheria kukata rufaa na wakaachiliwa. natamani sana tuwe watanzania wengi ambao tunafanya vitendo vya kuonesha wazi yale tunayoyapinga. Lissu ni taa muhimu katika mambo haya. nashangaa unaonesha kupingana naye sana, au unaona "anaingilia profession" yako? mbaya zaidi unatangaza kukubaliana na Naiko "kuna ya ukweli aliyoongea Naiko".

by selectively choosing to paint Naiko positively, albeit on some issues, and taking issue on the points you do not agree with Lissu, you are making a very big point, which I have a big problem with. Naiko is an instrument of the plunderers and is there to protect the interests of big companies. someone has to speak for the disadvantaged majority, and Lissu is doing a good job.
 
What would you expect from Ole Naiko? He is as hopeless as his superiors! He always talk nonsense, I saw him on tv the other day suggesting or rather justifying fuel taxes exemption for mining investors because of limited access to electricity. Can you imagine? it is as if the so called investors were not aware of the conditions around their investments. I kindly ask Ole and the likes including the Ministerof Energy ..., to keep quiet instead of talking nonsense. We very much know what is going on in the mining sector and just because we are quite don't assume we are stupidy. Please give us break
 

You have said it all!

Kwa nini tunang'anga'ania wawekezaji wa kizungu?

I believe tungeelekeza mawazo yetu Asia at least tungekuwa mbali sana kwa mambo mengi, kwanza kuanzia vifaa vyao ni affordable japo siyo durable sana, lakini kwa sasa ilivyo is easy to transfer knowledge kutoka Asia to Africa na siyo kutoka western.

I strongly believe tungewezana kushindana nao na hasa kwenye mikataba, lakini inakuwa ngumu ku-tie nao kwa sababu tumejidekeza kuomba omba kwa wazungu!



I know well that project is interesting, the same kind of project has been done in Sudbury ambapo nimewahi kuifanyia project ya ku-evaluate risk assessment. Tatizo sheria zetu zipo na zinasema fukia mashimo, ILA hatuna standard za kusema kuwa ardhi ikichafuliwa na cobalt, lead, nickel,zinc n.k hizi husambaa ardhini kwa namna nyingi sana na kwa umbali mkubwa, sudbury let say lead iko kila mahali! na mwekezaji inabidi afanye survey na kushusha viwango vya madini chafuzi haya sio alipochimba tu na maeneo mengine likely, sasa kuna vipimo vya haya madini ni kwa kasi gani yanatakiwa ardhini, ikizidi inabidi yanpunguzwe, sisi hatuna hizo standard na kwa wawekezaji wetu KUFUKIA tu sio tatizo kwao, they enjoy doing it because it is cheap for them! inabidi kuweka viwango kama hivyo vya victoria na sudbury. wanasiasa wengi hawajui hilo, hawataki kuelezwa na tunaishi katika hali hiyo, mfano mzuri sana hapa TANZANIA wa sehemu ambayo ni jangwa ni chunya.


Umeongea jambo zuri, hata hiyo 36% bado wanaliwa na kisingizio kilekile kuwa capital ni kubwa sana, ardhi yangu, machine zako, weka share ya nusu kwa nusu!! 50% would do better, au kutofanya kabisa. Botswana wana bahati nyingi mbali ya kuwa wako milioni moja na nusu, ila mahusiano yao na nchi za nje ni mzuri sana, ndio maana wanaenda nchi nyingi pasipo kuwa na passport, viongozi wao walifanyakazi ya ziada.

To my opinion Rufiji kama ingekuwa kuna uwezekano wa kuziondoa baadhi ya nchi, basi nchi hii haikupaswa kuwa africa!! there leaders are best.


Pole sana naona umeumia kusema issue kuwa Lissu ni activist, challenge niliyotoa ni kuwa ajikite zaidi kujua hali halisi ya mikataba, soko la dunia na akina nani ni wawekezaji na kwa nini tunalazimika hali iwe hivyo. ona mfano wa alichoongea Sikonge hapo juu-'ASIA thing', activist wengi wame-rely just one direction,one angle, one view, sijasikia wakisema wawekezaji watoke asia, sijasikia wakilalamika mfumo wa soko la madini duniani, sijasikia wakisema jambo la kutatua hali ya sasa, KILIO CHETU CHA MADINI NI SAWA NA UFISADI we may just ending talking and talking! kuwa aina Lissu wakishirikiana na wataalamu hasa wahandisi wanaweza kufanya kazi nzuri sana na hata ya vizazi vijavyo, kukaa na kuongea na akina Ole NAIKO ni kupoteza muda!!1 I repeat is a waste of time na ndio maana naona issue zimekaa kisiasa zaidi kuliko hali halisi.

Tatizo ni kubwa na Ole kama ni issue za madini ni chekechea
 
Hii nchi mbona ni kama haina enyewe??
Ukisoma post za kwenye hii thread, ukimbuka wale vikongwe waliooza sura kule Northen mara kwenye ule mgodi halafu mtu kama Ole naiko anasema kila kitu ni sawa na huwezi kubadilisha, wakati huo huo JK anaandaa bakuli la kwenda kutembeza huko ulaya wakati resouces tunazo ila tunendekeza ubinafsi na kuruhusu watu wajichukulie unabaki na maswali yasiyo na majibu........But thanks kwa JF maana haya tusingeweza kuyajua.
 

Then we need to find sensible people to discuss this serious issue at hand! Ngeleja likewise is another confirmed fisadi. Tukilijadili hili kwenye medani ya kimataifa tutapata result nzuri kuliko kuwaambia CCM wale matapishi yao. Naiko ni injinia wa madini ni registered na ni mwanasiasa unaona kabisa siasa ilivyodumaza taaluma yake.

Museven alichofanya ni kuwapeleka nje wataalamu na kuwasomesha hasa issue za mikataba, na kasema wakikosea tu , anao!
 

Is Naiko realy qualified engineer? IS he engineer by profession? Au kajificha kwenye mgongo wa bodi wa hiyo registration. Jaribu kufutilia toka alipokuwa huko buckreef

Je kwa maneno ya ni Ole Naiko ni sawa kusema wale wote waliosajiliwa na hiy bodi ni mainjinia wa ukweli ukweli na sio wa kisiasa.
 

Weberoya umeeleza mambo mengi vizuri nakubaliana na wewe menbi na nina tofauti kimtazamoa kwa mengine

Naongeza kuhusu sera mbovu za na sizizo na mwelekeo za mambo ya nje
kitu kikubwa sana kinachotuangusha Tanzania ni policy mbovu ambazo hazina tija kwa taifa na na za kisiasa zaidi. Sekta hii ya madini imekamatwa na waisrael. Tanzania haina uhusiano wa moja kwa moja na waisrael kwa sababu za kisiasa. Mtokeo yake tunaweza kujika tunpokea second class investor wa madini.

Waisrael wafungue kampuni South africa then ile kampuni ndiyo ije kwa mgongo wa wasouth au wacanada. Hiyo Maana yake kuna mapato yanapotea. Utashangaa kenya haina mashimo ya dhahabu mengi lakini dhahabu wanayouza mhhhh. Wamekuwa wajanja wenzetuwamekamta waisrael

So it time watu viongozi waache wa mambo ya sera za kisiasa za mambo ya nje zinazowafungia wawekezji halisi
 
OLe NAiko;Madini ni Renewable nenda India na hata SouthAfrika madini baado wanachimba tuu na hayaishi

Mnaomjua Ole Naiko na kwa kauli hii;huyu jamaa huwa anapuliza bange au?
 

Tatizo la mikataba wala siyo gumu au kitu cha ajabu kama wengi wanavyotaka watu waamini. Mikataba yetu ni mibovu kwa sababu walioiandaa hawaifahamu biashara ya madini kikamilifu, wengi wanadhani kwa kuwa ni wanasheria, basi wanaweza kuandaa mikataba ya kila aina hata kwa business ambayo hawaijui vizuri. Tunatakiwa kuwa na wataalam wa mikataba ya biashara ya madini ambao watashirikiana na wataalam wa biashara ya madini.

Nimewahi kuangalia mikataba ya baadhi ya makampuni ya madini na pia kuitazama sheria ya madini na sera ya madini, kote utagundua kuwa kuna upungungufu mkubwa wa kuielewa biashara yenyewe. Wengi wanaiona kuwa ni kama biashara nyingine. Waandaji wa mikataba kwanza wanatakiwa kujua ni kwa namna gani makampuni ya madini hupata faida, uwekezaji wake upoje na ni kwa namna gani sekta ya madini huweza kuchangia maendeleo/ustawi wa Taifa. Usipojua makampuni ya madini hutengeneza faida kwa namna gani unaweza kushtukia sehemu ambapo kodi imeweka siyo sehemu inayotengeneza faida kubwa. Utasubiria hiyo kodi na hutapata. Kama hujui kuwa uwekezaji wake upoje, ndiyo unaingia kwenye mitego kama kuanza kutoza kodi baada ya kurudisha investment costs ilhali investment kwenye migodi ni continuous process, utashangaa mpaka mgodi unafungwa kodi uliyokuwa ukiisubiria hujaipata. Usipojua ni kwa namna gani migodi huchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi, unaweza kushtukia unahangaika zaidi na kodi za moja kwa moja huku ukiacha sehemu kubwa ya mapato ikienda kustawisha mataifa ya nje, n.k.

Kusema kuwa madini yetu tusiyachimbe mpaka tutakapokuwa tayari, sidhani kama ni wazo jema, tunahitaji rasilimali hizi zitumike kusaidia maendeleo ya nchi yetu. If we do not practice we will never acquire any skills in this sector. Ole Naiko not well understanding this industry does not mean everyone in Tanzania is equally ignorant. Kinachotokea ni kuwa kama ilivyozoeleka utendaji wa mamlaka zetu za serikali, hawataki kuwatumia watanzania wote wenye uwezo inapolazimika, hata kama si waajiriwa wa serikali.

Watanzania hatuwezi kuendesha migodi mikubwa pekee yetu na wala siyo hitaji muhimu la kuhakikisha kuwa tunapata faida kubwa zaidi. Leo hii hakuna hata nchi moja Duniani ambayo migodi yake humilikiwa na wananchi wake tu. Hii biashara ni ngumu lakini yenye faida kubwa. Inahitaji mitaji mikubwa, tecknolojia na uzoefu wa hali ya juu na pia ina risk kubwa. Na ndiyo maana ukienda karibu mataifa yote Duniani kwenye migodi, makampuni yanayoendesha shughuli za uchimbaji ni yale yale. Sababu kubwa ni kwamba makampuni haya yana mitaji mikubwa, yana teknolojia na uzoefu mkubwa, lakini pia yana uwezo to absorb risks. Katika sekta ya madini kampuni inaweza kutumia $100m kufanya utafiti katika eneo fulani, na baada ya miaka kadhaa ya utafiti majibu ya mwisho ni kuwa 'the project is not viable', na kampuni ikaondoka. Tunao watanzania wangapi au kampuni ngapi hapa Tanzania ambazo zinaweza kutumia kiasi hicho cha pesa, zikawa zimepoteza na wamiliki wakaona siyo tatizo, kwa vile ndivyo biashara hii ilivyo. Kwa mfano pale BuckReef (Biharamulo), IAM gold mpaka mwaka jana ilikuwa imetumia U$37m, wakaona mradi hauna faida, na wameondoka kurudi kwao. Haya makampuni yana uwezo wa kufanya hivyo kwa vile yana miradi mingi Duniani, wakati anapata hasara Afrika na Asia, amepata faida South America. Tusihangaikie sana umiliki wa migodi uwe wetu bali tuhangaike kupata faida kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini zinazofanyika Tanzania regardless who own those mines.
 
Nimeipenda hii;

GrEatThinkers,

OLe NAiko:
Madini ni Renewable nenda India na hata SouthAfrika madini baado wanachimba tuu na hayaishi.

Yaani mbavu sina, maana hii Serikali yetu inavyojifanyia mambo bora ucheke tu ukajiongezea maisha kuliko kuwakasirikia,, Nimeshachoka kuchukia aisee!

Kha!!!!!
 
Mtazamaji,
Si kweli maelezo yako. Kwa sasa, Wahindi ndiyo wana kampuni kubwa duniani la Almasi.

Pia USA sasa hivi wana-ZALISHA dhahabu. Hizi ni MAN MADE dhahabu na huwezi kuzigundua kama ni Natural au artificial.

Kwa sasa ni UK pekee kama sikosei ndiyo wana darubini ya kujua.

Na wanaweza kuzifyatua za rangi ya njano?? au zisizo na rangi (kama kioo).

Hii kitu walianza Warusi zamani na Ukoministi ulipokufa, USA wamenunua Technology na kuiendeleza.


Kama nilivyoandika jana, mambo ya biashara yalivyo sasa, unaweza kabisa kuwazidi akili Wayahudi. Kama Wahindi wameweza, kama Wachina wameweza, kama ...... Sisi tunashindwa nini? Tuache imani ya kusema ni Wayahudi tu au sijui South Africa. Masoko ni mengi sana sasa hivi. Tunaweza hata kufungua masoko yetu ya vito, saa, nk hapo China, India, Malesia, Taiwan, etc kama USA na EUrope watakuwa wanadengua.
Pesa tutakazopata, tunaweza kwenda kwao kununua vitu vingine. Wakiringa basi kila kitu tunaweza kununua ASIA.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…