H.Kasongo Hour-Emanuel Ole Naiko Katia Aibu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

H.Kasongo Hour-Emanuel Ole Naiko Katia Aibu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by spencer, Dec 20, 2010.

 1. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,796
  Likes Received: 1,338
  Trophy Points: 280
  GrEatThinkers,
  Jana sa3 usiku nilipata kutazama Channel Ten(Hamza Kasongo Hour) mjadala ulihusu Madini.

  Mambo yalikuwa hivi.
  TunduLissu:
  Madini si Renewable, maana yake mahali pakichimbwa na madini kuondoka haitatokea tena kuwa na madini pale. Hivyo mikataba yake ilitakiwa kuwa ni rasmi kwa mazingira yale

  OLe NAiko:
  Madini ni Renewable nenda India na hata SouthAfrika madini baado wanachimba tuu na hayaishi.

  TunduLissu:
  Kuna Uchafuzi mkubwa wa mazingira na kuna mashimo makubwa makubwa huko migodini, wananchi pia wanabwia Vumbi bila hata kufaidika na chochote. Nendeni mkajoinee jinsi maji yanavyomwagika na kuathiri aridhi yetu na sie tupo hata hatujali.
  OLe NAiko:
  Hakuna uchafuzi wa mazingira maana kuna utunzaji mkubwa wa kimazingira ile waste inahifadhiwa na miti kupandwa.

  Ukweli Halisi.
  Mgodi wa Buhemba ulifungwa na Mwl.1968 lakini hata leo ukienda kuna mashimo yaliyoachwa na wakoloni pia Geita mashimo yapo yaliyachwa na wakoloni. ni hatali sana

  TunduLissu:
  Hitimisho:
  Nadhani kuna umuhimu mkubwa wa kubadili Ownership Structure
  • Makampuni ya madini lazima yajiandikishe DSE ili watanzania wawaze kununua Share.
  • Serikali lazima ipate share no matter of the size lakini tuwemo kama taifa.
  • Local Authorities lazima zipate share na villagers ambawo wamehamishwa kupisha migodi.
  • Tutumie mapendekezo ya tume ya Masha na Bomani kwa sababu kuna mambo ya muhimu yameelekzwa ispokuwa hayafuatwi na serikali.
  • Marekebisho ya kupata 4% kutokana na revenue/mapato yote ya mgodi husika bado ni PEANUT/Kidogo sana ukilinganisha na uhalisia wa mambo.
  OLe NAiko:
  HITIMISHO
  Kila kitu kilichofanywa na Serikali hasa kwa sasaivi chini ya Ngereja ni safi kabisa.
  Naomba watanzania turidhike na tunachopata na bado narudia kuwa biashra ya madini ni kama biashara nyingine yoyote.
  Mikataba tuliyoingia hatuwezi kubadilisha katu.

  @@@:loco:Jamani ni machache kati ya mengi waliyoyaongea jana na niakamuona huyu Ole naiko kama kibaraka wa mafisadi.
  Shame On You OLE NAIKO.
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135


  Huyu jamaa wakati anzungumza haya alikuwa amepiga bange kidogo??????????
   
 3. c

  chamajani JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naogopa ku-comments "umbumbumbu" wa huyu Naiko bcz atakuja dai tunamwonea kwa kuwa Mmasaai! This guy z unrenewable! Shame on 'him'!¿
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Nilichoka jana, baada ya kuangalia mhojiano ya hicho kipindi
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Jina hilo kama nalifahamu vile??

  Hivi unamzungumzi Ole Naiko yupi au unamaanisha yule wakala wa Mnada wa Taifa wa UFISADI aliyewekwa kazini na EL??

  Tatizo mlipohama stesheni na kuporomosha kidhungu nyie wewenye mlitarajia akaseme nini zaidi.Rafiki, madini hata yachimbwe vipi kesho yanarudia tena na kujaa mishimo ile kwa ujazo ule ule tu.

  Achana na Lissu ni mtundu sana. Mwambie Teweli Teweli naye alikuambi hivo hivo kwamba madini yakichimbya na kupelekwa ma-ughaibuni huko wala haitoweshi kitu nchini hivyo MIKATABA FEKI ruksa tu!! Vema sana kwa jinsi ulivyoishukia hili swali.
   
 6. Mwanamalundi

  Mwanamalundi JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 3,034
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  nipeni mimi hiyo nafasi ya ole naiko.
   
 7. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #7
  Dec 20, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Lowasa alipoachia ngazi, nayeye kuulizwa kuhusu madini alisema Kuna mkakati wa kuwaandama Wamasai.
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Dec 20, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,600
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  Tatizo kubwa la hizi issue ni kuwa kuna tofauti sana ya professionals view na activist view

  Nikiwa kama Civil/Mining Engineer kuna nyakati ambazo siwezi kuongea na Lissu maana ideas nyingi ziko ki-activist zaidi kuliko professional point of view.

  At a glance bado watu wengi hawajui mambo mengi ya madini nchi hii, tumekuwa wageni, na hatutaki kujua, wala kujishughulisha kujua, hivyo kila siku hizi issue zitakuwa za hivi hivi tu, kuongea kulaumu n.k

  Kuna ya ukweli aliyoongea Naiko, nadhani challenge kubwa kuliko zote ambazo serikali ya sasa ina zi-face ni kuingia mikataba ya madini ambayo ni kichekesho, na ombi langu kwa activist kushika mpini hapo, mikataba ni mibovu saana, ambayo haiwezi kuelezeka wala kutamkika kirahisi

  Tukija mambo ya mazingira they will always find justifications na ujanja wao wakiishapata justification ya mazingira basi inakuwa assumed kuwa hata mikataba ni SAHIHI!!! digressive technique!

  Mikataba kwanza!!!!! kusema mazingira ni kusema mikataba iko sahihi!
   
 9. fige

  fige JF-Expert Member

  #9
  Dec 20, 2010
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hujaeleweka mkuu, naomba uweke sawa hasa pointi yako ya Tundu lisu kitaaluma. Kwa kuwa umejitambulisha kama mtaaluma
  Naomba utueleweshe alipokosea
   
 10. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #10
  Dec 20, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  namuunga mkono OLE, Uwezo wetu umefikia hapo na hatutaki kufuatilia mambo acha maisha yaende bwana!
   
 11. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #11
  Dec 20, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  NINA MASWAI MACHACHE KWENYE HUU MJADALA WA JANA

  1-Ole Naiko alipoanza alijitambulisha kama Engineer wa madini na mtu mwenye interest kubwa kwenye haya maswala sikumwelewa vizuri ina maana yeye ndiye Plan Maker au ni Mind seter wa serikali hkuhusu migodi na madini?Maana alisema walitembelea baadhi ya nchi na kuangalia utaratibu uliopo na wameridhika na hali ilivyo hapa kwetu
  2-Ole Naiko ni Director wa TIC,nataka kujua makampuni yote ya madini yamesajiliwa TIC au kuna chombo kingine kinachohusika na usajili huu
  3-Tundu Lisu alisema madini kama sekta inachangia 2.7% ya GDP kufikia 2009 ilhali 1997 ilichangia 1.9% ya GDP SIKUELEWA PIA
  4-Naomba riport ya Masha na Boman kama kuna mtu anayo hapa tafadhali
  NAOMBA WAKUU MNIELEWESHE
   
 12. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #12
  Dec 20, 2010
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wabeloya sijakuelewa una lenga nini??? Je Tundu Lissu pamoja na kuwa ni activits alichokuwa akisema kina logic au hakina??? Je Madini ni Renewables au non-renewable?? Je makampuni hayaachi mashimo na uchafuzi mwingine??? Je kama nchi 3 or 4% ya mapato tunayopata kama nchi ni halali??? Je suala la kusema kampuni zilipe cooperate tax baada ya kupata faida, je ni haki kwa nchi??? Je ni lini hizi kampuni kweli zitapata profit??? Ni nani anayekagua kujua kuwa kampuni zinapata faida au hasara ili zilipe Cooperate tax???. Mkataba mzuri ni ule utakao angalia masuala yote ya mahimu katika mkataba kama mapato kwa taifa, shares, uchafuzi wa mazingira na namna ya ku-mitagate matatizo hayo. Good project plan ni ile inayokuwa na mitigation plan wakati huohuo huku uchimbaji ukiendelea na sio kusubiri hadi mwisho wa project kama kampuni nyingi zinavyofanya.
   
 13. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #13
  Dec 20, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,875
  Likes Received: 2,817
  Trophy Points: 280
  Yaani TZ hatuna wasomi jamani tusidanganyane! Kama hata mtu aliyesomea madini anaona hiki tunachopata sasa hivi kinatosha unafikiri tuna chetu hapo? Kwisha kazi TZ!!

  Naungana na Mh. Lissu kwa yote aliyosema jana! Mbona kwa wenzetu wanafaidika na raslimali zao? Hatuwezi hata kwenda kujifunza Botswana jamani? Yaani Ole Naiko ole wako! hutufai bwana, upo hapo kulinda maslahi ya wachache mbumbumbu wewe!!
   
 14. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #14
  Dec 20, 2010
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mmoja wa wapokea Rushwa wa hatari anafaa awe wa kwanza kuozea Segerea. Ningekuwa Prezidenti wa nchi hii ningeanza naye na U-RichMonduli wake.....K.....mama yake
   
 15. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #15
  Dec 20, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo ole naiko alitakiwa achapwe viboko 6 asiwe anapotosha wtz,madini SIO RENEWABLE (i 'm a geologist)
   
 16. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #16
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,796
  Likes Received: 1,338
  Trophy Points: 280
  Hata mimi sikumwelewa kabisa kabisa kama alikuwa fiti kichwani.
  Lazima utaratibu udadilike, Tuanze na hawa hawa wanaojdai ndiyo wenye nchi.
  Wadai mikataba ni siri, kwa nini siri????:peep:
   
 17. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #17
  Dec 20, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,562
  Likes Received: 621
  Trophy Points: 280

  Una maana gani hapo ndg. kwa kuzingatia mahojiano ya hicho kipindi cha Hamza Kassongo?
   
 18. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #18
  Dec 20, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ole Naiko ni moja ya wasaliti na maadui wakubwa wa maendeleo ya nchi hii, siku utawala ukibadilika moja watu wa kufikiswa mahakamani kutubu na kuhukumiwa kwa waliyoyafanya wakiwa madarani ni huyu Ole Naiko
   
 19. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #19
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,796
  Likes Received: 1,338
  Trophy Points: 280
  Iwapo MUNGU huwa anaadhibu hadi Vizazi,
  Huyu naye siku tumeangusha serikali ya mafisadi vizazi vyake watatukoma.

  Wanafaidi wao na sisi ni watumishi wao! NO WAY.
   
 20. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #20
  Dec 20, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,617
  Likes Received: 2,998
  Trophy Points: 280
  HITIMISHO
  Kila kitu kilichofanywa na Serikali hasa kwa sasaivi chini ya Ngereja ni safi kabisa.
  Naomba watanzania turidhike na tunachopata na bado narudia kuwa biashra ya madini ni kama biashara nyingine yoyote.
  Mikataba tuliyoingia hatuwezi kubadilisha katu.


  Kama mtaalam mzoefu, anayeielewa vizuri sekta hii kiutendaji na falsafa yake, ninachoweza kusema ni kuwa hata kwa sheria mpya ya madini ya 2010, hakuna chochote ambacho kinaweza kutajwa kuwa ni maendeleo yaliyofanyika katika sekta hii. Kwanza Watanzania wanatakiwa kufahamu kuwa mabadiliko ya shera yaliyofanywa hayatahusu miradi ambayo ilianza wakati wa sheria ya zamani. Migodi kama ya Bulyanhulu, Geita, Buzwagi, Tulawaka, Lusu, North Mara, Tanzanite One - Arusha na Mwadui, haihusiki katika hayo mabadiliko.

  Hata kwa miradi mipya, ile ambayo itakuwa ni miradi ya kuanzia U$100 kupanda juu, haitalazimika kufuata sheria ya jumla ya madini kama inavyoainishwa bali kutakuwa na makubaliano maalum yatakayoainishwa katika MDA (Mining Development Agreement). Mabadiliko chini ya Ngereja hayajaleta chochote kwa Watanzania kuweza kujivunia, mengi ya yaliyoandikwa ni ya kufurahisha katika kuyasoma lakini hayatekelezeki.

  Tanzania kuweka kipengere kuwa corporate taxi italipwa baada ya makampuni hayo ya madini kuanza kupata faida, walipotea kabisa maana makampuni haya huendelea kuwekeza karibu wakati wote wa kipindi cha uhai wa mgodi. Na sasa wameingia kwenye mtego mwingine tena kwa serikali kuwa mwanahisa katika miradi yote mipya ya madini. Ukiwa mwanahisa unategemea kupata dividends (gawio) kampuni inapopata faida. Serikali isichojua ni kuwa ukitazama takwimu za makampuni mbalimbali ya madini Duniani hayatoi dividends kwa wanahisa wake, kwa hiyo wewe kama unangojea dividend utashangaa utakapogundua miaka inapita na hakuna unachopata. Wanahisa wa makampuni wa madini hufaidika na uuzwaji wa hisa zao pale ambapo thamani ya hisa hupanda ambayo mara nyingi husababishwa na new discoveries na kuongezeka kwa bei za madini ambayo kampuni inayachimba.

  Ole Naiko ni kati ya wengi waliopo serikali, huyu mmemtambua kwa kuwa ameongea.
   
Loading...