Hujaeleweka mkuu, naomba uweke sawa hasa pointi yako ya Tundu lisu kitaaluma. Kwa kuwa umejitambulisha kama mtaaluma
Naomba utueleweshe alipokosea
Wabeloya sijakuelewa una lenga nini??? Je Tundu Lissu pamoja na kuwa ni activits alichokuwa akisema kina logic au hakina??? Je Madini ni Renewables au non-renewable?? Je makampuni hayaachi mashimo na uchafuzi mwingine??? Je kama nchi 3 or 4% ya mapato tunayopata kama nchi ni halali??? Je suala la kusema kampuni zilipe cooperate tax baada ya kupata faida, je ni haki kwa nchi??? Je ni lini hizi kampuni kweli zitapata profit??? Ni nani anayekagua kujua kuwa kampuni zinapata faida au hasara ili zilipe Cooperate tax???. Mkataba mzuri ni ule utakao angalia masuala yote ya mahimu katika mkataba kama mapato kwa taifa, shares, uchafuzi wa mazingira na namna ya ku-mitagate matatizo hayo. Good project plan ni ile inayokuwa na mitigation plan wakati huohuo huku uchimbaji ukiendelea na sio kusubiri hadi mwisho wa project kama kampuni nyingi zinavyofanya.
Una maana gani hapo ndg. kwa kuzingatia mahojiano ya hicho kipindi cha Hamza Kassongo?
Ideas za activist wengi ziko against na wahandisi na kwa kifupi activist ni kama wanasema migodi isiwepo kabisa. Kwani swala la mazingira ni very relative term, na kwa Tanzania hatuna sheria, standard, za mazingira za hawa wazungu kuweza kuzifuata, kwa kifupi hazipo, kuna sheria za mazingira.
Swala la standard za mazingira linatakiwa liwe kwenye mikataba, si Lissu wala mapadre wala wachungaji wala nani wanaosema tuweke standard zetu, kila siku utasikia wanapiga kelele mazingira!!! yaani si activists wala viongozi wa serikali wala sisi raia wengi wanaojua issue za madini.
Kwa mfano soko la madini sasa hivi bado liko monopolised usitegemee utachimba madini yako na kuuza hovyo hovyo tu, bado wanatufanyia kama ilivyokuwa Pamba na mkonge vile. kuanzisha migodi lazima uchukue mikopo benki ya dunia (kitengo hiki kiko chini ya waingereza kwa sasa), bila kujua soko la madini yako litakuwa wapi, hupati mtaji/mkopo, bila kujua wataalamu gani watakuja kuchimba haupati mkopo/ bila kujua nani mchimbaji na huyo mtu anashirikiana vipi na WB hupati kitu! maana kuaanzisha mgodi sio kujenga machinga complex
Vita hii ya madini ni kubwa kiasi cha nikisikia Lissu anaongea na Ole Naiko nabaki nacheka kwani issue hii hata JK haiwezi kwa sasa! we need one crazy leader kulisawazisha hili swala liko international level! Canada mathalan bila Nickel yao kununuliwa na China wanafunga migodi!
Tukubali tu hatuji issue za madini na hii utaona wengi wetu tunasema ila kuna siri nyingi, haziwekwi wazi aidha kwa makusudi au kwa kutojua, kiasi cha kuwa wote kuonekana walewale
nimesisitiza sana kuwa tuangalie zaidi mikataba, maana hapa ndio mfupa wenyewe, ukisema tu uingize issue za mazingira, watakuwa na la kujitetea wakijitetea unaona kama vile mikataba iko safi, ukilisema tu wanaona wako nchini kihalali!!
Bulyhanhulu Bush anashare pale, na kila siku wanagawana viwanja Toronto Canada, ukiwa Toronto unaona watu wanavyoijua Tanzania kama vile wamezaliwa huku!
Point ya kusema activist ni kusema kuwa wengi wao hawajui lolote wala hawako wazi kusema status ya madini kidunia, soko likoje, uanzishwaji wake ukoje. tukijua hapo tutajua ukubwa wa tatizo lakini kutafuta mchawi hapa na hali tukijua hawawezi kufanya lolote basi ni bora tujikite kuwafukuza hawa CCM, na sio kusemea issue za renewable ou non renewable,hatujagusa hata robo ya robo robo ya roo ya robo ya madini nchi hii!! other issues are joking.....MIKATABA KWANZA MENGINE BAADAE! au tuache kabisa kuchimba, tuwe na akili za kufanya mengine ya maana zaidi.