Gwajimanization: Ni ngwala au mileage?

Gwajimanization: Ni ngwala au mileage?

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
464
Reaction score
687
Kufuatia Press conference ya Askofu May 24, 2025 kuhusu utekaji, utesaji na mauaji, ambapo alidai huenda kipo kikundi kinachotenda mambo haya kwa maslahi ya mwanasiasa fulani, kumekuwa na mijadala mingi kitaifa yenye hisia mchanganyiko, huku chama chake kikimwona kuwa aliyepotoka.

Pamoja na mambo mengine, watanzania wataukumbuka mkutano mkuu wa CCM, May 30, 2025 kwa kutupatia msamiati mpya town, "Gwajimanization." uliopewa maana kutokukitenga chama na "majuzuhu" kwani "Mcheza ngoma si yake ataharibu." Bila shaka, hili lilikuwa ni jawabu kwa press ya bishop.

Kama tuijuavyo hulka ya bishop, June 1, 2025 kanisani kwake, miongoni mwa mengi aliyoyazungumza, mojawapo lilikuwa ni kutoa maana mpya ya "Gwajimanization" kuwa ni “Ujasiri wa kusema ukweli bila woga, hata kama ukweli huo unawaumiza walioko madarakani.” Maana ambayo kwakweli ndiyo inayoonekana kukubalika zaidi kwa sasa huku mtaani.

Kwaupande mwingine, Msajili wa asasi za kiraia kaona isiwe tabu, June 1, 2025, sio tu kalifutia usajili kanisa la bishop, bali pia polisi walilizingira kanisa la bishop, ikiwa ni hatua muhimu ya anti gwajimanization campaign, sio tu kukitenga chama na "majuzuhu", bali pia kuwatenga watanzania na "majuzuhu" chini ya falsafa ya "mcheza ngoma si yake, ataharibu"

Hapo ndipo tulipofika sasa! Kama gwajimanization ilikuwa popularity project, bishop kapata mileage, ila kama ilikuwa ni serious political agenda, ninawasiwasi bishop kapigwa ngwala. Watanzania wanasubiri kuona atafanya nini? Je, atakinukisha? Au ataufyata. Kwa hali ilivyo lolote laweza kutokea.

Hata hivyo namkumbusha bishop, "The skillful General subdues the enemy without fighting" Art of War by Sun Tzu, "It is dangerous to be right when the government is wrong.” Voltaire, French Enlightenment thinker of 18th century na "Never outshine you Master" The 48 Laws of Power by Robert Greene
 
Itafahamika TU!
Lakini upstair pale hakuna kitu ni debe tupu ndio maana ni rahisi kwa kiongozi yoyote yule akiamua anam outshine tu!
 
Form four yake ilikuwaje kwani ndugu zangu?
 
Ukiona Wapumbavu 100 wanafanya Kitu cha Kipumbavu na wote wanaelewana

Wewe ambae unajua wanakosea usithubutu kurekebisha, Nyamaza kaa Kimya

Huwezi shindana na kundi la watu wengi waliokosea ukiamini utawashinda kwa sababu uko sahihi..

KAtika Hili kwa Kua Kashalianzisha Basi asimame nalo asipoe wala asitulie, akaze nati vizuri

Kama kweli ana nia ya kusaidia wananchi, Apige Press ndani kwa ndani kama OSAMA tena ingetakiwa ile PRESS angeifanyia nnje ya Nchi unapoanzisha fukuto la hivi hakikisha haupo nchini.

Kama yupo nchini lazima wamtie Mikononi..

Lakini : Kosa lake ni nini? Hata wamdake leo, Watampotezea muda tu ila Hamna Kesi hapo.

Wao waseme wanataka Kanisa Life walishushe ghorofa Chini
 
Back
Top Bottom