Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 122,418
- 95,830
Wakati unaomba ubunge ulituahidi mambo mengi sana.
Tulikuamini kwa kuwa wewe ni mchungaji yaani mtumishi wa Mungu hivyo hatukujua kama wewe utakuja kutugeuka.
Ulituahidi kutuletea boti za kuvulia samaki kwenye bahari yetu ya Hindi maana ndiyo ipo karibu na makazi yetu.
Ulituahidi kutuletea treni ya abiria kutoka Marekani kwa rafiki zako ili itusaidie masuala ya usafiri lakini hadi Leo hii tunaendelea kuhenyeka na daladala tu.
Mwishowe leo hii unakuja kutukimbiza mchaka mchaka bila kutekeleza ahadi zako za mwaka 2020?
Tumekuchoka mchungaji wa kondoo, Rudi kanisani mambo ya siasa waachie wenyewe.