mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,722
Kwanza niseme, siungi mkono cheti feki au mambo yoyote bandia maana ni kinyume na taratibu za nchi yetu tulizokubaliana ikithibitika pasipo shaka hatua kali zichukuliwe...
Ni maswali ninayojiuliza kila nikiangalia hotuba ya mtumishi Gwajima jana.
Kama Kigezo ni KUTUHUMIWA, Watumishi wa Mungu kuanzia Mwanzo hadi Ufunuo wanatuhumiwa. Yesu alituhumiwa kuwa Mlevi,ana Mapepo, Mzushi, Muongo....
Mtumishi anafundisha kisasi ni cha Mungu sio aliyetendwa baya, anaenda mbali kwa kutoa kisa cha NABOTH na Ahabu ambapo naboth alinyang'anywa shamba lakini kisasi akalipa Mungu kupitia mtu mwingine sio MTENDEWA BAYA. Hakuna popote alipotoa Mstari unaoonyesha Mungu kuhamasisha Mtendewa mabaya kulipa kisasi badala yake yesu anasema WAOMBEENI WANAOWAUDHI.
1/ Je! Mtumishi anapopindisha maandiko ili Kuhalalisha kulipa kisasi kwa kutuhumiwa (SIo Kuhukumiwa), hatuoni hapa anapaswa kurekebishwa ?
2/ Je mtu huyu akifanikiwa kuwa na Waumini zaidi ya Millioni, na akapandikiza mbegu hii ya kisasi kwamba ukipigwa moja(Tuhuma) wewe piga Visasi 10+, taifa litaishia wapi?
3/ Anatufundisha nini watanzania kwa kuhamasiha Visasi pale Tunapotuhumiwa(Tuhuma inaweza kuwa kweli au si kweli) na vyombo halali kisheria?
4/ Kama mamlaka (Zimewekwa na Mungu) zina haki ya kutuhumu yeyote, Kwa nini mtumishi usitumie jukwaa la kanisa kuwafundisha waumini ukweli huo?
5/ Je ikiwa wachungaji wote na mashehe wote wakahamasisha Visasi waumini wao kwa misingi ya kutuhumiwa huku wao wakiahidi kulipa mara 10+, Hii nchi nani atakayeishi?
Ushauri:
Badili mwenendo wa hotuba zako, Maneno yenye Sura za kisiasa Ita Press Conference kama unataka kutoa ushauri au ufafanuzi wa jambo lenye sura ya kisiasa, au kuisaidia serikali katika mapambano juu ya vyeti au vitu vyovyote visivyohalali:
Yesu kuonyesha umakini alimuuliza Petro mara tatu kama anampenda, Baada ya kuthibitisha akampa agizo LISHA KONDOO WANGU. KONDOO ALISHWI VISASI AU PERSONAL CONFLICTS BALI NENO Mtumishi. Pia wale ni wanafamilia wa Mungu, Mungu ndio baba yao wewe ni Muangalizi tu usijibinafsishie.
GWAJIMA LISHA KONDOO WA BWANA