Guts mnazitoa wapi wababa..??

Da Asia

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2011
Posts
731
Reaction score
819
Ulioa lakini it didnt work na mkeo mkaachana. Hali kadhalika na mimi the same. Tumekutana ukubwani kila mmoja na maisha yake na familia yake.
Tunaelewana maana binadamu company muhimu. Baada ya miezi 6 hivi tangu tujuane, baba anaona hapa kuna umuhimu wa kuhalalisha haya mahusiano, yaani mwende next step.
Katika muda wote huu wa miezi 6 ambayo mko pamoja, baba ndio anayekuja nyumbani, watoto wanamfahamu vizuri na ni waelewa. Mimi ambaye natakiwa niwe mama mtarajiwa wa watoto wake, siwajui hata kwa sura, na hata mwanamme anapoishi sipajui najua tu anakaa mtoni (sio kwake kikweli).
At least 5 days katika wiki lazima akitoka kazini apite nyumbani kwangu. we have super togather ndio aende kwake
Ajabu ni kwamba huyu mume mtarajiwa, sina hakika anawaza nini, hajawahi kufikiria hata siku moja kurudi japo na chungwa moja tu hata watoto wangu wampe credit kua uncle anafaa.
Nilijaribu kuongea nae kuhusu hili tatizo, akaja na mlolongo wa hadithi za kisanii, nikampa muda kama alivyoomba. Miezi mitatu imepita sioni mabadiliko.
Kumbuka kua quantity ya chakula inabidi tuongeze kwa zile siku ambazo baba mtarajiwa anakuja. kama kilo 5 za mchele tulikuwa tunatumia kwa wiki 2 sasa hivi ni wiki 1.
Hata dada atokee aseme mama luku imeisha, hawezi kujigusa. DSTV ikikatwa, amekauka, lakini ikilipiwa, ana remote yeye na ndio mchagua channel.
Kusifia utamu wa chakula ndio zake. Anashindwa kujua kua ili chakula kiwe kitamu kinahitaji vikorombwezo, ambavyo vinahitaji pesa.
Mtu huyu ana kazi nzuri, well paid, maana kuna siku nilifuma salary slip yake nikabaki mdomo wazi. Mshahara wake ni mara 3 ya wa kwangu, wakati mimi nilikua najiona nina mshaharaa mzuri, nilibaki hoi.
Sasa hivi nimemuamulia kua 6x6 nooooo under any circumtances. Tuna mwezi sasa. NImeshindwa mimi! Kwanini nikufikirie wewe iwapo wewe huwezi kunifikiria?
Hatuna social life, maana ni bahili anaona atatoa pesa tukitoka, sisi ni nyumbani, nyumbani na sisi. ukizungumzia going out, ataanza si tukae nyumbani tuangalie movie.
Mnapata wapi nguvu hata ya kutaka hiyo tamu? Kama inakunogea, gharamikia basi. Nikupe chakula cha bure na bado tamu ya bure!!! excuse me!!!!
Akina kaka na kina baba, mwenye tabia kama hii maana yake ni nini? maana kama ni ubahili wa huyu umepitiliza. hana aibu.
 
ULIMUULIZA KWA NINI ALIACHANA NA MKEWE?
Hiyo ndio sababu......
Halafu unapaswa umsome mwenzako toka kipindi cha dating...kabla ya kumkaribisha nyumbani......
Ya nini kuwa na mwanaume asiyejua majukumu?
Kwako kageuza hoteli aje ale na kulala, na kudoo bila kugharamia?
Shtuka dada, huyo mwanaume ukute hajaachana na mkewe.... Hujiulizi kwa nini hakupeleki kwake? Ndugu zake wawajua?

Anakutumia tu....
Wanawake mnapaswa kugundua haya na kujiengua mapema....
 
bidada amka toka usingizini,huyo baba inawezekana ana mke hawajatalikiana.. amekutamani kwa kuwa unamvutia na wala hana mpango wa kukuoa kama asemavyo. ktk hali ya kawaida angeshakupeleka kwake at least upajue maana we si mama watoto mtarajiwa..

muulize vizri kuna vitu havipo clear hapo..
 
Haloooooooooo!!!!! Nicheke Ninenepe!!!!!!Khaaaaaaaa!!!

Dada acha UCHOYO!!!! Wanaume wengi ndo walivyooooo!!!!!!!! NDOA 70% ZINAENDESHWA KWA HISANI NA UDHAMINI MZITO WA KINA DADA!! Usione watu wanangaa na PETE zao vidoleni. Wanaume wagumu kweli kutoa, HASWAA AKIJUA UWEZO WA KUTOA UNAO!!!!!!!!

As long as HE MAKES YOU HAPPY, HE DSNT CHEAT, HE LOVES YOU AND HE MAKES YOU HAPPY, Hayo mengine we just BULLSHIT!!! Ndio wanaume wengi walivo HADI UWAKABE KOO!!!!!

Umri umeenda usipoangalia U WILL END UP LONELY!!!!!! HAKUNA MWANAUME COMPLETE PACKAGE!!!!!!!! Wote wana m apungufu yao tu!!! KAMA HELA UNAYO JST BUY YOUR HAPPINESS!!! ITS WORTH IT!

Usiwe kauzu kama Mama Lara 1, pamoja na mshahara na biashara zake, Hata Kuku wakipitishwa ofisini LAZIMA AMPIGIE MUMEWE kuulizia achukue wangapi, na pesa yake atarudishiwa lini! Akigomewa ndo hatuli kuku hivooooo!!!!! Hata pesa ya chumvi akitoa lazima adai!!!!!! BE GENEROUS TO YOUR MAN BANA!!!!!!!!!
 
jivue gamba mamiie!utachunwa wewe hapo mpaka basi!halafu wanaume wa hivo hodari wa kutoa amri nyumbani kwa wapenzi wao yani mpka watoto wanakereka
sentensi kama hizi hazikauki midomoni mwao!
-DADA MBONA LEO HAMNA MATUNDA MEZAN?
-WE NANII HEBU LETA HIYPO REMOTE HAPA KUNA MOIRA SA HIZI
-HONEY HIVI UMELALA MPKA SA HIZI?
-WANAO WANA KELELE SANA WAKITOKA SHULE
-HUYU MSICHANA WAKO WA KAZI HANA ADABU
-HII GARI NI KAMA IMETEMEBE KILOMETA NYINGI VILE
-MAHARAGE KILA SIKU ?
 

lara 1, mwanaume lazima awajibike kwa nafasi yake hata kama mama anajiweza.. for me sioni shida kuhudumia familia as long as nina kiapato but kuna vitu ambavyo vinaonyesha kabisa hapo hamna long term commitment,
 

umeona eeh yaani wakuwa na visheria vya ajabu ajabu as if yy ndo anahudumia everything
 
Nimejuana nae about 5 years ago, by then alikua na mkewe. Pamoja na jitihada zake sikutaka kuanzisha uhusiano wowote nae kwa sababu ya yeye kua na mke.
alianzisha mawasiliano na mimi mwanzoni mwa mwaka huu na kuniambia kaachana na mkewe. sababu nimesikia za kwake tu mkewe sijamsikia hivyo unaweza kupata picha kua lazima ajipendelee.
nilihisi ananaitumia kiaiana, ila kabla sijamhukumu nikaona wababa mnipe mawazo yenu.
Nashukuru nitalifanyia kazi hili. Ila nina sababu nyingi zinazonishawishi kuwa kweli jana mke, ila ni bahili aliyepitiliza.


 
hahahhaaaa!!! Lara 1 umeniua, ila my dear sikubaliani na wewe.
biashara ya kulea baba zima na meno yake 32 siiwezi. aende zake njia nyeupe. nilishajisemea kua mwanamme ambaye hawezi kubadili maisha yangu sina haja nae, maana mimi kupelekwa kitandani sio issue, nawezi ishi bila hiyo kitu.
Sijawa mpweke that much kiasi cha kulea mwanamme. bora angekua hana kazi ningesema zigo langu, lakini employed and well paid..!!! Siwezi kwa kweli. Hata kama hakuna aliyekamilika huyu asojua wajibu wake kazidi.
Anyway, nashukuru kwa ushauri pia.


 
Asante snowhite, well said. kweli hapa nahisi ni kuchunwa kwenye maakuli.
lol, ngoja nivue gamba mapema kungali mchana, wakati bado naonekana.
thanks.

 
He is just using u, why keep and feed a cow while u can enjoy it 4free? Una2mika akikuchoka u wont see him so akil kumkichwa bibie!!
 
Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni hawatatikisika milele.Mimi kwa uelewa wangu sijui mdogo ama mkubwa that man has no future with you, anakutumia then after sometime akubwage.Kwa kuwa umeshalitambua hilo tokea mapema just leave him kabla hajakujeruhi nasema hivo maana unaweza ukamweka kichwani sana wakati kwa sasa maybe kuna wanaume wenye future zao wanakuaproach unawakatalia eti upo na mtu.Sasa siku ukithibitisha kuwa jamaa hayuko na wewe you will regret to the maximum. So the earlier the better changanya na za kwako hapo dada yangu
 
Kama tatizo ni ubahili tu basi you can put up with him. Namjua jamaa yangu mbahili kununua vitu vya kula na matumizi mengine nyumbani kwa mkewe lakini amejenga nyumba kibao mjini. Those houses are for the family not himself

Da Asia, hapo una bonge la resource ni wewe tu una papara. look here:
Kama jamaa liko fit kunako 6x6 piga tick ya 1
kama hana mambo ya cheating kwenye relationship piga tickya 2
kama ana ubahili ili afanye vitu vya uhakika kama kujenga nk piga tick ya 3

Mambo mengine ya vizawadi, kukupeleka kwake etc will fall into place. Mambo mengine madogomadogo utamfundisha wewe taratibu. Angalia mbali zaidi na tathmini kama he is worth your heart!! akili ku mkichwa bidada!! achana na papara za watoto umeshakua sasa ebo!!

Regards
 
Uwiii, nilikuwanae dizaini hii, nikashtuka, nikakata nikatupa kulee ptuuuu, hawanagamshipa wa aibu nyangau hao. Lol nakwambia muache mapema maana hata ukivumilia hana mpango na ww huyo. Na siku unamtema wala hataumia. U will witness this.
 
Hapa pagumu aisee..manake sipati picha jamaa anavokuvuruga for free!..Ila my advise would be to talk with the guy gently..wakati mwingine ni suala la uelewa tu ..ukute hata mshkaji wala sio bahiri kiviile..ila ni issue ya timing tu naiona hapa!
 
Dah! Watu mnavijembe humu jf baba wa watu akipita hapa mbona unatalaka leo,leo.Chamsingi achana naye huyo jamaa kuliko kuishi maisha ya kunung'unika kila kukicha,nafikiri malengo ya uhusiano wenu hayafanani.
 

Kwa heshima na upole, nikiwa nimepiga magoti wakati huu nikitype keyboard yangu, naomba nafasi ya kutuma maombi kwako lara1.Ndimi mtiiifu LINCOLINMTZA.
 

Daa Asia we jifanye NUNDA kama Mama Lara 1, ila sijaelewa HUYO MBABA PESA ANAYO HATOI AU HANAAAA? Wanaume wengi si watoaji haswaa hawa HANDSOME NA WASOMI!!!!!!!!! Utamucha huyo sawa ila utajikuta UNAMALIZA MABUCHA TU!!!!! Mimi kaka yangu pia alikuwa SI MTOAJI KABISAAAAA!!!!!! Mkewe ndo kuhudumia familia, ILA WALIISHI! Kwani pesa kitu gani banaaaa! We ukigoma kumuhudumia wenzio wanahudumia!!!!!

Fanya tafti kwa wanaume unaowajua wangapi ni WATOAJI??????
 
Dah! Watu mnavijembe humu jf baba wa watu akipita hapa mbona unatalaka leo,leo.Chamsingi achana naye huyo jamaa kuliko kuishi maisha ya kunung'unika kila kukicha,nafikiri malengo ya uhusiano wenu hayafanani.

Na wewe bakhili nini?
 
Kama mwenzio aliachwa na wewe hujui sababu ndugu, huoni pengine hiyo tabia ya ubahili huenda ndio ilianzisha timbwili kwenye ndoa yake ya awali!!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…