Gundua tabia ya mwanao pindi upo naye matembezi

Gundua tabia ya mwanao pindi upo naye matembezi

jeipm

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2018
Posts
500
Reaction score
826
Wazazi wenzangu natumai mko vyema na maisha yanaendelea kama kawaida

Mada hii natumai itakufungua macho kwa kubaini tabia za mwanao pindi utembeapo nae pamoja barabarani

1. Mtoto anapopendelea kutangulia mbele:
Hapa mtoto hutangulia mbele na kumuacha mzazi nyuma
-Mdadisi
-Anapenda kujifunza mambo mapya ila ni..
-Muoga

2. Mtoto anapopendelea kutembea pamoja na mzazi:
Hapa mtoto hutembea hatua kwa hatua na mzazi, hapa Mara nyingi mtoto hupenda kumshika mzazi vidole watembee wote
- Hajiamini
- Mtulivu ila
- Mwenye upendo

3.Mtoto anapopendelea kutembea peke yake na kubaki nyuma:
Hapa mtoto anapotembea ubaki nyuma na kumtanguliza mzazi mbele
- Mvivu ila mpambanaji
- Hujiamini
- Si muoga
- Huwa na kiburi

Tuambie mwanao yupo kundi gani hapo
 
Nilipokuwa mdogo mpaka ukijana wangu mama alikuwa ananikemea sana kubaki nyuma tutembeapo barabarani. Hii imeniathiri mpaka sasa hivi nikiwa na mtu natembea nae nakumbuka mama alivyokuwa akinikaripia basi utaona naongeza hatua niende sambamba na niliyenae au ni mzidi mbele.

Binafsi najiamini sana, sina woga napenda kusikiliza kwanza kabla sijaongea au labda niombwe kuchangia jambo pia napenda kusuruhisha au kuwa sehemu ya utatuzi wa tatizo.

Sipendi dharau hata kidogo ika niko very charming na nasocialize na watu easily sana.
Haya ni marafiki na ndugu zangu wananiambia ndivyo nilivyo
Sifa zingine reserved

Sasa sijui mama alishanitambua nitakuwaje😊😊
 
Mi mwanangu mara nyingi tunatembea sambamba,nkimwacha nyuma ujue kuna kitu hakijakaa Sawa either kuna kitu kataka sijampa so kanuna anabaki nyuma au hataki kwenda tunakoenda.Lakini mara nyingi habaki nyuma wala hatangulii mbele.Iyo no. mbili inamuhusu kabisa.Nifanyaje ili kajiamini ana kauoga flani hivi Kwa watu asiowazoea.Kuwa mtulivu naona ni poa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
3.na alifika kijiweni akagoma kumpa tano jamaa mmoja tena akiwa anacheka,sijui kisa nini.yaani alitoa kwa wengine kiroho safi kwa jamaa alikataa,hata kwa kurudia.ana 3.5yrs
 
Mkuu kuna scientific research kuhusu hii kitu?

Maana kama ni kwa uelewa wa kawaida kutangulia mbele ni alama ya ujasiri, uthubutu na sio woga kama kubaki nyuma,

Naongeza:
Ukiona kwenye michezo ya watoto ya kubebana mtoto anayebeba wenzake hyo ana nyota ya punda
 
Ukweli mtupu namba tatu wengiwao introvert hatupendi dharau,tunapenda amani,tunajiamini,tunaishi mazingira yoyote wacheshi wastarabu na tunamapenzi ya dhati.
 
3.na alifika kijiweni akagoma kumpa tano jamaa mmoja tena akiwa anacheka,sijui kisa nini.yaani alitoa kwa wengine kiroho safi kwa jamaa alikataa,hata kwa kurudia.ana 3.5yrs
Hyo jamaa anakumegea mkeo fungua macho we jamaa 😡 😡
 
Mtoto anaetangulia mbele ni mdadisi/mtu makini hataki kuyumbishwa na mipango yake.(nmeexperince)

Wapenda sanjari ni watu wenye upendo (nme experience) mtu nnae mpenda napenda tuwe sanjari , bi mkubwa wangu hapendi aisee mi napenda tukitembea nae tuwe sanjari, Babe [emoji873]

Sijawahi kubaki nyuma ila naonaga wanaobaki nyuma ni watu wavivu/wasio makini
unakuta mnatembea na mtu anasalimia kila mtu au kila anachokiona anakifata nakwazika mno.
 
Wangu ana 3.5 yrs,kila nikitoka naye nje ya nyumba hutangulia mbele tena huniacha kwa umbali mrefu sababu anakuwa kwenye mbio,kituo chake duka la mangi kuwahi pipi,hata kama sina safari ya dukani yeye anajua naenda dukani tu!!
 
Back
Top Bottom