Gundu...!

Gundu...!

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,454
Reaction score
872,085
Ni imani ya kikale isiyo na ithibati kisayansi kuwa
usiku wa kwenda vitani usilale na mwanamke
Siku ya kwenda kuwinda kurina au kuvua usilale na mwanamke
Kwamba kuna wanawake mlango wa 8 ukimuoa kila kitu kinapukutika
Kwamba ukipata balaa lolote unaulizwa kwani jana ulilala nanani ?
Kwamba mashetani majini na mizimu hupendelea kuweka makazi yao milini mwa wanawake hivyo kuwafanya wawe na nuksi au gundu
Nikitafakari haya yote na mengine pia naona mwanamke anabebeshwa mizigo mingi na mizito asiyostahili kubeba
 
Voice of Mtwara ni sawa ni imani. tu lakini kwanini imkandamize mwanamke zaidi ?
 
Ni imani ya kikale isiyo na ithibati kisayansi kuwa
usiku wa kwenda vitani usilale na mwanamke
Siku ya kwenda kuwinda kurina au kuvua usilale na mwanamke

Kwamba kuna wanawake mlango wa 8 ukimuoa kila kitu kinapukutika
Kwamba ukipata balaa lolote unaulizwa kwani jana ulilala nanani ?
Kwamba mashetani majini na mizimu hupendelea kuweka makazi yao milini mwa wanawake hivyo kuwafanya wawe na nuksi au gundu
Nikitafakari haya yote na mengine pia naona mwanamke anabebeshwa mizigo mingi na mizito asiyostahili kubeba

Jamani hata haya nayo unahitaji notes? Its obvious ukilala na mwanamke kabla ya mambo haya muhimu utakuwa umepungukiwa nguvu kidogo. Hata wachezaji wakishaweka kambi ya mashindano fulani huwa wanazuiwa sex kwa sababu nguvu zao zinahitajika sana. Watu wa zamani walijua hizo habari ndo maana wakawa wanasema ni gundu ili wanaume wasifanye hivyo
 
Imani ziko za kila aina, kuna wengine wanaamini unaweza kuigeuzia mimba mgongoni kwa muda unaotaka, hata miaka 10. Imani ni imani tu.

Wakiona mwanmke mzigo, oa mwanamme, thanks to haki za makundi madogo.
 
Kweli wanaonewa sana kwa hili

Kama mlienda kucheza mpira mkifungwa, kelele zinaanza kuna wengine walilala na wanawake wenye gundu ndio maana tumepoteza

Biashara zisipotoka na mengine mengi

Hapa nakubaliana na mkuu mleta mada
 
umewahi kujiuliza kuwa kwann wanawake ndio wanakumbwa na ugonjwa wa mashetan?? Na jaribu kufuatilia chanzo cha dhambi ya Adam na Hawa/Eva
 
umewahi kujiuliza kuwa kwann wanawake ndio wanakumbwa na ugonjwa wa mashetan?? Na jaribu kufuatilia chanzo cha dhambi ya Adam na Hawa/Eva
Kula tunda la mti wa kati ambapo hawa/eva alimshawishi adamu kama niko sawa
 
ukilala na mwanamke utatumia nguvu ...kwa hiyo hutoweza kufanya kazi ngumu vzuri kama ni kucheza mpira,kuwinda,kulima,vitani n.k
nadhan ndo maana wazee wakaamua kusema ni gundu ili kuepusha vijana.
 
ukilala na mwanamke utatumia nguvu ...kwa hiyo hutoweza kufanya kazi ngumu vzuri kama ni kucheza mpira,kuwinda,kulima,vitani n.k
nadhan ndo maana wazee wakaamua kusema ni gundu ili kuepusha vijana.
Hata iwe hakuna aliye lala na mwanamke mkifungwa mara nyingi lawama zinakua hizo

Lawama zinaelekezwa kwa wanawake kumbe kiukweli hakuna hata mmoja aliyelala na mwanamke usiku wa kuamkia siku ya mechi
 
Hata iwe hakuna aliye lala na mwanamke mkifungwa mara nyingi lawama zinakua hizo

Lawama zinaelekezwa kwa wanawake kumbe kiukweli hakuna hata mmoja aliyelala na mwanamke usiku wa kuamkia siku ya mechi

ha ha ha wapo wanaochepuka fasta..

kwanini lawama kwa mwanamke...
 
ha ha ha wapo wanaochepuka fasta..

kwanini lawama kwa mwanamke...
sheria kandamizi na mfumo dume usishangae hata mtoto akifanya kosa anaambiwa kachukua akili za mamaake...!!!
 
ha ha ha wapo wanaochepuka fasta..

kwanini lawama kwa mwanamke...
Nakupa mfano hai

Kuna siku tulienda kupiga gemu mkoa tumelala kambini hakuna mazingira ya kutoka wala ke yoyote karibu na maeneo

Tulipopiga gemu jioni tulifungwa

Basi wee lawama zikaanza wengine wana magundu yao hata wakikaa wiki ngapi hayatoki

Tatizo mnatembea na wanawake wenye gundu
 
Maskini wanawake.....!maskini wanangu....!
 
Kula tunda la mti wa kati ambapo hawa/eva alimshawishi adamu kama niko sawa

tangu zaman iman ya babu na wazee wetu waliamin kuwa mwanamke ni kiumbe dhaifu na hvyo ni rahsi kushawishka au hata kuangukia ktk maovu ndio maana hata mashetan huwaingia zaidi wanawake, hata ng'ombe hamuogopi mwanamke.... Kwahyo ile mikos ya mashetan inaweza kupitia kwa mwanamke kumwingia mwanamme...... Ni mtazamo tu lakin
 
NDG ZANGUNI MAGUNDU YAPO TUACHE KUZUNGUKA MBUYU WAKO WATU NI NUKSI KWELI KWELI WANAWAKE KWA WANAUME,UKIMGUSA TU UTAJUTA KUZALIWA AJALI SOMETIMES KIBARUA KWISHEYI,BUT WAKO AMBAO UKIGUSA MBONA UTACHEKA! KESHO CHEO KINAPANDA,BIASHARA ILIYOGOMA KWA MUDA MREFU HIYO INAKWENDA TUBISHE TUJIFANYE TUNAAKILI YA KISAIKOLOJIA BUT hayo yapo TENA UNAWEZA KUTANA NA MWENYE GUNDU BAYA KABISA ukajifia kimya~kimya kisailence!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom