Gumzo la IDD: ‘Covid-19 added you’

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,845
Leo ni IDD ya Ansur - Sunna .... Na BAKWATA
Happy IDD El-Fitri Waislam safi waliotimiza funga yao kwa hakika.. Allah awape wepesi na barka tele
Happy IDD wale walio sindikiza wafungaji
Nawatakia Idd njema makobe wote

Legacy ya mzee wa Msoga inaishi kupitia matamshi yake.. Yule Mzee wa pale Chalinze karibu na CHALINZE MZEE... Sio mbali sana na Msata kilingeni.. Yaani naweza kusema ni majirani kabisa japo hatuwezi kuombana munyu... Sasa usemi wa.. ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZA KWAKO... Unapata umaarufu wake.. Ukisikia mahitaji ya nyakati ndio haya...

Wewe ni mtumiaji mzuri wa WhatsApp na kwa vyovyote umeshawahi kukutana na hii adha ya kuungwa kwenye kundi la WhatsApp bila ridhaa yako.. Kundi ambalo huna hata kaliba nalo.. Achilia mbali maudhui yake... Tena unaungwa na mtu usiyemfahamu kabisa..

Inaingia msg.. Pengine kuna msg muhimu ya mchongo au shekeli ulikuwa unasubiria kwa hamu kubwa.. Mara paaap! Unachokiona huamini macho yako...

Shenazi added you (group la wadangaji)
Shilawadu added you (group la wambea wa kiumeni)
Aunt Abuu added you (group la mashoga)
Half ray added you (group la kijani)
Jr added you (group la walozi)....
Juliana added you (group la wasaliti)
LMb7 added you (group la praise n worship)
Jo added you (group la great sinkers)
Freemason added you (group la wapigaji)

Unasonya bonge la msonyo kwakuwa waliomo wote humjui hata mmoja na chats zao zote hakuna inayokuvutia hata moja.. Usiumize kichwa.. Usiumie moyo.. WhatsApp wamekuja na tiba bora kwenye hili... Sasa kuna option ya kupuuza kuungwa kwenye ma group bila ridhaa yako.. Na hiyo option iko kwenye SETTINGS.. Hakuna kulalamika tena...!!!

COVID-19 Added you.. Loh unaonaje unapopata huu ujumbe? Kwamba sasa wewe ni mpendwa kwenye group la Corona.. Unaweza kutoka kajasho fulani kembamba kabaridi sana....

Huna haja ya kupaniki... Una option ya ku block COVID19 asikuunge kwenye group lake... Maudhui yake si mazuri na hayana nia njema kabisa na wanachama wake...

Za kuambiwa changanya na za kwako...
Nawa mikono kila wakati
Kaa mbali na wengine
Epuka misongamano
Vaa barakoa halisi
Fuata Kanuni za afya na miongozo ya Wataalam kwenye kujikinga na kukinga wengine... Usiwasikilize wanasiasa.. Wana ajenda zao... Siasa sio taaluma.. Wasikilize wenye taaluma zao..
Kwenye siasa hakuna weledi wala miongozo.. Kwenye taaluma kuna weledi kuna miongozo kuna kanuni... Fuata hizi.. Utasaidika na kuokoa wengi pamoja na wewe mwenyewe....

Za kuambiwa ukichanganya na za kwako.. Utashangaa tu kuona kwenye ma group
COVID-19 LEFT
COVID-19 LEFT
COVID-19 LEFT
COVID-19 LEFT
COVID-19 LEFT
NA HUO NDIO UTAKUWA USHINDI WETU SOTE...!!!

INSHALLAH NA EID MUBARAK!!!!!!


Jr
 
Za kuambiwa... SHIKAMOO Mzee wa Msoga...
IMG-20200523-WA0026.jpg


Jr
 
Wanasiasa ni viumbe wa hatari sana. Hatutakiwi kuwaamini kwa chochote, kwa lolote! maana hawana cha kupoteza zaidi ya kupambania tu umaarufu wa kisiasa na sifa mbele ta hadhara.

Hakika tuendelee kuchukua tahadhali na pia kujikinga dhidi ya hili janga la Corona. Kwa hili hakuna namna, ni lazima tutumie falsafa ya Mzee wa Msoga.
 
Wanasiasa ni viumbe wa hatari sana. Hatutakiwi kuwaamini kwa chochote, kwa lolote! maana hawana cha kupoteza zaidi ya kupambania tu umaarufu wa kisiasa na sifa mbele ta hadhara.

Hakika tuendelee kuchukua tahadhali na pia kujikinga dhidi ya hili janga la Corona. Kwa hili hakuna namna, ni lazima tutumie falsafa ya Mzee wa Msoga.
COVID-19 left.... COVID-19 unable to add you...

Jr
 
Back
Top Bottom