Guinness a.k.a Vega, Muboroboro. Ni bia imported foreign extra yenye kilevi Cha 6.5v/v
Ni bia nimeanza kutumia miaka Saba iliyopita hakika Ni bia iliyopikwa ikachemka na kutokota ikapoa ikachujwa kwa umakin wa Hali ya juu karbu tupate.
Wale wadau nawaonaga wanaomba Ushauri Ni jinsi gani wanaweza kuacha pombe Ni nawasii wasiache pombe chonde chonde Sasa unataka kuacha pombe ili unywe nn? Ukiona mtu ana hizi kauli za nataka kuacha pombe Ni Kuna mawili
Moja- anakunywa tapu tapu wanzuki , banana ,gwagwa, rubisi,pombe za kupima ,kitokosi,shujaa nk hzi pombe ukiwa na buku mbili lazima ulewe na unaweza fanya utopolo kesho yake majuto.
Pili - wapenda sifa una ka laki unataka kwenda sehem wanauza bia moja buku nne haraka haraka ukinywa bia kumi mfukoni umebaki na 60 Apo hujapanda Uber,bolt apa ukiendelea kuwepo utapanda boda boda utakula upepo mpka ukome mpka umefika pombe imeisha na kula hujala unapata vichomi Hadi vya matako.
Watu wanaoteseka kwenye pombe Ni wale unajikiuta umezungukwa na wapambe all bills on you ,wapenda madem classic Dem anaagiza kinywaji Cha elfu 40 mapigo ya moyo Yana Anza kwenda zigzag ...wapenda sifa mtaendelea kuumia
ili uendelee kupata lager zako bila majuto zingatia yafuatayo
- Uwe na rafiki mmja au wawili ambao Ni nipe nikupe or let's share this bill
- Kunywa pombe peke yako kwenye bar ambazo Ni nzuri lakin wanauza beer au kinywaji chochote kwa reasonable price kula bia zako safi kabisa afu nenda home kapambane na chaga zako
- Nunua vimiminika weka ndani uwe u akunywa nyumbani kwako
- ikitokea umekutana na mtu bar nae Ni mtumiaji hii Ni emergency mnunulie bia moja tu afu kausha akianza kununua yeye tabasam moyoni we zipige ukitosheka potea na usiage mtu.
- ukipata Dem mtumiaji ...wewe ndo final say wa ku suggest sehem ya kwenda sio Dem anachugua ..labda Kama atalipa bill Apo bro kua mpole fata nyuki .. unless otherwise uswe fara
Drink responsibly
Karbu Guinness Niko chocho tulivu.