GUINEA: Kila ukifiwa unakatwa kidole kimoja

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,077
17,207
Jamii nyingi hutofautiana jinsi wanavyomkaribisha mtoto wao humu Duniani na pia jinsi wanavyomuaga anayetangulia mbele ya haki.Katika jamii nyingi duniani, kuna tamaduni tofauti za kuomboleza, kuadhimisha, na kuwazika wapendwa wao.Jamii moja inayoonesha mbinu za kipekee za kuomboleza na ya kupigiwa mfano ni ile ya Dani, iliyoko Magharibi mwa Papua New Guinea.

Tabaka hilo huwa linaomboleza wapendwa wao kwa kujikata vidole vyao, kama dhihirisho ya kuwa kweli ulikuwa unampenda yule aliyeaga dunia! Tamaduni hiyo ambayo inaonekana ya kutisha imekita mizizi sana miongoni mwao na si ajabu unapotembeatembea kijijini utashangaa kuwaona watu waliokatwa viganja vyao vikaisha.Hilo likiwa dhirisho kuwa amefiwa na wapendwa wake. Wakaazi hao wa bonde la Baliem wamekuwa wakifuata tamaduni hiyo kwa miaka na mikaka na hivyo sio jambo ambalo linawezatoweka kwa haraka.

Mtindo huu hufanyika kwa yeyote ule mwenye uhusiano na marehemu, wakiwajumuisha wazee, wanawake na hata watoto.Utamaduni huo huanza kwa ibada kwa minajili ya kufukuza mapepo ya marehemu, na pia kama njia ya
kutumia maumivu ya kimwili kuonyesha huzini na mateso ya kufiwa.Vidole vyao hufungwa kwa kamba, kisha kukatwa na shoka, vipande vilivyokatwa huchomwa kwa moto na jivu huhifadhiwa.
 
Hiyo jamii wote watakua walemavu
Ile boyfriend wako anakuchkua muende kwao kuna msiba, kufika unakutana na mila hizo alafu nawewe ndo mkewe wanakwambia wakukate ,,,,,,
 
Hiyo jamii wote watakua walemavu
1468766785344.jpg
1468766794161.jpg
1468766800597.jpg
1468766804023.jpg
1468766807757.jpg

Kama hao
 
Ile boyfriend wako anakuchkua muende kwao kuna msiba, kufika unakutana na mila hizo alafu nawewe ndo mkewe wanakwambia wakukate ,,,,,,


Watakata dyudyu zao! mimi sifanyi ujinga huo
 
Mmmmmh! sasa kwa wale wenye nyota za kufiwa si wanakatwa mpaka vyote 20 vinaisha?
Nawaza kwamfano ndugu zako ndo wamepata ajali safarini wakafariki wote, Watakukata vyote kwa mkupuoo au????
 
Ila n nzr hasa kwa wachawi... Maana mchawi haez kumuua ndg yake vngnevo atakatwa vdole
 
Back
Top Bottom