verify
JF-Expert Member
- Dec 31, 2024
- 1,313
- 3,164
Tarehe 18 Agosti 2026 ilianza kama siku nyingine kwenye safari ya Rockstar kuelekea release ya Grand Theft Auto VI, lakini ikageuka kuwa nightmare. Mtu au kundi linalotumia jina CyberLeek lilianza kusambaza gameplay footage, screenshots na taarifa kutoka kwenye build ya GTA 6, ikiwa ni pamoja na footage yenye Jason, maeneo ya Leonida na vipengele ambavyo Rockstar ilikuwa bado haijavifichua rasmi. Kilichofanya leak hii iwe nzito zaidi ni timing yake ilitokea siku tisa tu kabla ya official Extended Look ambayo Rockstar ilikuwa imeipanga, hivyo mpango wa kampuni wa ku-control kile ambacho mashabiki wangeona na muda wa kukiona ulivurugwa ghafla. Baadhi ya taarifa zinaonyesha CyberLeek alidai kuwa alikuwa akifanya hivyo kama protest dhidi ya digital pre-orders na masuala ya ownership ya games, huku pia akihusisha leaks na cryptocurrency yake. Hata hivyo, utambulisho halisi na namna alivyopata access kwenye material bado haujawekwa wazi kikamilifu.
Lakini kilichofuata ndicho kilifanya hii isiwe leak ya kawaida. Take Two Interactive, kampuni mama ya Rockstar, ilianza kutumia DMCA takedowns na hata kuchukua hatua za kisheria kutafuta chanzo cha leaks. Mnamo 20 Agosti 2026, Take-Two iliwasilisha maombi ya subpoenas yanayolenga Microsoft na Discord ili kusaidia kutambua watu waliohusishwa na kusambaza material hayo. Wakati huo huo, CyberLeek aliendelea kutoa footage mpya, na baadhi yake zilionyesha mechanics ambazo mashabiki hawakuwa wameziona kabla ikiwemo interaction za magari, refuelling na response ya polisi. Cha kushangaza zaidi, ripoti zilisema footage hiyo ilionekana kutoka kwenye build halisi kiasi kwamba CyberLeek aliweza kuonyesha gameplay ikiwa imekamilika vya kutosha kuashiria access ya kiwango cha juu, ingawa chanzo halisi cha access bado hakijathibitishwa rasmi.
Na hapo ndipo heartbreak ya Rockstar ilipoingia. Baada ya kukaa kimya huku footage ikiendelea kusambaa, Rockstar hatimaye ilitoa statement tarehe 26 Agosti 2026, ikieleza kwamba kuona kazi ya timu ikitolewa kwa namna hii kabla ya wakati ilikuwa “heartbreaking” kwa watu waliotumia miaka kuijenga. Hii si kuhusu kampuni kupoteza surprise pekee ni kuhusu developers kuona kazi yao ya miaka ikikatwa vipande vipande na kuhukumiwa kabla haijakamilika. Rockstar iliomba mashabiki wasiharibu experience kwa spoilers na ikasisitiza kwamba GTA 6 iko “nearly there.” Pamoja na vurugu zote, Rockstar haijasogeza tena tarehe iliyotangazwa ya release 19 Novemba 2026. Kwa upande mwingine, kampuni bado inaendelea na official reveal yake ya 27 Agosti 2026 ikimaanisha kwamba CyberLeek aliweza kuvuruga pazia, lakini bado hajachukua stage yote.