GSM wametoa ufafanuzi kuhusu pesa yao juu ya mchakato wa mabadiliko ya Yanga, je watafaidika vipi?

RAKI BIG

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
394
456
VIWANJANI LEO

"Sisi kazi yetu kubwa ni kuhakikisha klabu yetu inaweza kusimama kwa miguu yake miwili, hilo nataka ufahamu na watu wote wafahamu.

"Hatuna nia ya kufanya chochote, transformation yoyote inapofanyika inawahusu wanachama zaidi, ndio maana kipengele cha kwanza ambacho ni muhimu kuliko vyote ni kitu kinachoitwa fan engagement.

"Ni mahusiano kati ya wanachama na klabu yao, hakuna kipengele kinachozungumzia uwekezaji au ununuaji wa klabu,
"Klabu yetu inapaswa kujihusisha asilimia mia na mashabiki wake, ndio maana kama unakumbuka slogan yetu sisi Wanayanga ni kwamba sisi wenyewe wapenzi na wanachama ndio wawekezaji wa kwanza.

"Kwa hiyo tunaenda kutengeneza mazingira ambayo mwanachama atajihusisha na klabu yake kwa asilimia mia moja ili zile gharama za uendeshaji mwanachama aweze kuzichangia kupitia ada ya uanachama.

"Hakuna mahali pameandikwa hiyo pesa ni deni au tumeiazima klabu ya Yanga kufanya mabadiliko, tukumbuke mabadiliko ni malengo ya Mwenyekiti wa Yanga kipindi anagombea

"Gharama hizi ambazo tunazilipa tunafanya kwa nia njema." - Eng Hersi Said, mkurugenzi wa uwekezaji GSM
 
Anza kujua Mo ananufaika vipi na Simba. Itakupa picha jinsi GSM watavyonuifaika na Yanga.

Haa!!!,,,GSM wanajitolea tu ili wapate swawabu kwa Allah!!!
Shida ya hawa wawekezaji uchwara hawanyooki.Janja janja sana
 
Hivi vilabu 2 , tako moja fc na Dar Young Africans. Ni vilabu vilivyochezewa sana na malofa ambao walikuja kuchuma na kunufaisha matumbo yao.

Wanasiasa ambao, walifanikisha malengo yao ya kisiasa , wafanyabiashara ambao nao malengo yao yalitimia na kuviacha vilabu hivi vikizidi kudidimia siku hata siku.

Ukombozi ni kuwapata matajiri wenye upendo na nia njema , kuwaongoza na kuwasimamia katika hali na mali wapenzi , mashabiki na wanachama waweze kuungana pamoja na kuviendesha vilabu hivi kwa usasa na weledi pamoja na kuvichangia katika mfumo sahihi.

GSM anachokifanya ndicho haswaa , Matajiri wenye mapenzi mema wanapaswa kuvisaidia vilabu hivi, mwisho wa siku wao pamoja na vilabu na wapenzi , mashabiki na wanachama wakifurahi pamoja na kwa haki.

Uwekezaji mwingine ni malengo ya kuwanufaisha wachache na kuimiliki timu toka kwa masikini ili utajiri wako ukue , kw kisingizio nasajili, nalipa mishahara nyie kaI yenu kushangilia.
 
Back
Top Bottom