Great thinkers: Njooni tuumize kichwa tunusuru watu wa mtaa

Kuumiza kichwa kwaajili ya mtu/watu ambao hawajaumiza vichwa vyao nikupoteza nguvu na wakati wangu binafsi..

Vujana wanashinda kuzungumzia mipira, beting na majungu, wakike wamejikita kwenye umbea mitandaoni na kujipiga mapicha kwenye social media..

Hawa unaanzaje kuwasaidia,..?!
 
Nina mazao ya kilimo, soko hakuna. Mwaka huu na mwaka jana, watu wanalima na kuvuna lakini soko bovu, unaishia kuuza kwa hasara au huwezi kuuza kabisa! Vijana wakikutana na hali kama hiyo unategemea nini?

Heshima kwako kama kijana unaetumia akili yako kujisimania..
Uwekezaji wowote unachangamoto hakuna jepesi hayo mawazo ondoa..
Kilichobaki nikujikita kuangalia ni namnagani unaweza kubadili mtazamo wa soko..

Mfano unaweza badili mbinu ukawa unazalisha mahindi kwajili ya mbegu na sio chakula. Lamsingi umeshanza safari nilazma ufike..kulalamika nikukata tamaa
 
Mkuu, hapo kwenye Serikali kufungua viwanda it's not like you think. Huko nyuma Serikali Iliwahi kuwaza km unavyowaza wewe sasahivi ikataifisha viwanda karibia vyote vilivyo chini ya watu binafsi ikaanza kuviendesha yenyewe lakini ilifeli vibaya sana....

Ikawa bora hata kipindi viwanda vinamilikiwa na watu binafsi sera ya Utaifishaji wa vwanda ilikua ni Mzigo mzito ambao serikali ilishindwa kuubeba, wakapata funzo....

Kwa sasa serikali inachofanya ni sio kujenga yenyewe viwanda ama kuviendesha, bali kuhimiza watu binafsi wawekeze kwenye industry hiyo huku yenyewe ikiweka mazingira bora kwa wao kufanya hivo

Sera ya viwanda ya JPM ni ngumu mno kutekelezeka maana kwa sera hiyo serikali inategemea watu binafsi ndio wafungue viwanda huku yenyewe ikifaidika kutokana na Kodi lkn pia wananchi wake kuajiriwa kitu ambacho ni kigumu kwa sasa kwa kuwa mazingira ya biashara YAMEKUWA magumu mno

Sera ya kilimo mfano, Mtu anaweza akawekeza shambani akalima hata eka 100 za mahindi akivuna mf. gunia 2000 akataka kuuza soko la ndani hakuna wa kununua zote hizo maana sekta ya viwanda (manufacturing) bado haieleweki, sasa soko kwakua ni dogo akataka kuuza nje nako ni shida Mipaka inafungwa matokeo yake ndio unaona mahindi yanazagaa tu bei nayo inashuka mpk 500/kilo bisnes as Usual

Tunarudi kule kule Mazingira hayajawa rafiki kwa sekta kuoperate smoothly
Nimelima mwaka jana yamenikuta hayo.Unatumia gharama kubwa hata hairudi.Serikali inafunga mipaka shida tupu.Sera za uchumi mbovu sana .
 
Heshima kwako kama kijana unaetumia akili yako kujisimania..
Uwekezaji wowote unachangamoto hakuna jepesi hayo mawazo ondoa..
Kilichobaki nikujikita kuangalia ni namnagani unaweza kubadili mtazamo wa soko..

Mfano unaweza badili mbinu ukawa unazalisha mahindi kwajili ya mbegu na sio chakula. Lamsingi umeshanza safari nilazma ufike..kulalamika nikukata tamaa

Kwa hiyo wakulima wote wa mazao ambayo hawawezi kuyauza wafanye kama ulivyoshauri?
 
Miii hua sielewagi hii policy ya tz. Ya viwanda, wakati tulipaswa kwanza kuwekeza serious kwenye kilimo..then tuhamie kwenye viwanda.
Alafu kipindi cha mwl. Nyerere tulikuwa tuna viwanda vingi tuu..lakini nowdays vimekufa
Sasa hivi serekali imewekeza kwenye ndege, shingler na SGR, tu

Sijasikia kiwanda hata kimoja serekali ikijinasibu kukijenga kwa ajili ya kuongeza wigo wa ajira kwa raia wake
 
Nimekuelewa mkuu...ila serikali inatakiwa itengeneze mazingira na sera nzuri za kuwavutia wawekezaji. Wee angalia mahusiano yaliyopo kati ya wafanyabiashara wakubwa na serikali yalivyo mabaya. Hili nalo ni doa kwa taifa letu
Ni kweli, wakati mwingine mpaka unacheka tu yaani watu hao hao ambao serikali inategemea wawekeze ndo hao inaowafanyia visa mfano mdogo cheki Manji walivyomnyong'onyeza sasa cjui huwa hawafikirii hawa watu
 
Mimi hata uwezo wangu wa kufikiri naona umepungua toka nimalize chuo nipo kitaa deal zote nazopiga zinajamba watawala wanafurahia tunaishi hata wakitoa fursa mpaka ikufikie wameshawapa watoto wao na marafiki zao solution ni kuendelea kuvumilia kuwa watanzania tusubiri kipindi cha pili labda nitasaidiwa na upepo
Ni hayo tu kama hujitumi piga mihayo tu
Unajituma vipi wakati fursa zimezibwa kila upande mkuu kiukweli watu wanaishi kama mashetani
 
Nina mazao ya kilimo, soko hakuna. Mwaka huu na mwaka jana, watu wanalima na kuvuna lakini soko bovu, unaishia kuuza kwa hasara au huwezi kuuza kabisa! Vijana wakikutana na hali kama hiyo unategemea nini?

Mkuu ndio maana nikaishauri serikalii Iinvest,wenyewe kutumia wataalamu wataonyesha nini kinahitajika katika soko na what amount.....
 
Tatizo lingine vijana wengi na tabia ya kukaa mjini sijui Daresalama, chuga, rokusite na wengi mnadaiwa na serikali coz elimu ya juu.

Fulsa zipo ila mnataka mshikwe mkono, mfano mnashindwa kukusanyika vijana kumi mkaanza kuunda mifuko mbadala na kuanza kuuza!

Mchina akimwaga kontena 100 za mifuko mbadala mnaanzisha uzi hapa jf mmh..!!
 
Back
Top Bottom