Great thinkers: Njooni tuumize kichwa tunusuru watu wa mtaa

kombaME

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
2,115
2,809
Hali ni mbaya mtaani, watu wanahangaika sana kufanya hiki na kile bado mambo hayaendi, watu wananyenyekea ajira zao na maboss wao kipindi hiki hadi hatari, Ajira hamna, Soko la kuuza bidhaa mtaani linazidi kushuka siku hadi siku, hali ni mbaya mno.

Vijana wengi wanaingia kwenye msongo wa mawazo kwasababu ya ugumu wa maisha, kutoboa kwenye life imekuwa ngumu mno siku hizi. Unapiga kazi tembo unapata kipato sisimizi, Hii inawafanya vijana wengi wa kike na kiume kukata tamaa, mwanga wa mafanikio unazid kufifia kwao, viongozi wenye dhamana nao Sioni kama wana maarifa kuwatoa vijana kwenye mkwamo huu zaidi ya maneno yale yake ya "MJIAJIRI NA ACHENI KUKAA VIJIWENI".

Mazingira hayamuwezishi kijana kupiga hatua mbele, akifungua kibiashara chake anakutana na kodi mfululizo hadi mtaji unakata, akisema afanye kiujanja ujanja ndo kabisa hatoboi. Serikali ni kama haijadhamiria kumkomboa mtu wa chini, Sioni strategies zozote kumkomboa masikini zaidi ya maneno ambayo mi naweza kuziita porojo.

Mtaa umekuwa Sumu kwa vijana.. unaua vijana kimya kimya, kutokana na hali ngumu inawasababisha vijana kutafuta kipato kwa njia nyingne isiyo halali.. wizi, utapeli, michezo ya bahati nasibu imekuwa mbadala wa kutafuta unafuu wa maisha kwa vijana..

Kifupi hali ni mbaya..

GREAT THINKERS HEBU TUJE TUSHAURI JINSI YA KUTOKA HAPA...
 
Usiumize kichwa kutafuta hela

Fikiria kuhusu matatizo yanayoizunguka jamii, then umiza kichwa namna ya ku solve matatizo hayo

Then kwa ku solve matatizo yao ndio watakua wanakupa hela

Watu kama waliogundua sijui M pesa, Uber, facebook, Youtube ambao ni bilionea sasa hivi walokuwa wakifiria namna ya ku solve matatizo na kurahisisha maisha
 
Tatizo la vijana Wa sasa nnataka uajiriwe Leo ulipwe mamilioni.

MTU umeanza business Leo kesho unataka ushindane kula bata nakina Dick sound nakina Dayamond

Hebu anzeni kuchange mindset zenu kwanza
 
Kilimo ni utajiri mkubwa sana haujui tu.

Nitafute mwezi wa 11 kama utakuwa tayari nikupe hekali mbili tu za kuanzia (bure) ulime kilimo cha alizeti au unipe pesa nikulimie kwa nguvu kazi ya serikali!

Seriously Dripboy Tanzania kilimo ni backbone with 80% depends on it ni basi tu tumekosa kipaumbele
 
Back
Top Bottom