Great Brink’s Robbery: Wizi wa Karne

Great Brink’s Robbery: Wizi wa Karne

Me nafkr wez wa bongo ni moto wa mabua tu..kaona leo aibe kesho, hapo jamaa walipasua miaka 2 ndani ya plan, bigup sana.
 
Nilibanwa mbavu targets zangu za weekend zikafa... BTW how are you doing???

Battery za ABC kuchomolewa ni transition tu yatapita haya
I'm doing fine.Ilibaki kidogo niende likizo hadi mambo ya kuchomoleana betri yaishe. Nikakumbuka story zako nikaamua kubaki
 
Wezi hao walishuka wakiwa wamevaa uniform kama za walinzi wa Brink ambazo ni makoti ya navy, kofia, gloves, viatu vyenye mpira kwenye soli zao ili kutuliza nyayo zao huku wameshika kinyago mkononi teyari kwa kuvaa, walijichelewesha tu kuvaa vinyago ili waweze kumdhibiti mlinzi alikuwa amebaki baada ya wenzao waliokuwa wametoka kwa ajili ya msosi. Kwa namna walivyokuwa wanakuja mlinzi alikuwa amewapa mgongo na kujishtukia ghafla amenyang'anywa bunduki yake na kuwekwa chini ya ulinzi walipomdhibiti uzuri kabisa waliingia nae ndani na kumfungia kwenye stoo ya kuhifadhia vifaa vya usafi.

Wezi walioingia ndani walikuwa saba tu na kuwaacha wawili nje kwa ajili ya kushughulikia suala la usalama na endapo akitokea mtu yeyote basi adhibitiwe ili asije akatia ndimu wizi wao. Wakaanza kufungua milango kama yao maana teyari walishakuwa na funguo bandia za kuwasaidia kufungulia milango mitano ya awali na walipofika wa sita ambao hawana funguo ikawabidi wagonge, na mfanyakazi alikuwa ndani akaenda kufungua akidhani ni mfanyakazi mwenzake mara ghafla alivyofungua tu akakutana na mdomo wa bastola na kuambiwa akae kimya.

Wafanyakazi wa Brink hawakuwa na wasiwasi wowote wa kuvamiwa maana waliuamini ulinzi wa chini na pia waliamini ni vigumu kuvamiwa na wezi kuweza kufungua milango yote mitano hivyo ndiyo maana walifungua mlango bila kuwaza chochote. Walipoingia ndani waliwaweka chini ya ulinzi wafanyakazi wengine ambao walikuwa hawana habari kabisa na walikuwa wakiendelea kupiga kazi. Kilichowashangaza ni kukuta fedha zote zipo nje ya vault ina maana hakuna haja tena ya kuhangaika na mfumo wa kengele.

Walichokifanya walijigawa ambapo wengine walikuwa wanakusanya hela na kuweka kwenye mifuko huku wengine wakiwafunga kamba na plasta mdomoni wale wafanyakazi ili wasiwasumbue na kazi hiyo ilikuwa ikienda faster ili kuendana na muda. Hawa wezi muda wote wakiwa ndani walikuwa hawaongei na walikuwa wanatembea mwendo wa hovyo hovyo kama walevi ama kilema ama mdudu ngadu ama kaa, yote hayo ni kuhakikisha wale wafanyakazi wanashindwa kuwaelezea FBI jinsi walivyo.

FBI unaweza kuwaelezea kuwa sauti zao zipo hivi, tembea yao ipo hivi, mitetemo yao ipo hivi, sura zao zipo hivi au urefu wao ni kiasi hiki na wao wakaweza kudadavua na kumpata mhalifu wao. Sasa hawa wakaja kivingine kwa kubadili mwondoko wao na kutoongea yaani ni mwendo wa ishara tu. Hii ndio dawa za hawa jamaa kwa kutowapa mwanya wa kukudavua na walikamilisha zoezi lao kwa kuiba $2.775 sawa na $28.9m kwa hivi sasa, kwa wakati huo ndiyo rekodi kubwa ilikuwa inawekwa toka taifa hilo liwepo hapa duniani na niyo maana ukaitwa wizi wa karne na walitumia takribani dakika 27 tu na wezi wote wakapotea eneo la tukio.

Nyuma kuna mfanyakazi alipishana na wezi hawa na ndio aliyegundua kuwa kumefanyika ndivyo sivyo akapiga simu polisi na FBI nao walitia timu muda huo huo, walivyofika ghorofa ya pili walikuta wenzao wamefungwa na kuwafungua.

Tuangalie uchunguzi wa tukio:
Baada ya FBI na polisi kutia timu walianza kukusanya ushahidi walioukuta eneo la tukio kuona kama utaweza kuwapa mwanga kuwa ni kina nani hawa wameweza kuweka rekodi! Pia katika majadiliano na hao wafanyakazi waliokuwemo kwenye ghorofa ya pili waligundua kuwa waliondoka na silaha za wafanyakazi hao na mlinzi wao rasmi.
Maafisa wa FBI sasa wakaingia kazini ili kutambua ni kina nani hao. Zile shahidi walizozikusanya eneo la tukio ni kamba walizowafungia hao wafanyakazi, tape walizowazibia mdomoni na kofia moja ya wezi wale ambayo ilianguka eneo la tukio lakini vyote hivi havikuwasaidia chochote katika uchunguzi wao.
IMG_20190829_071725.jpg

Chauffeur's Cap: Wezi wote walikuwa wamevalia kofia aina hii.

Maelezo ya wezi kuwa walikujaje hayakusaidia kwani wafanyakazi walishindwa kuwaelezea kwani walihisi walikuwa walemavu kutokana na mwondoko wao. FBI wakajua tu hamna mlemavu hapo bali ni janja janja tu za wezi hao ili kuwapoteza maboya.

Joto la kesi hii likaanza kwa wezi wote wa jijini Boston kutokuwa na amani kwani kila kukicha FBI na polisi walikuwa wakiwakamata na kusumbuana nao wakijua fika watakuwa miongoni mwao au watakuwa wanaufahamu wizi huo. Hapo tayari FBI washajua namba za noti zote zilizoibwa na kuzijulisha taasisi zote za fedha nchini Marekani kuwa endapo wataziona noti hizo basi watoe taarifa kwao ila kumbe wenzao hawana mpango kabisa wa kuzitumia hela hizo mpaka itimie miaka sita!

Wakati FBI wakiendelea kuwapa joto wezi na makundi yote ya kihalifu jijini Boston, mwezi Februari waliweza kupata silaha mbili ambazo ziliibwa kutoka wafanyakazi wa Brink aina ya Revolver, moja ilipatikana ufukweni na nyingine dampo ila silaha hizo hazikusaidia lolote kung'amua wezi hao. Ilipofika mwezi Machi wakatambua kuwa gari lililoripotiwa kuibwa mwezi Novemba 1949 likitumika katika wizi huo na kuanza kukitafuta kuona kama litawapa mwanga wowote.

FBI mwezi huo huo waliweza kukuta vipande vya gari hilo na kuvifanyia uchunguzi huku wakimshirikisha mmiliki na kutambua ndilo lenyewe, wezi hao walipomaliza kulitumia hilo gari hawakutaka kuwapa mwanya FBI kwani walilikata vipande vipande na FBI kupitia vipande hivyo hawakuweza kuambulia lolote.
IMG_20190829_073813.jpg

Gari aina ya Ford ya Kijani ikiwa imekatwa katwa vipande na kutelekezwa.

Mnamo mwezi Aprili walifanikiwa kuokota mifuko iliyotumiaka kubebea fedha hizo ila bado hawakupata mwanga wowote, yaani mpaka muda huo FBI walikuwa watupu kiufupi wamezidiwa kete na wezi hao. Miezi ilivyozidi kusogea Pino akawa mwizi wa kwanza kukutana na joto la jiwe la FBI kwani alikamatwa na kuhojiwa kama atakuwa amehusika na wizi huo. Pino alikuwa mtu wa kujiamini sana na alitoa ushirikiano wa kutosha kwa FBI na swali kubwa kwake lilikuwa jioni ya tarehe 17 Januari alikuwa wapi?

Kama unakumbuka kwenye mipango yao waliweka kipengele cha ushahidi wa uongo kuwa siku hiyo ya wizi walikuwa sehemu fulani endapo FBI watataka kujua ratiba yao hiyo siku ilikuwaje? Kitu kizuri ni kuwa wezi hao walikuwa wameshajipanga kwa hili kwani walitegemea ya kuwa FBI lazima wangewahoji baadhi yao kama siyo wote na Pino alielezea siku hiyo kabla ya saa moja usiku alikuwa bar anakunywa na aliweza kukutana na kukutana na polisi McGinns na kupiga nae story mbili tatu baada ya hapo akaelekea zake nyumbani na alipoulizwa polisi huyo alikiri kukutana na Pino usiku huo hapo bar na FBI wakashawishika kuwa Pino hakuhusika.

Kiukweli Pino alipita kupata mvinyo ila akiwa na lengo la kutengeneza ushahidi wa uongo sema polisi huyo alikuwa hakumbuki hasa ni mida gani alikutana na Pino hapo bar maana kiza ndio kilikuwa kikiingia na akaasume ilikuwa saa moja usiku kumbe jamaa alipotea mapema tu na wenzake kuelekea Brink. Hapa wakawa wamemkosa Pino na miezi inasogea tu huku kukielekea mwishoni mwa mwaka 1950.

Ikumbukwe wezi hawa walipeana kibarua kigumu cha kutofanya wizi mwingine wowote mpaka watakapogawana mshiko wao baada ya miaka sita kupita. Sasa O'Keefe alishindwa kutimiza sharti hilo na kunasa kwenye uhalifu baada ya kukutwa na sare za polisi ambazo alizitumia kiudanganyifu kwa kutaka kujinufaisha na kutiwa nguvuni na mapolisi wa jijini Boston. Hii ilikuwa mwezi Septemba 1950 ambapo alifikishwa mahakamani na kuhukumiwa kifungo cha miaka minne! Wenzake walimsisitiza ya kuwa wataendelea kuufuata mchoro mpaka atakapotoka gerezani ambapo atakuwa amebakiza miaka miwili kula matunda amyake.

O'Keefe yupo gerezani na huko uraiani FBI wanaendelea kukinukisha bila matumaini yoyote na kupelekea kampuni ya Brink kutangaza donge nono la $100k kwa atakayefanikisha ukamatwaji wa wezi hao, ila bado halikuweza kuwaibua wezi hao kwani raia walikuwa wakifuatilia mtu anayefanya manunuzi ya hovyo ama kula bata sana na kumripoti polisi, kitu ambacho hawa wezi hakuwa nacho kwani wana grace period ya miaka sita!

IMG_20190826_223245.jpg

Mafundi wakiweka vitasa vipya mara baada ya wizi.

Miaka ikawa inasonga mpaka kufika mwaka 1954 ambapo O'Keefe ndiyo alikuwa akitoka jela na alipokuwa gerezani FBI walimuuliza pia suala la Brink na alikataa katu katu kuhusika na alieleza uongo wake kuwa siku ya tukio alikuwa wapi.
Januari 23,1954 O'Keefe alikuwa uraiani tena na akaonana na wezi wenzake ambapo kweli walikuwa hawajagusa hata senti kwani walikuwa wanaziangalia tu kama picha huku wakisubiri wakati sahihi. Wakati wezi hao wakifurahia mwenzao kurudi uraiani mwizi mwenzao Jazz anatiwa nguvuni kwa makosa ya ukwepaji kodi na anapigwa nyundo miezi tisa.

Tuangalie kukamwatwa kwao:
Mpaka O'Keefe anatoka gerezani na Jazz kutiwa hatiani FBI walikuwa hawana mwanga wowote kuwa waliotenda wizi huu ni akina nani na imeshapita miaka minne! Vyombo vingi vya habari vikawa vinauita wizi huu perfect crime kwa kuona FBI wameshindwa kuwabaini wahusika.

Siku zote matukio mengi ya wizi yanafeli kwa makosa madogo madogo ama kwa wezi hao kuzinguana wenyewe kwa wenyewe, ila huu wizi ulikutana na upepo mbaya kwa O'Keefe kuburuzwa tena mahakani kwa kukuta na kosa la kudaiwa pesa na jirani yake. O'Keefe akawa anahitajika kulipa hizo pesa ama ataburuzwa mahakamani naye kipindi hicho alikuwa apeche alolo yaani majalala. Akawa anawasiliana na wenzake Pino na Big Joe kuwa wampe chake ili ajinusuru na mvua nyingine, wao wakamjibu kwa kukataa ya kuwa ataharibu mchoro wao na yeye apambane na hali yake kwani hata wao wana matatizo lukuki ila wamejikaza kisabuni mpaka siku yenywe itimie.

Sasa O'Kefee akawa haelewi tena mambo ya mchoro wala maagano akawa analazimisha kupewa chake hivyo akawa anawatumia barua mara kwa mara kwa vitisho kuwa asipopata chake basi atawachomolea betri na dili zima litabumburuka huku yeye walau aambukie michuzi iliyotangazwa na Brink kama zawadi kuliko kuendelea kuteseka.

Pino akaona O'Keefe ashaanza kuwa tatizo na akajadiliana na Big Joe na wakakubaliana inabidi wafanye maamuzi magumu na wamuondoe duniani kwani ataweza kuwachoma kwa mapolisi kutokana na njaa zake. Pino ndio aliratibu mpango mzima wa kumuua O'Keefe kwa kukodi hitman wa kufanya kazi hiyo na tarehe iliyopangwa ilikuwa ni Juni 5, 1954 kwa majina Elmer "Trigger" Burke na alimvizia O'Keefe wakati anatoka nyumbani kwake mida ya asubuhi. Basi huyo muuaji akatoa bastola yake na kumlenga O'Keefe, kwa bahati nzuri alimuona muuaji na kuinama huku risasi zote zikimkosa na kuishia kupasua vioo vya gari yake na hakudhurika popote.

Wakina Pino baada ya kusikia hivyo walikasirika kweli kuwa kwanini operation imefeli na O'Keefe hakujua nani amemshambulia au katumwa na nani kwasababu yeye ni mhalifu hivyo wanakuwa na visa vya kudhulumiana, visasi, mabifu n.k hivyo hakuwahisi wenzake kuwa ndio walimsukia kifo hicho alichonote tu ni kuwa yupo hatarini na muda wowote anaweza kuuawa.

Yule muuaji akawatoa wasiwasi akina Pino kuwa safari hii lazima ammalize na ikapangwa tarehe 14 Juni ndipo atekeleze mauaji kwa jaribio la pili na hii siku muda wa asubuhi O'Keefe alikuwa na mwenzake wanaenda kununua vitafunwa, muuaji naye hakucheza mbali kwani alijifanya naye mnunua vitafunwa na akazama dukani na alipofika tu akaanza kuwarushia risasi ila wakawahi kuinama chini na kujificha na meza kujikinga na risasi na wakati huo O'Keefe na mwezake walikuwa na silaha wakazitoa na kuanza kurushiana na muuaji alipoona anazidiwa ikabidi kukimbia.

Mara ya pili anakoswa Pino na mwenzake wakaanza kukosa imani kwa muuaji wao kushindwa kuimaliza target yao na kadiri anavyochelewa ndivyo wanahofia O'Keefe anaweza kuropoka kwa kuhisi muuaji huyo katumwa na wao.
Muuaji akaomba nafasi ya mwisho na ikapangwa tarehe 16 Juni, huu mwezi wa sita ulikuwa mbaya sana kwake kwani ameshakoswakoswa mara kadhaa kuuawa na wabaya wake safari hii muuaji akabadilisha silaha na kutumia silaha yenye uwezo mkubwa aina ya machine gun ili awe anazimimina risasi tu na asipate mwanya wa kukitoroka kifo safari hii.
Kwa wakati huo aina hizo ya silaha zilikuwa chache sana jijini Bustoni hata nchini Marekani.
Safari hii O'Keefe alikuwa Donchester na muuaji alikuwa maeneo hayo hayo akimvizia na alipomuona tu akachomoa machine na kuanza kumminia risasi kama mvua na takribani risasi 30 mpaka 50 zilirushwa kuelekea kwake. Waswahili wanasema Mungu si Athuman na kati ya risasi zote zilizomiminiwa kwake ni tano zilimpata na yeye akatoa bastola yake na kuanza kujibu mashambulizi ila akawa anazidiwa, akafanikiwa kutoroka na muuaji alipoona damu zimetapakaa akajua amemaliza kazi.

Baada ya mirindimo ya risasi kusikika wananchi ilibidi waripoti polisi na kuona hivyo muuaji hakuona haja ya kwenda kukagua kama amemmaliza ama lah... Polisi wakawasili eno la tukio na kukutana watuhumiwa wote hawapo eneo la tukio ila wanakuta bastola ya O'Keefe ipo chini na saa yake ya mkononi vyote vikiwa vimeloa damu na waliona michirizi ya damu ikionesha manusura alikimbia.

Kutokana maganda ya risasi yaliyookotwa eneo la tukio waligundua aina ya silaha iliyotumika kuwa ni machine gun na kwa kipindi hicho zilikuwa silaha chache sana hivyo wakajua lazima watamng'amua mwenye silaha. O'Keefe alipotea jijini Boston bila kujulikana alipotelea wapi ama amefia wapi maana alijeruhiwa maeneo ya kifua. Akina Pino nao walikuwa wanamtafuta bila majibu kwa sababu ya milio ya risasi zile walijua hawezi kutoboa ila kwa walitaka wajiridhishe kabisa kwa kuona maiti yake.

Tarehe 17 Juni polisi walimkamata jamaa huyo majina Burke ambaye ndiye alikuwa mshtumiwa kwenye mauaji ya O'Keefe maana ndiye alikuwa mmiliki wa mchine gun na alikuwa akijulikana kuwa ni muuaji. FBI walipomhoji nini nyuma ya hayo mauaji aliwaambia ameagizwa na watu flani kutekeleza hayo mauaji ila hajui sababu na hawezi kuwataja mabosi wake.

Akawekwa chini ya ulinzi mahabusu huku kwa kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria na mauaji, O'Keefe akiendelea kusakwa kila kona na Agosti 1, polisi waliweza kumtia nguvuni alipokuwa anatibu majeraha yake.
O'Keefe anakamatwa kwa kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria na siku tatu baadaye alipelekwa mahakamani na tarehe 5 Agosti alihukumiwa miezi 27 jela na alipelekwa gereza la Hampden County.

Lacter rafiki yake mkubwa O'Keefe ambaye alihitajika katika uchunguzi ili kumtambua Burke na aweze kusaidia kuwa alitumwa na akina nani ili kumuua rafiki yake huyo aliweza kufika siku ya kwanza katika mahojiano na hakurudi tena mpaka walipokuta gari yake imetelekezwa na siku chache baadaye wakakuta mwili wake akiwa ameshakufa. Pino na mwenzake ndio walimuua ili kupoteza ushahidi kwani walihisi O'Keefe atakuwa amemwambia rafiki yake kuhusu wizi ule.

Huku FBI wanaendelea na uchunguzi wao kuhusu tukio la Burke ila bila kutarajiwa jamaa huyo aliweza kutoroka mahabusu. Pino ndio alifanikisha mchakato huo mzima kwa gari binafsi kuhusika kumbeba na kuliegesha karibu na emeo la tukio, FBI katika uchunguzi wao walikuta gari lilohisiwa kumtorosha Burke linamilikiwa na Pino. Pino akatiwa nguvuni na alikubali siku ya tukio alikuwa maeneo hayo ila alikuwa hajui chochote kuhusu utorokaji wa Burke na alijitetea sana kiakili mpaka FBI wakaingia laini na kumuona hana hatia na kuamua kumuachia.

Agosti 27, Burke tena akatiwa nguvuni na FBI chini ya ulinzi mkali baada ya msako wa nguvu na alikuja kusomewa mashtaka kede ya mauaji na majaribio matatu ya kutaka kumuua O'Keefe na akahukumiwa kifungo cha maisha jela kwani hakutaka kutoa ushirikiano wowote ule na mwaka huo yaani 1954 hakuwa mzuri kabisa kwa wezi wa Brink kwani wezi wanne walitiwa nguvuni kwa makosa tofauti tofauti ya uvunjifu wa sheria na kufungwa jela miezi tisa mpaka miaka miwili na mmoja wa wezi alifariki kwa ugonjwa kawaida bila kupata gawio lake na huyo ni Banfield.

Pino na Big Joe hawakuwa kati ya wezi hao waliokamatwa kwani wao walimantain nidhamu ya hali ya juu ila baadaye kidogo Pino alisumbuliwa na uhamiaji kwasababu asili yake alikuwa Muitaliano na aliingia Marekani kipindi cha miaka ya 1920.

Maafisa wa FBI waliokuwa wanachunguza wizi wa Brink mpaka kuingia mwaka 1955 hawakuwa na mwanga wowote ule kwenye kesi hiyo na ulikuwa umebaki mwaka mmoja gawanyo lipite na uzuri wote waliofungwa walitarajiwa kutoka kabla ya mwaka 1956! O'Keefe akiwa gerezani aliendelea kuwatumia akina Pino barua kudai chake akiwaambia muda wa kukaa jela utaongezeka endapo hatolipa kile kiasi anachodaiwa kwasababu hapo anatumikia kifungo cha kumiliki silaha kimakosa.

Mwishoni mwa mwaka 1955 mwanasheria wa O'Keefe alimtaarifu kuwa yule muuaji Burke alikuwa akitumwa na akina Pino kukuondoa duniani na hata ukitoka na kurudi jijini Boston wataendelea kukuandama na kutaka kukua ingawa mwanasheria wake hajui kwanini mteja wake anaandamwa hivyo akabaki kuamini ni mabifu ya shughuli zao za uhalifu.

Hiyo hali ilimuumiza sana O'Keefe na hapo kilikuwa ni kipindi cha Xmass na akiangalia ratiba ulikuwa umebaki kama mwezi tu wizi wao utimie miaka sita na gawio lipite na bado alikuwa gerezani na hata akitoka alijua hawezi kupewa chake kwani teyari yupo kwenye radar za kuuawa.

Sasa ikambidi kufanya maamuzi magumu na kuomba kuongea na FBI, na tarehe 6 Januari 1956 yaani siku11 kabla ya wizi kutimiza miaka sita akawaambia FBI kinagaubaga kwa yote yalitokea kwenye wizi wa Brink na wahusika, ila hapa alikuwa mjanja kidogo kwa kuomba kupunguziwa adhabu na hawakuwa na pingamizi lolote kwani kesi hii ilikuwa ishawapiga bao.

Basi baada ya hapo walianza kukamatwa mmoja mmoja mnamo tarehe 12 Januari ambapo ni siku tano kabla ya mgao wao kuanza, wafuatao walikamatwa Baker, Costa, Geagan, Maffie, McGinnis na Pino. Baadaye Faherty and Richardson walikamatwa mnamo Mei 16 huko Dorchesterna na ikumbukwe gerezani kulikuwa na mwizi mmoja tu hivyo basi wakapandishwa kizimbani na kuanza kujibu mashtaka yao, O'Keefe alisimama mahakamani kama shahidi na alielezea mahakama kila kitu. Kabla ya hukumu ya Agosti 6 Gusciora alifariki mnamo Julai 9 huku nae McGinnis akafariki. Hivyo basi wahusika 8 walipigwa mvua ya maisha gerezani isipokuwa O'Keefe alipigwa mvua nne tu ambaye iliisaidia mahakama kuhitimisha kesi hii ngumu sana, wote waliswekwa State Prison huko Walpole, Mass.
IMG_20190829_071101.jpg

Mwanasheria mkuu wa Marekani wakati huo Anthony Julian akiwaammbia wanahabari wa jijini Boston juu ya kukamatwa kwa watuhumiwa sita wa kesi hiyo, Januari 12, 1956.

Kwa maana hiyo hii tayari ilishakuwa perfect crime kabla ya njaa kumpanda O'Keefe kichwani na kuchomolea wenzake battery na kusaidia FBI na mahakama kuwatia nguvuni wezi wote na cha kushangaza katika kesi hii fedha zilizopatikana ni $58k tu kati ya $2.7m zilizoibwa!

Kwa upande wa Hollywood hawakuwa nyuma nao waliweza kutengeneza filamu nne kuhusu tukio hili nazo ni kama ifuatavyo; 6 Bridges to Cross iliyotoka mwaka 1955 ambapo bado wizi ulikuwa perfect crime, Brinks: The Great Robbery ya mwaka 1976, The Brink's Job ya mwaka 1978 na The Town ya mwaka 2010.
 
Hatari sana...

Ndiyo maana gerezani wale wahalifu wenye matukio makubwa sana na ya kutisha mara nyingi hawachanganywi na wengine, kwa sbabu za kuepuka mipango na mikakati kufaulishwa kwa wengine...



Cc: mahondaw
Wakikutana vitasa hawakawii kusuka mipango hatari humo humo na wakitoka wanakinukisha kama kawaida
 
Back
Top Bottom