Nyamemba
JF-Expert Member
- Nov 3, 2011
- 845
- 446
Katika kile kinachoonyesha kuwa mabadiliko ndani ya jamii hayaepukiki,wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya wavulana ya mzumbe iliyopo hapa morogoro wameendelea na msimamo wao wa kuushinikiza uongozi wa shule hii kongwe na mahili katika taaluma hapa nchini uwaalike viongozi wa CHADEMA katika mahafari yao ambayo yalikuwa yafanyike alhamisi hii na kuahilishwa mpaka hapo itakapo tangazwa tena.Wanafunzi hao wameendelea kumnyima usingizi mkuu wa shule huyo kwani amebainisha wazi kuwa hawezi kutimiza matakwa ya wanafunzi hao kwa kuwa anahisi atapoteza kibarua chake,yeye ameendelea kuwashinikiza walete viongozi wa serikali mfano mh SITTA/MWAKYEMBE au yeyote ilimradi atoke ndani ya serikali lakini wamekataa na kuahidi kufanya kituko iwapo ataenda kinyume na matakwa yao,wanamtaka either mh MBOWE/ZITTO/dr SLAA au MNYIKA.