Graduate kuomba kazi za utendaji kijiji

Graduate kuomba kazi za utendaji kijiji

TINDIX

Member
Joined
Jun 4, 2015
Posts
26
Reaction score
7
Habari za jumapili wapendwa wangu nauliza kama graduate anaweza kuomba hizi kazi za utendaji wa kijiji III zilizotoka katika halmashauri nyingi, au ukiwa na degree huruhusiwi kuomba?

Hadi tu hao wenye certificate?, nataka kuomba ili iwe starting point yangu ya kuingia kwenye government system
 
Kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma huruhusiwi.
Graduate kuomba nafasi ya mhitimu wa astashahada na stashahada.
Ila kama degree yako ilikuwa ya kuungaunga, yaani from certigicate to diploma and then degree unaweza kuomba kwa kuficha vyeti vya juu. Na baada ya miaka 3 unaweza kufanyiwa
recategorization na ukakaa mahali pa juu. Katika suala la kuficha sifa lianze kwenye barua ya kazi, nakala na C.V.
Ukijichanganya sehemu moja tu imekula kwako.
 
Mimi kama HR wa nakukata mapema...status inakuwa...over-qualification...
 
habari za j2 wapendwa wangu nauliza kama graduate anaweza kuomba hizi kazi z utendaji wa kijiji III zilizotoka katika halmashauri nyingi, au ukiwa na degree hurusiwi kuomba? hadi tu hao wenye certificate?, nataka kuomba ili iwe starting point yangu ya kuingia kwenye government systyem
graduate kutoka chuo gani? Kuna some of the universities sawa na certificate. Omba tu watachambua huko huko



Sent using Jamii Forums mobile app
 
We ni mtu wa ajabu sana, yani umesoma degree (kwa kufauru kwako), na unataka kutubania sisi vilaza wa certificate. Ebu komaa na degree jobs bana tuachie sisi
 
Back
Top Bottom