Heshima zenu wakuu. Nakuja leo kuomba maelekezo kwenu mliobobea katika maswala ya teknolojia. Mie nina simu Tecno M7 ina mwezi 1 tu toka upya. Juzi imeanza kujiwasha GPS nikipiga Simu kwa line ya Airtel au nikiingia internet ya 3G kwa Airtel pia. Nikitumia voda halijitokezi. Hata nikiizima bado itajiwasha tu. Ni tatizo gani hili na nalisovu vipi? Nawasilisha.
Mkuu, angalia usije ukawa unatafutwa na jamaa hivyo wanaiwasha wenyewe ili wajuwe upo sehemu gani, chukuwa tahadhari mkuu.
Kama upo sahihi vile??
Nimeshajaribu kufanya factory reset lakini bado. Nimeinstal nova launcher bado sioni tofauti, au kuna setting sijafanya kwenye hiyo nova launcher? Nisaidieni jamani.