GPA yako unaeza ukafa nayo maskini

GPA yako unaeza ukafa nayo maskini

The Humble Dreamer

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2015
Posts
8,011
Reaction score
11,444
NI WAZO TU

Wewe ni Msomi mwenye Digrii,na Ulipata GPA 4.6 ukiwa unajua GPA ni dili lakini ulizunguka 2YEARS bila kazi mpaka ulipodaka Kibarua hiki cha Benki ukiwa kama LOAN OFFICER,na wakakupa Mshahara wao wa 750,000 Kwa Mwezi.

Baada ya Mwaka Mmoja ukajihisi UNA HADHI huna haja ya kurukia Daladala kama wengine,ukajibandika KAMKOPO KA PASSO ambako unakatwa LAKI4 Kila Mwezi na unabakiza 350,000 inayoenda Mfukoni kila Muamala Ukisoma.

Pale Chini ya Ghorofa la Ofisi unakofanya kazi yuko Kijana,Mchafu Mchafu,ANAOSHA MAGARI,na kila "MABOSI" mkifika wote mnamuachia Funguo za Magari yenu ya Mikopo Awaoshee.

Mtaji wake ni KOPO LA FUNGUO,SABUNI,na MAJI anayochota kwenye Kimtaro karibu tu na mnakopaki gari zenu.

KWA SIKU anaosha MAGARI 30,ya Mabosi Nyinyi kwa Shilingi 3000 kwa Kila Gari...Anakula Wali Maharage Kibandani kwa Sh 800 tu wakati WEWE na "HADHI YAKO" unaenda kula YMCA Canteen,IFM Restaurant au KFC,ili Kulinda Hadhi ambayo Actually HUNA!

Mshahara ukitoka,wewe una 350,000 Mfukoni,ila Kijana huyu Mchafu Mchafu anayekula kwa Mahesabu,ambaye sometimes kwa kuona ANA HALI NGUMU huwa unamuachia hata CHENJI imsaidie,Anatengeneza Sh 3000x Magari 30 x Siku 30 =2,700,000(Milioni Mbili na Laki Saba Kwa Mwezi,NON TAXABLE!

Tai Kubwa,Viatu Vimeenda Upande,Mkopo wa Gari,HELA HAITOSHI,ila TITLE KUBWAAAA Ofisini unazunguka kwenye Kiti,Kila Siku una STRESS na unashangaa huyu kijana ANASMILE KILA SAA na Kukusalimu "Shkamoo Bosi" na unajiuliza Huyu Maskini Mbona Ana Raha Kila Siku na Mimi Majanga?

NANI MASKINI KATI YENU?

NANI BOSI WA KWELI?
Wake Up Brother/Sister,Find a Plan B for Your Life,Huwezi Kuwa Mjinga Milele na Ukaamua Kutulia tu...Unalipwa Laki 4 TANzania Hii,HUJALA,HUJALIPA KODI,HUJANUNUA UMEME,HUJAHONGA,HUJAZUNGUSHA RAUNDI ZA BIA,na HUNA KIPATO KINGINE ZAIDI YA AJIRA lakini Unahisi UKO SAWA TU, Shaur yako.
 
sikuiz mjini hawaruhusu kuosha magari

hii kitu mara ya kwanza kuisoma ilikuwa 2014 zama zimebadilika unajua?? hiyo 350k ni nyingi sana kwa maisha ya sasa
 
Anayeyasema haya kakosa kazi sasa anawatisha wasaka ajira, je mbona hujazungumzia ambaye hakopi gari Malengo yake ni kujikusanya miaka kadhaa akafungua kazi yake?
 
Masikini ambao hatujasoma hebu tuache kudanganyana na kujipa moyo.

Mtu aliyesoma na ambaye hajasoma wana tofauti kubwa sana.

Huyu aliyesoma na kufanya kazi anapata mkopo ila huyu muosha magari mkopo hapati na akipata basi ni kwa resources zingine.

Tukubali tu mtu aliyesoma ana advantage kuliko ambaye hajasoma.
 
Hatuwezi kuwa matajiri wote.

Hatuwezi kuajiriwa wote.

Hatuwezi kujiajiri wote.

Duniani ni mapambano ya kutafuta ridhiki,na wote tunategemeana.

Kila mtu apambane na hali yake.
 
Uzi ungesisitiza vijana kuwa na plan B peke yake ingetosha kutupa motisha,mengine hayo ya mkopo wa passo,cjui kuosha magari ni stori za kufikirika/fiction..
 
Back
Top Bottom