GPA ya 32, maandiko yametimia

GPA ya 32, maandiko yametimia

Dk.Shika,Rashid Mashaushi,Mama wa mapapai,muomba nauli wa bandarini na degree 32,kwa nini yanatokea awamu hii?

Sent using Jamii Forums mobile app
"Basi kiongozi yule mtarajiwa wa Malaika akayachukua yale mapapai akawaonyeshea makutano,akawaambia kuleni haya mapapai maana imeandikwa awamu hii hata kula yenu itakuwa taabu na mateso kwenu sababu nimeamua kuwalimisha kwa Meno"aliposema hayo wale makutano wakala yale mapapai na kumshangilia Kwa unafiki ili maandiko yapate kutimia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimenote kitu hapo miaka 32 tangu mchonga ang'atuke madarakani... Na GPA ya 32... Kiroho ina tafsiri yake pana sana japo ni tukio lenye viashiria vyote vya kutengenezwa

Jr
Source kubwa ya GPA 32 ilianzia kwa mchonga,the guy was pathetic.Toka hao akina Mwaikambo walipompa za uso kuwa afadhali ya mkoloni ndio akaanzisha mitaala ya kuvunja challenge.
1.Walimu wa UPE
2.Serikali kuchukua shule za Taasisi za dini.
3.Propaganda za Azimio la Arusha.
4.Kuzamishwa matumizi ya lugha ya Kiingereza katika shule.
5.Musoma Resolution
Pammoja na anguko la uchumi lilosababishwa na
6.Vita ya Kagera
7.Gharama kubwa ya Ukombozi kusini mwa Afrika.
 
Alitakiwa akamatwe na Afungwe kwa kosa la Kumdanganya Mh Rais Mbele ya Umma kiasi kile.
 
Ukikutana na chizi anaimba na we kama yeye utatoka salama rais ameshindwa kutumia akili ya kujiokoa kwa chizi tena eti chizi analazimishwa atoe maelekezo na anafata maelezo kama rais anavyotaka chizi apangiwi la kuongea eti utaki elimu ya kuanzia chin amepitia wap anataka kujua chuo gan amesoma president apewe mafunzo jinsi ya kucheza na watu wanaoenda kufanya nao maigizo mbona mwanzo alikua ana perform vizur nao amekua mzoefu ataki tena kufundishwa nn

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Propaganda ni neno linalotokana na neno la ki-latini lililotumiwa kihistoria kwa Mara ya kwanza na chombo kipya katika kanisa katoliki kilichoundwa mwaka 1622 ambacho kilijulikana kwa jina la "Congregation de Propaganda" au kwa lugha isiyo rasmi "Propaganda".Ki-latini neno "Propagare" linamaanisha kusambaza yani Spread au Propagate.

NINI LILIKUWA DHUMUNI LA PROPAGANDA
Chombo hiki yaani Congregation de Propaganda kiliundwa mahususi ili kusambaza jumbe na kuhakikisha watu wanaamini katika U-Catholic na hasa ambao awali hawakuwa katika imani hiyo.Mnamo mwaka 1970 neno hili lilianza kutumika katika nyanja ambazo si za kiimani(Secular activities).
Na hatimaye katikati ya karne ya kumi na tisa ilichukua taswira mpya ambayo ni hasi hasa baada ya kuanza kutumika katika siasa(Political Sphere).
Kabla ya hapo na ambapo neno hili limeanza kutumika tayari,Propaganda inatajwa kufanikisha mabadiliko na matukio makubwa ulimwenguni baadhi ni Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Rumi 44-30 BC,Reformation katika bara Ulaya na Mapinduzi ya Wamarekani(American Revolution) n.k

PROPAGANDA TANZANIA.
Ni miaka 32 sasa tangu Rais wa kwanza wa Tanzania hayati mwl Julius Nyerere ang'atuke,maadui wakuu watatu Ujinga,Maradhi na Umasikini graph yake inapanda kwa kasi,Tumeongeza Ujinga,Maradhi na Umasikini umekithiri,Mission failed.
Adui wa CCM si hao watatu tena,Sasa CCM adui yake namba moja ni Elimu na inafanikiwa kwa kasi sana kupitia propaganda zake mahsusi.
Si rahisi sana kueleweka pasipo kazi ya ziada katika jambo zito kama hill ambalo kwalo serikali ya Chama cha mapinduzi inaanza kufanikiwa pakubwa sana katika hili...Hivi sasa kote duniani serikali hutumia Propaganda kufanikisha Maslahi yake,kwa maana hii bila shaka Tanzania ni jambo ambalo lipo.

GPA YA 32
Binafsi nina mashaka makubwa na kijana yule mwenye GPA ya 32 na SUA ya Dodoma badala ya Morogoro,Pamoja na maelezo yake mengi sana yenye utata.
Kwanza,tukiangalia kwa muktadha kwamba Kijana yule alidhamiria kumdanganya mheshimiwa kuhusu elimu yake ili apate ajira,swali ninalojiuliza vipi kama Rais angempatia ajira angelipeleka vyeti gani?
Pili,kama yule bwana alikosa Confidence katika umati ule bado nashindwa kisadiki kwamba inaweza kupelekea aongee mambo ya ajabu kama Degree ya Udaktari wa Engineering, Non Sense,kwa msomi hata temper isingelikuana namna ile.
Tatu,Kama alikua ni kichaa yani mgonjwa wa akili basi it makes sense.

TUKO KATIKA NYAKATI GANI
Ninaomba niwakumbushe ndugu zangu,hivi sasa tuko katika nyakati ambapo ajira ni tatizo sugu ambalo serikali yetu ya Ccm imezidiwa,kuna umuhimu mkubwa was serikali kutafuta kichaka cha kujifichia.

PROPAGANDA ZA CHAMA CHA MAPINDUZI
Kwa hakika tukio kijana yule ni la kutengenezwa kwa zaidi ya 100%,ili umma uamini yafuatayo
01.Wasomi hawapati ajira na ni haki yao ya msingi kutopata ajira kwasababu hawakuwa makini na walochobobea.
02.Wasomi hawapaswi kusikilozwa katika jamii ya Kitanzania kwa sababu hawana tofauti na wasiosoma,tukio like lilitengenezwa mahsusi ili kuuhadaa umma kutokuwasikiliza wasomi kwasababu CCM inaelewa wasomi na adui wao nambari moja.

Shame On CCM

Sent using Jamii Forums mobile app

Uko sahihi na ni wachache sana watakoweza kuelewa ile logic. Pili, kimsingi walifeli sana, km waliwalenga wasomi watapuuza upuuzi kuwa mtu anaweza kusoma na asijue gpa na km waliwalenga wapiga kura wao, most hawajui gpa na mbaya zaidi hawatanunua upuuzi kuwa eti msomi ana degree lakini hajui alichukua wapi.
 
.Mimi ni mhitimu kutoka chuo kikuu flani, juzi kati wakati tunafanya mitihani ya mwisho, alikuja katibu wa ccm wilaya akiwambia vijana "kama mnataka ajira jiunge ccm" kwa kuwa vijana kwa sasa wanaangaika sana walikubali haraka wakapewa kadi za ccm, vyeti vya kuonesha kuwa valikuwa wanaccm wakati wakiwa chuoni, wakauziwa t-shirt na wakaambiwa waache namba zao za simu kuwa watapangawa kazi punde
Kweli nilishangaa sana kuona jinsi Tanzania inako elekea kwa sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Propaganda ni neno linalotokana na neno la ki-latini lililotumiwa kihistoria kwa Mara ya kwanza na chombo kipya katika kanisa katoliki kilichoundwa mwaka 1622 ambacho kilijulikana kwa jina la "Congregation de Propaganda" au kwa lugha isiyo rasmi "Propaganda".Ki-latini neno "Propagare" linamaanisha kusambaza yani Spread au Propagate.

NINI LILIKUWA DHUMUNI LA PROPAGANDA
Chombo hiki yaani Congregation de Propaganda kiliundwa mahususi ili kusambaza jumbe na kuhakikisha watu wanaamini katika U-Catholic na hasa ambao awali hawakuwa katika imani hiyo.Mnamo mwaka 1970 neno hili lilianza kutumika katika nyanja ambazo si za kiimani(Secular activities).
Na hatimaye katikati ya karne ya kumi na tisa ilichukua taswira mpya ambayo ni hasi hasa baada ya kuanza kutumika katika siasa(Political Sphere).
Kabla ya hapo na ambapo neno hili limeanza kutumika tayari,Propaganda inatajwa kufanikisha mabadiliko na matukio makubwa ulimwenguni baadhi ni Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Rumi 44-30 BC,Reformation katika bara Ulaya na Mapinduzi ya Wamarekani(American Revolution) n.k

PROPAGANDA TANZANIA.
Ni miaka 32 sasa tangu Rais wa kwanza wa Tanzania hayati mwl Julius Nyerere ang'atuke,maadui wakuu watatu Ujinga,Maradhi na Umasikini graph yake inapanda kwa kasi,Tumeongeza Ujinga,Maradhi na Umasikini umekithiri,Mission failed.
Adui wa CCM si hao watatu tena,Sasa CCM adui yake namba moja ni Elimu na inafanikiwa kwa kasi sana kupitia propaganda zake mahsusi.
Si rahisi sana kueleweka pasipo kazi ya ziada katika jambo zito kama hill ambalo kwalo serikali ya Chama cha mapinduzi inaanza kufanikiwa pakubwa sana katika hili...Hivi sasa kote duniani serikali hutumia Propaganda kufanikisha Maslahi yake,kwa maana hii bila shaka Tanzania ni jambo ambalo lipo.

GPA YA 32
Binafsi nina mashaka makubwa na kijana yule mwenye GPA ya 32 na SUA ya Dodoma badala ya Morogoro,Pamoja na maelezo yake mengi sana yenye utata.
Kwanza,tukiangalia kwa muktadha kwamba Kijana yule alidhamiria kumdanganya mheshimiwa kuhusu elimu yake ili apate ajira,swali ninalojiuliza vipi kama Rais angempatia ajira angelipeleka vyeti gani?
Pili,kama yule bwana alikosa Confidence katika umati ule bado nashindwa kisadiki kwamba inaweza kupelekea aongee mambo ya ajabu kama Degree ya Udaktari wa Engineering, Non Sense,kwa msomi hata temper isingelikuana namna ile.
Tatu,Kama alikua ni kichaa yani mgonjwa wa akili basi it makes sense.

TUKO KATIKA NYAKATI GANI
Ninaomba niwakumbushe ndugu zangu,hivi sasa tuko katika nyakati ambapo ajira ni tatizo sugu ambalo serikali yetu ya Ccm imezidiwa,kuna umuhimu mkubwa was serikali kutafuta kichaka cha kujifichia.

PROPAGANDA ZA CHAMA CHA MAPINDUZI
Kwa hakika tukio kijana yule ni la kutengenezwa kwa zaidi ya 100%,ili umma uamini yafuatayo
01.Wasomi hawapati ajira na ni haki yao ya msingi kutopata ajira kwasababu hawakuwa makini na walochobobea.
02.Wasomi hawapaswi kusikilozwa katika jamii ya Kitanzania kwa sababu hawana tofauti na wasiosoma,tukio like lilitengenezwa mahsusi ili kuuhadaa umma kutokuwasikiliza wasomi kwasababu CCM inaelewa wasomi na adui wao nambari moja.

Shame On CCM

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimefuatilia kwa makini
Lakini
Bila shaka mwenye Gpa ya 32
Alipata ujasiri/kusimama mbele ya muheshimiwa
Akijua atapata anagalau ajila ya uteuzi
Na
Sina uhakika inawezekana alie muandaa kijana yule alimwambia
Aseme GPA ya 3.2 na sio 32
Sababu unampa mtu
Jukumu la technical kama lile
Ni rahis kuteleza kwa kisema 32
Sijui hali yake ikoje kwa sasa yule bwana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali ya CCM imezidiwa!!. Mkuu mleta mada tazama tu idadi ya wanaopata mikopo ndipo utajua kuwa serikali haijazidiwa.

Tazama wanaopata huduma mahospitalini kila kukicha ndio utajua kuwa serikali haijazidiwa.

Tazama sekta ya mawasiliano inavyozidi kukua ndio utajua kuwa haijazidiwa. Waliozidiwa maarifa ni wanasiasa ambao wanaongozwa na mtu mmoja kwa miaka 14 na hawana ujanja wowote wa kupata mwingine mwenye maono mapya yenye kuwa na faida kwenye chama chao!!.

Yule jamaa ni mmoja wa wabongo wengi ambao hupenda kutaka kuonekana kuwa wanajua kila kitu, japo wanachokiongelea hawakifahamu.

Yule jamaa ni sehemu tu ya kizazi cha wapenda uongo, na ni kizazi kitakachopotea ndani ya miaka michache ijayo kwani wasomi wa kweli ndio wenye soko kwa sasa na kuendelea.

Ana bahati kwamba rais aliamua kuachana nae baada ya kumjua ni mtu mtafuta sifa za kwenye halaiki. Alichokifanya ni kosa la jinai, kudanganya kuwa una elimu fulani wakati huna ni sawa sawa na kutengeneza cheti feki kwenye stationary fulani.
Unadhani kwa nini usalama walimuachia??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
lusinde utaelewa nini kwenye andiko lilipoangiliwa kama hili la mleta uzi
mtu amalize chuo asijue GPA inaishia ngapi!!!!
mtu asome SUA halafu aseme ipo DODOMA!!!!!
mtu amalize chuo ashindwe kutofautisha uhandisi naudaktari
ndio maana nasema usalam wa taifa wetu akili zao zimekuwa ndogo kama za ccm
maigizo yao yanatia aibu
 
Back
Top Bottom