GPA ya 32, maandiko yametimia

Wale akina Dr shika, nabii tito na huyu wa GPA 32 ni watu wa kitengo hutokea kipindi fulani ku interfere ishu zilizopo mezani hasa kama mazingira ya ufyatuaji lisasi yapo vibaya kwao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nabii Tito kweli alikuwa na matatizo.
Alifikia hatua alijikata hadi matumbo unafikiri ni propaganda?
 
.Mimi ni mhitimu kutoka chuo kikuu flani, juzi kati wakati tunafanya mitihani ya mwisho, alikuja katibu wa ccm wilaya akiwambia vijana "kama mnataka ajira jiunge ccm" kwa kuwa vijana kwa sasa wanaangaika sana walikubali haraka wakapewa kadi za ccm, vyeti vya kuonesha kuwa valikuwa wanaccm wakati wakiwa chuoni, wakauziwa t-shirt na wakaambiwa waache namba zao za simu kuwa watapangawa kazi punde
Kweli nilishangaa sana kuona jinsi Tanzania inako elekea kwa sasa
 
Propaganda utumika kama njia ya kuwaamisha watu kwenye reli waache kujadili jambo Fulani waelekeze kwenye kitu kingine ili kuizima ishu inayotrend,mfano Richmond Na kikombe cha babu,Dr shika,USA embassy vs chaguzi za marudio na GPA ya 32.nk.Ukiona ishu yoyote inayokaba kifuatacho ni propaganda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii uliy
Haya mawazo yako ulio andika in propaganda ya CHADEMA! Eti?
 
Huu uzi mgumu kukomenti....ngoja ntakomenti baada ya kutafakari
 
Naamini serikali haiwezi kufanya upuuzi huu.unless kama watanzania hawana akili kabisa,Elimu inatolewa na nani? Kama graduates wetu ni mazuzu shida ni wao au shida ni elimu inayotolewa na serikali ya ccm?
 
Serikali ya CCM imezidiwa!!. Mkuu mleta mada tazama tu idadi ya wanaopata mikopo ndipo utajua kuwa serikali haijazidiwa.

Tazama wanaopata huduma mahospitalini kila kukicha ndio utajua kuwa serikali haijazidiwa.

Tazama sekta ya mawasiliano inavyozidi kukua ndio utajua kuwa haijazidiwa. Waliozidiwa maarifa ni wanasiasa ambao wanaongozwa na mtu mmoja kwa miaka 14 na hawana ujanja wowote wa kupata mwingine mwenye maono mapya yenye kuwa na faida kwenye chama chao!!.

Yule jamaa ni mmoja wa wabongo wengi ambao hupenda kutaka kuonekana kuwa wanajua kila kitu, japo wanachokiongelea hawakifahamu.

Yule jamaa ni sehemu tu ya kizazi cha wapenda uongo, na ni kizazi kitakachopotea ndani ya miaka michache ijayo kwani wasomi wa kweli ndio wenye soko kwa sasa na kuendelea.

Ana bahati kwamba rais aliamua kuachana nae baada ya kumjua ni mtu mtafuta sifa za kwenye halaiki. Alichokifanya ni kosa la jinai, kudanganya kuwa una elimu fulani wakati huna ni sawa sawa na kutengeneza cheti feki kwenye stationary fulani.
 
Basi nimeamini watu tunawaza tofauti..
Mimi ninachojua yule jamaa sio mzima wa akili .
Yaani walifanya mistake ya kumpa chizi mic
Katika zama hizi ambazo Jiwe anahofia kutukanwa hata kwenye social media tu, wasingeweza kumpa mic kichaa. So ile haikuwa mistake. Well prepared in advance
 
Tukio liliandaliwa Kishamba sana. Maana hata mtiririko was maswali na majibu ilionesha kila kitu koliandaliwa.. Jamaa jakuwa kichaa ila in ulimbukeni was walioandaa scene.. Kama na muelewa ataelewa namaanisha mini..Yuki aware hakuna ajira mpya na ndio kilio kwa vijana wengi..aliyeulizwa ni mtu wa usalama...mkuu aandaliwa kuzika malalamiko ya ajira...wahitimu wanaosaka ajira wanaonekana kama vichaa sasa.
 
Hapo kwenye Conclusion, Ukiangalia kwa jicho pembuzi kama ndivyo wanavyo amini CCM wako sahihi. Makazini na mtaani tunakutana na wasomi wengi sana wa ajabu ajabu. Kwa sie wenye ofisi binafsi inatubidi wakati mwingine tuajiri kwa vigezo vingine nje ya elimu na kununua vyeti.
Hali ya wasomi wetu ni mbaya wala tusipepese macho kwenye hili
 
Hata mimi nilishitukia ile ni clip. Vinginevyo sasa hivi tungeambiwa yupo chini ya ulinzi kwa kumdanganya mheshimiwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya mambo yanashangaza sana, hata kama kapangwa, kwa nn asifubdishwe kwa makini nini cha kusema? Huenda akawa mgonjwa wa akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…