Gov. Ndullu na Msajili Mafuru: Tunajifunza nini?

Jambo linapopotoshwa kwa kuropoka hadharani njia nzuri ni kulitolea ufafanuzi kwa njia ile ile! Impact matters..
Ni kweli...ila kumbuka ukiwa mteule yakupasa kutii ya mteuaji wako. Mh raisi alisema juzi wakati anaongelea suala la machinga kuwa,hao anaowateua kwanza huwa hawajui kama watateuliwa,kwa hivyo wanatakiwa wafanye kazi kulingana na maelekezo ya wakuu hao maana wao ndo wanajua nini watanzania wanahitaji.
Ukiamua kupingana naye ni sawa lakini tafuta platform yako,usitumie ya kwake!!!
Mafuru yawezekana statements zake ziko sawa ila angesubiri ajiuzuru kwanza ndo aseme hayo.
 
even myself I knew it kwamba Mafuru na Gov Ndulu wanaweza tumbuliwa and may be case yao ikawa 1 but najiuliza, hivi gov. Ndullu yeye ni moja kati ya watu walioidhinisha pesa ile kuwekwa kwenye hiyo FDA, rais akagoma and then ukiwa nwachumi wenzio Arusha (bankers) mwandishi anakuuliza hilo swali ukiwa na wachumi wenzio, hivi alipaswa ajibuje!?
Kwa hilo swari lako ndo utaona hata mreta mada anatamani taalum ya kitu flani iwekwe uvunguni itumike siasa uchwara kama ile ya chinga juzi... Na yuko so excited waiting tz ya viwanda while anajua kwa siasa tuifanyao it will take us 100 yrs kuifikia tz ya viwanda.
 
Nisome tu vizuri mkuu, nimeuliza (kwa mtazamo wa mleta uzi) Ndullu kaulizwa na mwandishi wa habari kuhusu ile FDA (kumbuka yeye nae ni member wa ile bodi ilivunjwa) atoe comment yake, Ndullu yupo mbele ya Wachumi wenzie (bankers) na rais ameisha take action against body and Ndullu being a member of the dissolved board; hivi alitakiwa ajibuje zaidi ya alichokisema!? Binafsi sioni jibu linguine zaidi ya lile alilolitoa Ndullu, tafsiri za jibu lile kila mtu anaweza kua nayo.
 
Ni kweli...ila kumbuka ukiwa mteule yakupasa kutii ya mteuaji wako. Mh raisi alisema juzi wakati anaongelea suala la machinga kuwa,hao anaowateua kwanza huwa hawajui kama watateuliwa,kwa hivyo wanatakiwa wafanye kazi kulingana na maelekezo ya wakuu hao maana wao ndo wanajua nini watanzania wanahitaji.
Ukiamua kupingana naye ni sawa lakini tafuta platform yako,usitumie ya kwake!!!
Mafuru yawezekana statements zake ziko sawa ila angesubiri ajiuzuru kwanza ndo aseme hayo.
Mkuu, ni vizuri tukajifunza kutenganisha siasa na facts.. tukiendekeza hawa wanasiasa tutalishwa matango pori kila kukicha nao wakipata political mileage zisizokua na msingi, Kwa mfano kuvunjwa kwa ile bodi ya TRA kuna tija gani kama wale wajumbe wanaoingia kwa nafasi zao wako pale pale? Unawezaje kutuaminisha watu wanagawana interest ya fixed deposits wakati transaction za mabenki yote zinaangaliwa na serikali hiyo hiyo kupitia BOT? Kwangu mimi Mafuru ni shujaa
 
kama mkuu anapenda akae na wasema kweli,ambao mungu anawapenda,na sio wanafiki ambao wanamficha,basi akae na mafuru na ndulu,na awape wigo mpana wa kumshauri.

ningekuwa mimi ningewasogeza karibu kabisa wakawa wananifanyia uchambuzi pale ninapoletewa masuala mazito ya kiuchumi niyatolee kauli,awe hata msgauri wa rais kuhusu sekta ya mabenki,ni mtu aliyeiva.

Hii tabia ya kumkusanyia "ndiyo mzee" team rais,haimpi changamoto ya ubongo,akae na critical thinkers ambao,kama wanajadili zao la pamba,korosho,wachimbaji wadogo,makazi holela,elimu ya juu,viwanda vidogo,hakika wawe na uelewa wa nchi mikononi mwao,na rais aibuke na uamuzi makini.

wasaka tonge,team "ndio mzee" wakae mbali
Umenyoosha sawia mkuu!
 
Masanja

Nimemsikiliza Mafuru, sijaona alichokosea katika suala la FD (tizama/sikiza kuanzia dk 44). Habari za magazeti zilikuwa twisted na "wapinzani" wa Rais (kwa maoni yangu). Sehemu pekee ambayo pengine ndio inaweza kuwa ilimkera Rais ni suala la uwepo wa wafanyakazi wa umma wanaolipwa milioni 40 kwa mwezi (tizama/sikiza kuanzia dk 57):

Kwa hivyo, nadhani katika hayo ya kujifunza (kwa nyongeza) hasa katika hii regime ni nguvu ya media na namna ya ku deal nayo.
 
Wengine sie Bosi akikukera basi una kinukisha na kuanza mbele kwa mbele kwani tunaamini kazi ni kazi haijalishi iwe serikalini, private au kujiajiri....yote maisha
 
Msemaji ni mmoja Mkuu wa Nchi alikwisha liongelea sana swala la Pesa za Serikali kuwekwa FD kisha Serikali kukopa tena Pesa zake yenyewe kwa Riba kubwa.

Hakuna uwazi kwenye hiyo Riba inakwenda mfuko gani? Inaingizwa Hazina ipangiwe upya?

Cheo ni Dhamana ni kweli kwa sasa aliyepewa Dhamana ni Magufuli na CCM yake, akiboronga 2020 wananchi watampiga chini.

Mafuru na Ndulo wamemkosea Adabu Mkuu wa Nchi nadhani hata Ndulo muda wake wa kustaafu umefika siyo kwamba amemstahi.

Magufuli yuko Sawa ktk hili.
 
Mkuu, ni vizuri tukajifunza kutenganisha siasa na facts.. tukiendekeza hawa wanasiasa tutalishwa matango pori kila kukicha nao wakipata political mileage zisizokua na msingi, Kwa mfano kuvunjwa kwa ile bodi ya TRA kuna tija gani kama wale wajumbe wanaoingia kwa nafasi zao wako pale pale? Unawezaje kutuaminisha watu wanagawana interest ya fixed deposits wakati transaction za mabenki yote zinaangaliwa na serikali hiyo hiyo kupitia BOT? Kwangu mimi Mafuru ni shujaa
mkuu samora10, hata mimi kama umefuatilia mada tofauti tofauti humu JF,zmepingana sana na hiyo ya ulaji wa interest na ndo maana kama umesoma vzr nlichoandika ni kuwa " Yaweza kuwa Mafuru alikuwa sawa" lakini tatizo ni kwamba, alipingana na bosi wake mbele ya hadhara huku akijua nafasi yake hiyo alokuwa nayo ni huyo bosi wake ndo alimtunuku....kumtoa kwenye nafasi hiyo wala hakuitaji kikao cha kumjadiri.....angejitoa kwanza kwenye nafasi hiyo halafu akaruka nae kwa kumpinga hata kama ni kwenye mkutano wa hadhara......
 
Back
Top Bottom