Gov hatimae yatoa ubani kwa wafiwa Arusha! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gov hatimae yatoa ubani kwa wafiwa Arusha!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 15, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wakati Jeshi la Polisi Makao Makuu nchini ikitoa taarifa ya kutetea hatua iliyochukua kuua waandamanaji, serikali imetoa ubani wa kiasi cha shilingi 10 millioni kwa familia mbili zilifiwa na marehemu hao huku kila familia ikipata kiasi cha shilingi 5 millioni.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira wakati alipoitisha mkutano na vyombo vya habari katika ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Arusha akiongozana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Arusha sanjari na viongozi wa dini mbalimbali.

  Tamko hilo la serikali linakuja wakati maelfu ya wakazi wa Arusha na miji ya jirani jana walijitokeza katika maombolezo makubwa ya watu wawili waliofariki kwa kupigwa risasi na polisi katika maandamano ya Chadema yaliyofanyika Januari 5 mwaka huu.

  Akizungumza katika mkutano huo, waziri huyo alilitolea ufafanuzi suala la Chatanda ambalo limekuwa gumzo hapa nchini na kusema ya kuwa mbunge huyo kutoka mkoani Tanga alikuwa ni mpiga kura halali katika uchaguzi wa umeya wa Arusha.

  Waziri huyo alifafanua ya kuwa mara baada ya wajumbe kutoka Chadema kuwa na mashaka juu ya uhalali wa Chatanda Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha alifanya jitihada za kutaka kuthibitisha uhalali wake kupitia ofisi ya bunge na tume ya taifa ya uchaguzi ambapo vyombo hivyo vilimthibitisha kuwa mjumbe halali.

  Hatahivyo,waziri huyo alidai kuwa CCM ina utaratibu wake wa ndani wa kuwaelekeza wabunge wake ni wapi wakapigie kura hivyo kwa suala la Chatanda ni mojawapo ya maelekezo ya chama chake wapi alipopangiwa apige kura.

  Akizungumzia tukio lililotokea mkoani Arusha waziri huyo alisema ya kuwa serikali kwa ujumla inasikitishwa na mauaji yaliyojitokeza mkoani Arusha huku akidai kuwa mkoa wa Arusha ni msingi wa uchumi kwa taifa kutokana na biashara ya utalii.

  Hatahivyo,waziri huyo alipoulizwa swali na waandishi wa habari kuhusu hatua ya kurudiwa kwa uchaguzi wa umeya wa Arusha kama matakwa ya wengi, kiongozi huyo alishikwa na “kigugumizi” na kusema kuwa hawezi kutamka uchaguzi huo urudiwe au hapana.

  Katika hatua nyingine, waziri huyo aliwaomba radhi waandishi wa habari kwa niaba ya serikali ambao waliopokea kichapo na wengine kushikiliwa na jeshi hilo na kisha kuamriwa kufuta picha za matukio na kusema kuwa serikali inajutia kitendo hicho kwani inaheshimu uhuru wa habari.

  http://www.darhotwire.com/home/news/2011/01/14/gov_hatimae_yatoa_ubani_kwa_wafiwa_arusha.html
   
Loading...