Wakati huyu mnyambo G. Begumisa Blandes alikuwa anasoma Seminary ya Kilutheri, Morogoro darasa moja na mkubwa (baba mmoja mama mmoja) na walikuwa marafiki sana, sisi tulikuwa Kilakala Sec. Pili, sote mimi naye ni wabunge wa CCM sasa na niliwahi kwa muda mfupi kuwa mkazi pale jimboni kwao Nyakakika, Karagwe. Namfahamu kiasi tokea hapo mpaka sasa.
Nakubaliana na waliosema kuwa uwezo wake ni mdogo sana. Darasani kwao alikuwa miongoni mwa watu wachache wenye vituko vingi na (wabovu) wa mwisho kimasomo.
Hili lilijulikana kwani alishindwa mitihani ya shuleni kwao kuendelea na masomo yake (ingawa alikuwa anajisingizia kuwa mgonjwa) hadi kusababisha kulazimishwa kurudishwa nyuma yaani badala ya kumaliza na mkubwa wangu mwaka 1986 yeye pekee darani kwao ilibidi abaki hapo Seminary na kumaliza 1987 kwa kusaidiwa na mwalimu mzungu mmoja alikuwepo hapo hadi wakawa wanamtania kuwa ni mtoto wa mzungu. Ushahidi angalieni hata CV yake kwenye hiyo site ya Bunge alisoma miaka mitatu badala ya miwili A level. Tena ieleweke wazi kuwa pale seminary A level alikuwa anasoma HLD (History, Literature and Divinity (Bible knowledge), hii ilikuwa combination ya watu dhaifu kiakili tena walikuwa wachache sana pale shuleni kwao; mara nyingi ni wale walioingia na Div. III au IV kutoka form IV. Bahati kwa credit nzuri ya hiyo Bible na kidogo History ndizo nadhani zilimbeba kuingia mlimani akachukuwa hiyo LLB nako kwa kujikongoja sana.
Huyo mwalimu wao mzungu kama bado yuko hai leo, anaweza toa machozi huko aliko akisikia kuwa huyu Blandes anaweza eti kuwa miongoni mwa wana Kamati au Tume maalumu zinazohusika na maadili na uongozi wa Bunge kama ya tuhuma za rushwa na ile ya sakata la Jairo ambazo zote amekuwa mjumbe.
Ni bayana kwamba Begumisa ni mwanasheria mbabaishaji kutokana na huo huo uwezo wake mdogo kiakili na anatutia aibu Wabunge wa CCM kwa kuwa mlaghai. Novemba, mwaka jana kadanganya Bunge kuwa alipita kukusanya maoni juu ya rasimu ya sheria ya marekebisho ya katiba; kwamba wananchi wamemtuma ipite kama ilivyo, ushahidi ni hansard ! Sitashangaa kama anajihusisha na rushwa pia.
Hata uchaguzi wake ulipingwa sana hivyo akatangazwa chini ya ulinzi mkali sana kwa mwendo wa haraka kama ilivyotokea kwa rais Kibaki.
Ijulikane kuwa hata ndani ya CCM tumo tusiowakubali watu wa namna hii maana wanatuchafua na tunataka mihimili yote ya dola iwe makini kumfanyia vetting mtu yeyote ili afahamike vyema tabia na uwezo wake toka alipozaliwa kama anafaa kupewa nafasi kama hizi.