Google watangaza toleo jipya la Android

Joeli

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2011
Posts
4,941
Reaction score
3,417



Jana katika mkutano wakila mwaka na madeveloper uliopewa jina la I/O, kampuni ya Google ilitangaza toleo jipya la android lililopewa codename android m, ambayo inatarajiwa kuchukua nafasi ya android lolipop ambayo iko kwa sasa.
android m ambayo imeachiwa jana rasmi kwa ma developer, itaanza kupatikana kwa watu wote baadae mwaka huu.


kama tulivoona android lolipop ilileta muonekano mpya (material design), android m itajikita zaidi katika usability na stability ya mfumo wa android alisema msemaji wa google bwana Sundar Pichai.

kwa haraka haraka, maboresho yanayokuja kwenye android m ni pamoja na kumruhusu mtumiaji kuzuia au kukubali security permissions kama accessing camera na location access.



pia kutakuwa na maboresho kadhaa katika browser ya chrome, na pia Google wanaleta mfumo wa malipo wa Android Pay ambao utachukua nafasi ya Google wallet.


pia moja ya vitu vya kusisimua ni uwezo wa android m ku support usb type-c ambayo kama tunavyojua inachaji kwa haraka na kwa urahisi, na la kuvutia zaidi ni uwezo wa kuchaji kifaa kingine kutoka kwako.

jina halisi wala version number ya android m haijajulikana (kazi kwenu mabingwa wa kuguess)

tutaendelea kujuzana kadri mambo yanvozidi kunoga, mpaka wakati mwingine,
na sign off,

picha kwa hisani ya : TheVerge
 
App permision wamejitahidi google, atleast watapunguza malware kwenye android
 

Wanatuletea android m ila hadi sasa wapo ambao hata kitkat au lolipop hawajaionja.
 
Sasa wao inawahusu nini mkuu ?
jaribu kufungua upeo wako wakufikiri.

Kama wewe hujatumia windows 8/8.1 na MS waliitoa kwahiyo unataka wasilete windows 10 ?

Mimi nimesema na ndio ukweli, na hatutaki kuwaacha cha muhimu tuwape elimu ili waende na wakati.
 
Wanatuletea android m ila hadi sasa wapo ambao hata kitkat au lolipop hawajaionja.
Hiyo ni kazi ya kampuni ya simu yako sio Google, makampuni ya simu yanazipa update baadhi ya simu zake kulingana na hadhi ya simu na soko la biashara.
 
hv lolipop imemaliza hata mwaka kweli..,??
 
hv lolipop imemaliza hata mwaka kweli..,??

iliachiwa kwa watu wote November 3, 2014. hata hii M itatoka rasmi baadae sana mwaka huu, possibly mwaka utakuwa ushafika
 
Kanunue simu mpya uenjoy latest tech. Simu za android ni ngumu sana kufanyiwa updates za OS kama WP au Iphone.

hapa ndio utaona tofauti kati ya tecno na simu (za bei kubwa) wakati tecno utaishia toleo iloilo, hizi zingine utaweza kufaidi update za matoleo mengine bila kununua hardware mpya
 
hapa ndio utaona tofauti kati ya tecno na simu (za bei kubwa) wakati tecno utaishia toleo iloilo, hizi zingine utaweza kufaidi update za matoleo mengine bila kununua hardware mpya

Tena hayo matoleo mengine ni hadi zile flagships au zile simu zinazotolewa kama official phones.

Galaxy hawezi kuweka room kwa device zake zote zipate updates mfano galaxy j selfie
 
Kanunue simu mpya uenjoy latest tech. Simu za android ni ngumu sana kufanyiwa updates za OS kama WP au Iphone.

Natumia Sony nishaletewa updates siku mingi sana.

Soon baada ya kutolewa huko kwao namin niliipata.
 
Kanunue simu mpya uenjoy latest tech. Simu za android ni ngumu sana kufanyiwa updates za OS kama WP au Iphone.
Umenena vyema mkuu, karibia OEM wote wa Android OS wamekuwa wagumu kutoa update kiasi kwamba wanatulazimisha kununua simu mpya ili kupata features mpya za Android OS, Yaani ni kero na mwaka huu lazima niwakimbie Android
 
hapa ndio utaona tofauti kati ya tecno na simu (za bei kubwa) wakati tecno utaishia toleo iloilo, hizi zingine utaweza kufaidi update za matoleo mengine bila kununua hardware mpya
Mkuu hebu watoe akina tecno na na wenzie wengine tuje kwenye OEM wengine unaowaamini wewe, kila likiingia toleo jipya la Android wamekuwa wakitoa update kwa simu chache sana hasa flagship ambazo si kila mtu ana uwezo wa kununua, angalau Google wenyewe wamekuwa wakijitahidi kutoa update kwa simu zao zote kwa sababu hawana utitiri wa simu
 
Its a good release. The tech preview is out for Nexus 5, 6 and 9.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…