Google maps

Kilangi masanja

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
4,194
4,550
Hello habari wanajukwaa.
Natumaini ni wazima wa afya njema.Bila kupoteza mda naomba niende kwenye mada. Ninauhitaji mkubwa wa kujua matumizi /kujifunza kwa kina jinsi ya kutumia Google map kwa kina ila sijui pa kuanzia .Kifaa ninachotumia ni simu aina ya xiaomi redmi 7 .
Napenda kujuzwa kwa kina mfano napotaka toka point a kwenda be pasi na msaada wa mtu nafanyaje ili kuwezesha haya yoote kupitia gugo map?
Kifupi sitaki idea nahitaji darasa kamili .Asanteni wadau .
 
Google Map ina uwezo wa kukuelekeza kwa njia ya sauti(English) eneo unaloenda kutoka eneo ulilopo kwa sasa.

Japo inaweza kukupoteza vile vile(nitakuelezea sababu).

google map uses.PNG


Kama unaenda eneo ambalo hulijui na una usafiri binafsi basi google map inaweza kuwa msaada mkubwa kwa sababu ya features zifuatazo.

1. Ina uwezo wa kutambua njia fupi kati ya nyingi kuotka eneo ulilopo hadi mahara unapotaka kufikia.
Kufanikisha hili unatakiwa ufuate hatua zifuataze.

- Washa GPS yako na data kwa pamoja. Mimi hapo GPS ipo off so hilo sio eneo langu halisi. Hivyo ili kupata eneo lako sahihi GPS inapaswa iwe ON.

- Fungua google map.
- Kwenye sehemu ya kusearch, Ingiza eneo ambalo ndio destination yako.
- Chini kuna sehemu imeendikwa DIRECTION, ibonyeze

Google map itaanza kuscan routes zote na kisha kukuonyesha route fupi.

2. Kukuelekeza direction eneo unaloenda kwa sauti.

3. Inaonyesha umbali na kukadilia muda utakaofika eneo unaloenda

Ila Google Map Inaweza kukupoteza kwa sababu updates ya taarifa kwa maeneo mbali mbali inachukuwa mwaka 1 hadi mi3.

Mi binafsi ilishwawahi nitokea nikiwa naenda ofisi flani serikali, kumbe walihama jengo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom