Google I/O 13 San Fran Mwezi wa 5

Google I/O 13 San Fran Mwezi wa 5

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159
​
Google wametangaza rasmi na kusajili washiriki wa mkutano wao mkuu wa mwaka huu unaojulikana kama Google I/O 13. Mkutano huo utafanyika Moscone Center, San Fransisco kuanzia tarehe 15 - 17 mwezi Mei. Kwa sasa nafasi za usajili wa kushiriki zimeshajaa na hivyo usajili umeshafungwa rasmi. Miongoni mwa mambo mbali mbali yanayofanyika kwenye mkutano huo ni pamoja na kuwaongoza watengeneza apps kwenye masuala mbali mbali ambayo wamekwama au kupata na matatizo. Huenda Google wakazindua Android 5.0 Key Lime Pie kwenye mkutano huo.

​
Mwaka jana washiriki wote wa Google I/O walizawadiwa Nexus 7 na Nexus Q za bure, ingawa Google hawakuuza tena Nexus Q kutokana na matatizo ambayo hawakuyaweka wazi, Nexus 7 ndio ilitokea kuwa mfalme wa Tablet za 7" kwa mwaka 2012. Pia Google hutoa gajeti zao mpya katika mkutano huo ambapo mwaka huu bidhaa inayotarajiwa na kusubiriwa kwa hamu kubwa ni Google Glass.

Mambo mengine yanayofanyika katika Google I/O ni pamoja na Code labs ambapo developers wa apps hupata msaada mkubwa kutoka kwa wataalamu wa Google. Pia kuna Developers Sandbox; hapa watengeza apps hupata nafasi ya kuonyesha apps zao mpya na mambo mbali mbali ambazo zina mambo ambayo sio ya kawaida waliyoyaingiza.

​
Kwa upande wa simu na tablet haijajulikana kama Google watatoa simu au tablet mpya, hata hivyo kuna uvumi kwamba huenda kampuni iliyonunuliwa na Google (Motorola) itatoa X Phone mwaka huu, ingawa hakuna uthibitisho wowote kuwa X Phone itatoka kwenye mkutano huo.

Google I/O 13 itakuwa na jambo jipya ambapo Google wameandaa mikutano midogo midogo mbali mbali katika ofisi zao kwenye miji mingine kwa wanaopenda kushiriki lakini hawawezi kusafiri kwenda San Fransisco. Vile vile mkutano huo huandamana na viburudisho mbali mbali baada ya nyakati za mikutano kwa muda wa siku tatu. Mkutano huo huonyeshwa moja kwa moja kwenye Youtube.

Tiketi za kuingia kwenye mkutano huo zimeuzwa $900 taslimu, isipokuwa wanataaluma tu ambao tiketi zao zimeuzwa $300. hivyo ukweli ni kwamba Nexus unazopewa bure huwa umeshazilipia kwenye tiketi ingawa kwa watengeneza apps huapata faida nyingi za mafunzo mbali na gajeti za bure. Iliyopo chini ni ratiba kamili ya Google I/O 13

​
Chanzo: Gajetek Habari: Google I/O 13 San Fran Mwezi wa 5​
 
millah mzee wa google.

Mkuu nexus haijawah kua mfalme wa 7 inch. Yupo mfalme mmoja tu amazon kindle fire hd.
localytics-global-android-tablet-share-640x408.png

piga hesabu hapo 33 ya 56 utaona nexus bado
 
@Cheif-mkwawa Kindle Fire ziko 3 tofauti (Kindle Fire, Kindle Fire HD na Kindle Fire HD 8.9, Nexus 7 iko moja tu, Kindle zimeanza kutoka mwaka 2011 nexus imetoka kwenye Google I/I 2012. QUITE UNFAIR COMPARISON.

Na pia ufalme wa Nexus 7 upo kwenye specs (ubora) na sio kwenye sales. Ilikuwa mfalme kwa sababu it was the first 7 incher kuwa na Quadcore processor!

Halafu Table yako haiendani na hoja yangu, sikusema mfalme wa Android nimesema MFALME WA 7".Angalia hii table haisema 7" Android Tablets inasema Android Tablet kwa hiyo hii inaingiza 10.1 kama vile Galaxy Tab, Galaxy Note 10.1 na Asus Transformer Prime. Imejumuisha 8" na 8.9" kama vile Kindle Fire HD 8.9 na Motorola Xoom Media Edition.

halafu hapa kuna poor presentation of Data, where is Chindia (China and India), 1.2 bilion na 1.1 billion poeple markets respectively)? yaani Spain imetajwa kwa jina na 2% ina maana China imechanganywa kwenye others kwa vile ina chini ya 2% market share. I will never believe that!
 
Wala uspate shinda kindle ana 33 na nexus ana 8 so hapa tunacalculate hiviii.

33+8=41

percentage ya nexus 7
8/41x100=19.5 so kindle zinakua 80.5

hii ina maana katika kila tablet 100 zinazonunuliwa na watu za nexus na kindle za kindle zinanunuliwa 80 na za nexus 20.

So kindle ni mara 4 zaidi ya nexus

haya katika hio asilimia 80 toa 8.9 inayobaki still ni kubwa kuliko nexus. Gape ni kubwa sana bwana millah kiasi kwamba huwezi kataa.

Hio 59 ya us ukija hio 41 ilobakia samsung tu ana kama 70% so haidi kitu kwa nexus.

Na mkuu usisahau other ni 31% ambayo ni karibia mara 16 ya spain. Hizo nchi zilizotajwa ni maeneo ambayo amazon ana matawi sababu ye ndo leader
 
Kwa kawaida unapoweka Others maana yake kuna wengi ambao hawana kiwango kikubwa (significant amount) hivyo kimantiki huwezi kumchukua mwenye 10% ukamuweka kwenye kundi la others halafu ukamchukua mwenye 2% ukamtaja kwa jina. Ndio nikakwambia hizi data zimekuwa presented very poorly. Unless kama data zina lengo la kupotosha ndio unaweza kufanya mambo kama haya. Kwa hiyo kama China au India zina zaidi ya 2% kwa mfano ina maana aliyetengeza data hizi ana moja kati ya mawili hayo (yaani amelenga kupotosha au hajui kutengeza data)

Usichozingatia ni mambo matatu:

1. Mimi nimesema kwamba ni mfalme wa mwaka 2012, kindle Fire zimeanza kutoka mwaka 2011, kwa hiyo wameuza mwaka mzima kabla ya kutoka kwa Nexus 7, sasa utaweza je kulinganisha gajeti hizi?

2. Kindle Fire ziko tatu: Ni vipi ulinganishe mauzo ya gajeti 3 dhidi ya moja?

3. Kindle Fire zinalenga wanunuzi wa aina mbili 7" na 9" (8.9 to be precise), ni vipi untalinganisha na Nexus yenye lengo moja la kuuza kwa wenye kutaka 7" tu.

Narudia kauli yangu: NEXUS NI MFALME WA TABLET ZA ANDROID ZA 7". SASA LETE TAKWIMU ZINAZOONYESHA KWAMBA KUNA TABLET ILIYOBORA KULIKO NEXUS 7 KWA MWAKA 2012 NA INA UKUBWA WA 7"

Mwisho tunaomba uweke link ya source ya Data ili tuweze kuona ni nini hasa lengo la mwandishi kuleta takwimu hizi. Kwani zinatia mashaka mengi mno. Ukizingatia kuwa pia kuna takwimu kama hizi:

android-tablet-sessions.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom